Ndoa yangu inakwenda kuvunjika naombeni ushauri nifanyeje?

Ndoa yangu inakwenda kuvunjika naombeni ushauri nifanyeje?

Wanawake wanatutesa Sana wanaume pindi mambo yanapoyumba
Sio wote mkuu. Sometimes wanawake wanawatesa kwa sabbu kipindi mlivyokuwa nazo mliwatesa pia. Ninukuliwe vizuri..sometimes. kuna wanaume leo ana pesa. Ana gari kadhaa, nyumba na kila kitu. Anarudi nyumbani saa nane and akiulizwa anasema mimi mwanaume sihojiwi. Mwanamke anakuwa wa kulia na kupeleka kesi za usaliti, vipigo kutoka kwa mwanaume. Anaambiwa vumilia ndoa ndo ilivyo. Kama huyu mwanamke hana Mungu moyoni kwamba anatakiwa asamehe na kumuachilia mume wake usitegemee atasamehe jumla. Atatulia tu. Anaanza kujipanga taratibu. Anainuka na yeye kiuchumi. Akiweza kusimama vizuri..shetani anakudondosha wewe uliekua unamtesa.

Mwanamke anaanza kuzitoa karata zake sasa. Unaanza kuona mke wangu kabadilika. Kumbe mwenzako hakusamehe matendo uliomfanyia miaka nane,sita nyuma. Na hatasema analipiza. Anafanya vitendo dhidi ya maneno. Kuna wanawake wamelizwa na kuumizwa na wanaume sana na yote kisa madhaifu yao. Hata kuongea sana kwa mwanamke ni udhaifu. Kwa mwanaume mwenye akili anajua namna ya kudeal na huu udhaifu. Tena chap kwa haraka. Ni kuonyesha msimamo tu mbona kelele zitaisha.

Tumeona mama zetu zamani walivyokua waongeaji. Na walikua wapiga kelele wazuri tu. Saiv nimekua nilijua method mzee aliyoitumiaga mbona mama alibadilika bila kupenda. Lakin ndoa is a matter of sacrifice na akili mingi. Ukienda nayo kwa hisia utachoka mapema. And najua wako wanawake wazuri, wenye midomo yenye staha, vinywa vitamu na busara na hekima. Lakin hawa wanawake hawana chura baadhi yao, wengine si wazuri kwa muonekano, wengne hawana akili ya kimaendeleo sana. Na wengi wenu hamuwataki hawa mnaona mtaoa punguani hamtapata maendeleo.

Niko mkoa flani kwa sasa. Kuna siku nilienda sokoni. Nilijiuliza hawa wanawake wa hili soko wana ndoa? Almost 60% ya wanawake wana vinywa vichafu, ubabe, maneno ya karaha. Kama utanunua nunua kama hutaki kwendraaa. Nilijiuliza sana. No kubembelezwa in short. Basi hata kauli ya kukaribisha mteja..hakuna. lakin wanaume wao wamewazoea it seems.

So wanawake wema wapo najua hilo. Ila sasa wanaume kwa vgezo ambavyo huwa mnavitumia au kuangalia..sidhani kama mtawapata. And pia apandacho mtu ndicho avunacho. Kama umepanda udhalimu sana katika ujana wako, utapewa wa kufanana nae. Mungu sio dhalimu akupe mwanamke uje kumuumiza sana afu mwanamke awe mwema..if you want a good woman in character..jitahidi uwe a good man. Ni mtazamo wangu tu.
 
Mnisamehr ila wanaume wengi wa kichaga ni mazezeta kwenye mapenzi,, mko soft mno na mapenzi hamuyajui,, wanawake wanawapenda kwasababu ya uwezo wa kutafuta ila ule udume hamna mfano ni wewe mwenyewe ndo maana unajiliza hapa
Kama kuna ukweli hivi!!
 
