Ndoa yangu inateketea

Ndoa yangu inateketea

Mkeo yuko tayari kuishi na wewe wakati wa furaha tu tofauti na kiapo cha ndoa kinavyosema (Furaha na uzuni, shida na furaha). Hiyo ni kumaanisha kuwa hapo hakuna ndoa maana tayari kiapo kimesha vunjwa.

Anza maisha yako bila yeye. Miaka 35 ni inakuruhusu kuanza upya. Pambana usiku na mchana huku ukimtanguliza Mungu. Ukishafanikiwa mke utapata mwingine pengine mzuri na wife material kuliko huyu wa sasa.

Muhimu usiwatelekeze watoto wako. Kile kidogo ulicho nacho tenga mgao wao.

Japo si kwa umuhimu, ukifuata ushauri huu ambao unaendana na wa wadau hapo juu, siku ukitoboa na mkeo akajua basi atakuja kukupigia magoti yeye mwenyewe na kwa kutumia watu mbalimbali. Usije kubali kumrudisha. Huyu ni sawa nyoka mwenye sumu kali, ushang'atwa mara moja , ya pili hata Mungu atakushangaa.
 
Ningekuwa wewe baada ya kupona ningejikita kwenye mitikasi ya kupata hela. Mbona atarudi mwenyewe tu?

Tatizo la wanawake wengi si wa vumilivu. Anadhani hiyo situation utakuwa nayo kwa maisha yako yaliyobaki....hajui kwamba ni hali ya muda tu mambo yatakaa sawa.

Pole sana ndugu.
 
Kaka pole sana, ila jambo moja kubwa la msingi wewe ni mzima wa afya kabisa hajakuachia kilema.
Halafu jifunze kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Ni vigumu ww kukubaliana na hiyo hali kwasababu wewe hujajiandaa kuachana nae. Ili mradi yeye ndio kataka basi kubali kwasababu huwezi kubadili maamuzi yake.
 
Jitahidi upate hata chumba uwachukue...mengine yatajipa. Usikubali kupoteza wanao

Jitahidi upate hata chumba uwachukue...mengine yatajipa. Usikubali kupoteza wanao
Ni kwel siko tayari kabisa kwa hilo maana hao ndo furaha yangu,pia suala la makazi halikua changamoto sana.ila nivyopata msiba na maradhi ndo hapo mambo yalivurugika.
 
Pole sana Mkuu,
Kitendo cha mke wako kutafuta uhamisho wa kwenda Dar, nyumbani kwao ilipaswa kukupa ishara kuwa kuna jambo baya katika ndoa yenu kwa upande wake...

Mke wako ni mtu anapenda vitu (material wife) na kazi alonayo inampa kiburi.
Na pia familia yake inahusika katika kumshauri vibaya.

Kama kweli unampenda mke wako, bas tafuta mganga wa kienyeji afanye yafuatayo,
1.Amfukuzishe kazi na asipate kazi milele na
2.Amrudishe kwako.

Kila la kheri...
Tatizo waganga nao wezi, hawaaminiki.
 
amesema muachane, shukuru amekua wazi japo unahsijdwa kuyakubali hayo maamuzi, ni vyema ukakubali kuachana usifosi et kuna baya au nn huyo anae anampa jeuri anakuona tu takataka mkuu pigania afya yako tafta kibarua jua mustakabali wa mwanao huyo mwanammke hujazaliwa naye kwamba ujione dunia nzima inakuelemea

yes utaumia lakini ruhusu maumivu yakuumize umia mno lakini jua hutakuja umia tena, unapoanguka simama jikung'ute songa mbele na mpaka mtu anakuambia muachane ulishindwa kujiongeza babu??


mke wa ndoa unaumwa haji kukuona na wala hakutafti jua kunaye anayemtafta zaidi yako yupo aliechukua kila kitu chako toka kwake wewe yakubali hayo maamuzi mana ukilazimisha umemkosea nn kitakukuta kitu pengine kikubwa ukaja jutia unao watoto wanakutegemea hao wape kipaumbele zaidi ona tu ulikosea kuoa na umebahatika mtu anakueka wazi kabisa

move on.
 
Back
Top Bottom