Ndoa yangu inateketea

Ila pia jamaa akubali kutumika, ndio uanaume
 
Solution ni kuwa na mwanamke ambaye anakupenda,hela ni mwarobaini wa muda mfupi tu zikiisha na yeye anakimbia
 
Duuuh!
Kati ya vitu huwa sielewi ni kwanini wanawake tunafanya kazi, hivi kama kazi unayofanya haiwezi kusaidia familia yako ni ya nini?

Mwanaume filisika ujue tabia ya mkeo. Ifike mahali tuelewe kwanza maana ya ndoa kabla hatujaziingia. Tusioe na kuolewa tu eti kwasababu umepata muolewaji na muoaji.

Pole kwa kuumwa mkuu na masahibu unayoyapitia. Hebu jitahidi upate japo kanyumba ukachukue familia yako. Ila itabidi mkae chini mzungumze kwa marefu na mapana kuhusu mstakabali wa maisha yenu.
 

Aiseee!
 
Ukiachwa achika kaka.Achana nae. Kubali muachane na upate talaka yako. Maisha lazima yaende. Si kakuacha mwenyewe hakika ninakuambia utabarikiwa sana katika kila unafanya na utapata mke mwema.
 
Mwache aende mkuu japo ni ngumu kuhandle hali hiyo.
Chukua watoto uishi nao,hapo kwako itakuwa rahisi sana wewe kumsahau yy.halafu pambana kuzisaka kwa namna yoyote ile ili wanao wawe katika furaha tu.
Mwanamke akikutamkia hakutaki hilo ni jambo la kushukuru mungu sana tena sana.
Naamini kama watoto ulikuwa unaishi nao vizuri na walikuwa wanakukubali basi jua hawawezi kukusumbua kuhusu mama yao.

Mfano mimi mwenyewe
Ndoa yangu ya miaka 8 niliivunja mwaka huu mwezi wa pili.baada ya maugomvi yasiyoisha ndani kila siku.nikabaki na wanangu wawili mkubwa miaka 7 na mdogo miaka 4.

Nini nilifanya?
Baada ya kuachana nae nilifuta mawasiliano yake kabisa na kumblock kila sehem.
Nilitafuta kisimu kidogo na laini yake vipo nyumbani nikampatia namba kama atataka kuwasiliana na watoto apige kule ataongea nao.
Na iko hivyo hadi ninapoandika ujumbe huu.amekuwa akinitafuta kwa namba tofauti na kutuma tena wazee kila mara lakini hii safari haiwezi jirudia tena na tena.na kila namba anayonitafuta nayo yaani ile nikijua ni yy hakuna kinachofuata zaidi ya block tu.

Kwangu nimefanikiwa hili jambo kwa asilimia kubwa sana.kwa sababu....!!!!!

Nilijenga msingi imara kwa wanangu tangu yy akiwepo na nilikuwa naplay part kubwa sana ya baadhi ya majukum pale nyumbani ndio maana hata yy alivyoondoka wanangu hawajawahi kunisumbua mama yao yuko wapi na kwa nini kaondoka?imagine mtoto wa miaka 4 tena wakiume unadhani huo usumbufu ungekuwaje kuhusu mama yake?lakini huyu wangu hajawahi kuniuliza.unajua kwanini?

Yeye akiwa nyumbani anafanya majukumu yake,na mimi ilikuwa nikirudi kusaka mkate nilikuwa nafanya pale alipoishia yy.kuna nguo chafu nafua,chakula bado basi nafanya maandalizi yote na kupika kuna sehemu hapajakaa sawa ndani narekebisha then naendelea na mambo yangu mengine.uzazi wote wa watoto wawili sijawahi saidiwa na mtu hadi kumkanda ni mimi mwenyewe imagine hapo.

Kila siku watoto nilikuwa naamka nao,nawaogesha,niwape kifungua kinywa naondoka nao nawapeleka shule ndio nami naenda kibaruani kwangu.

Haya mimi nimeyaweza sababu malezi yangu sikulelewa kumtegemea mtu bali asilimia kubwa nijitegemee na kazi nyingi za nyumbani kwetu ilikuwa hazichagui wakike wala wakiume mpaka tunakuwa wakubwa.

Bro mambo ni mengi ila mteme huyo vinginevyo utaishi kwa tabu sana duniani hapa.hii vita manabii wenyewe waliopewa hekima na uwezo na muumba waliishindwa sembuse sisi.

Pambana upate hao wanao ukishindwa kukaa nao kutokana na changamoto za kimajukumu basi peleka kwenu hapo upambanie mkate wao tu huyo chap sana unamsahau.

Si lazima tuoe tena hali ya kuwa watoto tayari tunao kama hivi.mbususu mtaani kibao ni sisi tu kuchagua ipi inafaa kwa siku hiyo[emoji23][emoji23]..

MUNGU AKUSIMAMIE KWA KWELI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU UNACHOPITA..
Ila hapo mapenzi hakuna tena zaidi ya mateso kwako
 
Nani anisaidie kumtag Carlos Jakal..jana usiku tulibishana sanaa kuhusu suala la mwanamke kuwa na kipato kumzid mwanamke!ona hata siku haijapita shuhuda amepatikana
Naam.