Ngoja nikupe siri ya watu wa kilimanjaro siyo kupenda ndiyo maana ningumu kukuta watoto wa mitaani labda wawe wakuja ila siyo mzawa.Huwa tunajali sana watoto asilimia kubwa
Ila bora hamuwatelekezi mitaani ila mnawatelekeza kwa bibi zao au mama zao. Lakini ajabu hata wanawake wenu pia wanatelekeza watoto🙆🙆🙆🙆
 
Pole Sana mkuu kwa magumu unayopitia.
Mkeo atakuwa Ana mwanaume mwingine sio bure tu.Anza mchakato wa kutoa talaka maama huna jinsi kbsa.
 
Sijawahi kudate mchaga ila nawaona kwa ndg jamaa marafiki,, mh wamepoa km uji wa juzi na wengi walivyo weupe ndo kabisaa
😂😂😂😂😂😂
Ila kweli aisee!
 
Kukunyima papuchi hapa ndo shida kubwa mengine naona hayakuumi kiviile.

Humu wapo wanakudanganya umuache mkeo ulale mwenywe, ujipikie mtoto wako aanze maisha mapya.

Usikimbie tatizo tatua tatizo kwa kutafuta kazi nyingine kama hiyo haikulipi.
 
Screenshot_20230126-154445_Gallery.jpg
 
Jitahid ku solve mkuu , ikishindkn mchukue mwanao ishi nae jitahd kumuhudumia mwao hato maliza miez 3 atakuomba tuu mrudiane.
 
ETI UNA OGOPA KUACHANA NAYE KWA SBB YA MTOTO!! JE UNA JUA WEWE PIA NI MTOTO WA WAZAZI WAKO? anza kujiangalia wewe kwanza!!

kama uko 'smart' anza kutengeneza mazingira ya kupata ushahidi utakao kuja kuutumia mahakaman.
 
Shida ni hiyo pesa yake hataki muitumie wote au ni huo unyumba?
 
Kuna promo nyingi zinaendelea hapa Jf kupinga watu kuishi kwny ndoa,na watu kuowa na kuolewa.

Mambo ya ndoa na familia yajadiliwe kweny ngazi za familia sio mitandaoni.
 
Mwanamke akifanya hivi unafukuza pasipo mijadala wala kuomba ushauri

1. Akiku-cheat
2. Akiwa mshirikina au mchawi
3. Akikunyima unyumba bila sababu ya msingi au anakupa kadiri anavyojisikia.
Mwanamke lazima aelewe kuwa wewe sio mtoto Mdogo. Aelewe kuwa Wewe ni Mumevna mwanaume.

Unapofukuza MTU Kwa Makosa hayo usifikirie mambo ya itakuwaje, fukuza.
Mambo ya Watoto aking'ang'ana muachie.

Vijana WA siku hizi mmekuwaje, unang'ang'ania Watoto umekuwa Mama Yao.
Baba hang'ang'anii Watoto.
Watoto na Mama Yao ndio wanatakiwa wakung'ang'anie.

Kama kuna Mali, mwambie achukue anazoona zinamfaa, kama utapenda Haki gawaneni pasu Kwa pasu.
Ushapata Watoto Wawili wanatosha, Mwanamke kajichanganya mwenyewe, fukuza akupunguzie mizigo.

Ishi Maisha yako Kwa Raha,
Kwa Ulimwengu wa sasa Kwa Wanawake tunatafuta Watoto, ukishawapata Basi.
Unaweza soma huu mwandiko ukajisemea mwamba huyu hapa! Kuuumbe mtu akikujua vizuri anaeza jizarau adi ajiue
 
Kuna promo nyingi zinaendelea hapa Jf kupinga watu kuishi kwny ndoa,na watu kuowa na kuolewa.

Mambo ya ndoa na familia yajadiliwe kweny ngazi za familia sio mitandaoni.
Alafu kwa hili wimbi limekuja kwa kasi la ushoger sjui linachangia, haiwezekani mtu hata hajawai kuoa afu anasema hakuna kuoa!! Inamaana anaolewa yeye
 
Back
Top Bottom