Usishangae ... Wanawake wangapi wasokua na kazi ,wamewakimbia waume zao???


Wangapi??? Au unajitoa ufaham.



Inshu hapaa ni kupata mwanamke Mwema wa maisha yako, Awe anauchumi mkubwa, awe hana Uchumi, akiwa mwema atakua mwema, akiwa sio mwema atakua sio mwema.

Unataka kuniambia wanawake wote wenye kazi na uchumi wao, wote wana tabia ya kijinga kama yahuyo???????.




Hoja ya jana ilikua... Mwanaume Oa mwanamke hata kama kakuzidi uchumi. Maadam mmeelewana , OA...


Wewe umekomaa, atakudharau, atakufanyaje, sasa hiyo inaonyesha HUJIAMINI.
 
Sasa ndo mwamba kaamua kuoa mwenye kipato na elimu..angalia yaliyomkumbaa.....hapa utabisha tu ila ukwel unaujua,ndo maana hata wenyew hawatak kucomment chochote maana wanajijua
 
mkuu hapo hakuna mke, kubali kuumia Leo ili uwe salama kesho. Pole sana
 
Pole sana.
Hauna la kufanya zaidi ya kupitisha ombi lake kiroho safi kabisa.

Ila kama unaweza jitahidi muonane uso kwa uso kabla ya kufanya huo uamuzi. Najua akifikisha 40 ataanza kukumiss ,muda huo upo na kuku wa kienyeji mmoja mwenye chura ya ukweli unamtafuna hadi mifupa.

Kuwa makini na afya yako. Covid inazingua sana,- unaongea na mtu leo vizuri kabisa kesho unasikia kasepa.

Get well soon.
 
Sasa ndo mwamba kaamua kuoa mwenye kipato na elimu..angalia yaliyomkumbaa.....hapa utabisha tu ila ukwel unaujua,ndo maana hata wenyew hawatak kucomment chochote maana wanajijua
Wee Jamaa kabila gan?? Nadhan wee ni mmoja ya wale wanaoamin. "Ukioa mchaga, atakuua".



Yaan mimi nimesoma na mwananke wangu, tumemaliza chuo, tumepata kazi, tumeoana,... Alafu ulitaka tulipomaliza tuachane kisa yeye ana elimu ? Na kazi pia??


Wee ni mkurya ??


Wewe ni aina ya Wanaume wakoloni, wanaopenda kunyenyekewa , hawapendi wanawake wasonge mbele, yaan wale ambao utasikia. "Usisomeshe mtoto wakike".
 
Njia ipo ambayo ndio itakuwa muarobaini wa tatizo sema inahitaji roho ya kiume....

Labda nikuambie mwanamke wako alianza kuchepuka tu pale wewe ulipoanza kuyumba,na wewe ulikosa kujiamini ndio hapo ulipokaribisha matatizo(sikulaumu sababu hyo Hali inaweza kumkuta yoyote)

Sasa ipo hv mwanamke Ni mdhaifu kwenye kupenda,ikitokea amempenda mtu mwingne jua hawezi akakupenda wewe Tena hata umfanyie nn, tena hv unavyomsumbua sumbua au navyolaumulaumu ndo unazidi kumpandisha chuki...

Fanya hv: kwanza kata mawasiliano nae,(na hapo ndipo pagumu,ila ukiuvuka huu mtihani niamini maumivu yote yataisha)

Pili fanya mipango yako mwenyewe bila yeye kujua au watu wa karibu yenu wasijue lengo Ni yeye asijue wewe mipango yako hata kupitia watu wa karibu
Hii itakusaidia kumbuka huyo jamaa aliependwa na mkeo alimpata kwa kumrubuni mkeo kupitia udhaifu wako...na wanawake wakishapenda Basi jua Siri zote na mipango yako jamaa atakuwa anaambiwa na mkeo

Sasa Basi Mambo aliyokufanyia mkeo yawe chachu ya wewe kuinuka na kupambana sababu mtoto wa kiume asili yake Ni kupambana...kuwa na hasira ya mafanikio

Kwa kumalizia nikujulishe kuwa mkeo atarudi tu,ila msimamo wako utamfanya ajutie Mambo aliyokufanyia hivyo makosa aliyokufanyia usiyasemeseme mbele ya ndugu au jamii maana hao unaowaambia ukihisi wanakufariji ndo hao hao wanakusengenya ukiwapa kisogo....

Tafakari chukua hatua ...

Jah bless
 
Ha Wewe elewa tu kwamba inatakiwa uwe juu ya mwanamke kwa kila kitu..ukitaka kumjua kuwa huyo mke wako anakuvumila kwa sababu eidha mko sawa kielimu ma umemzid kipato..Itokee ufilisike ushindwe kuihudumia familia ata ndan ya mwez mmoja tu,hapa ndo utajua rangi yake halisii ni ipi...mwanamke anaweza kumvumilia mwanamme ambaye hana pesa kwa wik moja tu na siku mojaa..baada ya hapo tarajia kuambulia dharau na kejel za kutosha
 
Mnaambiwa msioe waajiriwa hamuelewi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…