Ndoa yangu inateketea

Ndoa yangu inateketea

Habari wana JF wote kwa ujumla, bila ya kupoteza muda naomba kuja kwenye mada husika. Mimi ni kijana wa miaka 35,ndoa yanagu mpaka sasa inamiaka 5 tuu. Katika kipindi chote hichi tumeishi kwa furaha na upendo mkubwa tumebahatika kupata watoto 2.

Mke wangu ni mtumishi chuo kikuu(mwalimu)na mimi ni unga unga mwana pangu pakavu baada ya kampuni fulani ya mawasiliano niliyokua nafanya kazi kufungiwa na serikali kwa madai ya kukwepa kulipa na kuhujumu uchumi hivyo kesi bado iko mahakamani lakini sijawahi kukosa rizik japo kipato changu ni kidogo ila upendo na furaha viliendelea kushamiri.

KUANZA TATIZO
Mambo yalianza kua mabaya ktk ndoa yangu pale tuu mke wang alivyohamishwa kikazi na kuja hapa Dar ktk chuo kikuu fulani mwaka huu mwez 3 hivyo mimi niliendelea kubaki mkoni kwa lengo la kujipanga ili nihamie dar ili niwe karibu na familia yangu.

Ifahamike kua uhamisho wake haukua wa malipo kutokana na yy ndo aliomba kuhamishwa hivyo alipofika hapa Dar alifikia kwao maana yeye ni mzaliwa wa hapa dar.

Baada ya miezi 2 kupita mimi pia nikatoka mkoani na kuja hapa Dar,ila nilifikia nyumban kwetu kwa wazazi wangu (Mkuranga)
Harakaki za kutafuta nyumba zikaanza,kwa bahati mbaya wakati sijalipia nyumba nikafiwa na mzazi wangu(baba) chakushangaza mke wangu hakuweza kufika msibani kwa madai ya kukosa ruhusa kazini.

Sikua na neno maana bado nilikua kwenye majonzi,baada ya msiba kumalizika nilinza kujisikia homa kali na kulazwa hospitali,baada ya vipimo niligundulika ni Covid 19,

Mungu alisaidia nikaruhusiwa na kuendelea na matibabu nyumban. Wakati naendelea na matibabu mawasiliano na mke wangu yalikua ya tabu sana,simu za zilikua hazipaikan kwa madai mtoto wetu mdogo ameharibu simu yake hivyo ilinibidi niwe namtafuta mama mkwe kuongea na mke wangu

Hali ya kimawasiliano ilizidi kua mbaya zaid kadri siku zinavyozidi kusonga mbele,akawa hanitafuti,mpaka mimi nimtafute yeye, upendo wake kwangu ulikua umepungua sana kwangu. Maana hata kunijulia hali imekua vigumu kwake. Kibaya zaid alinza kufuta account namba yake ya wasapu na kuwa online kupitia Facebook nilivyomuuliza mbona nakuona online ushanunua simu nyingine?alinijibu kua ni ya ndugu yake wanaishi karibu pia namjua huyo mtu.

Nilimuomba namba ya simu anayoitumia ya huyo ndugu yake akanipa. Chaajabu sasa nikipiga ile namba anapokea muhusika wa ile simu na ananimbia yy yuko mbali kidogo na mke wangu.

Hii hali ilinishangaza sana kwan mda ambao nachat na mke wangu Facebook ndo mda huo nimepiga simu baada ya yy kunipa hiyo namba na kaniambia ndo anaitumia kwenye hiyo simu,

Niliendelea kuvumilia hii hali kwakua sikua na jinsi maana bado naendelea na matibabu. Hapa juzi kanitumia ujumbe kupitia Facebook anasema tuachane yy amechoka na maisha ya ndoa hivyo anahitaji kua single,haoni faida ya kua kwenye ndoa. Kwa kwel moyo wangu wote ulikua unawaka moto kwa maumivi makari sana

Kwakua bado naumwa halafu nakutana na changamoto kama hii. Ilinibidi nimtafute kwa kumpigia simu kupitia kwa mama ake akampa simu nikaongea nae.

Nilimuuliza kwan kipi kibaya ambacho nimekufanyia mpaka umefikia maamuz hayo ya kutaka tuachane?alinijibua kua yy amechoka na kudharauliwa hapo kwao maana inaonekama kama mimi nimemdamp tuu hapo kwao,

Nilimuuliza kwan hujui hali yangu ya kiafya kwasasa? Akanijibu kua anajua ila hayo ndo maamuzi aliyaamua kwan kichwa chake hakiko sawa,pia kazin kwake pia hajapandishwa mshahara hivyo hayuko sawa. Baada ya kuniambia hiyo alinikatia simu.

Ifahamike kua kipindi hiki chote ninachoumwa kaja kuniona mara moja tuu mpaka sasa ni mwez umekata hajaja kuniona.
Na mda huu yuko likizo haend kazin.

Naombeni ushauri wenu na mawazao nini nifanye kuinusuru ndoa yangu?hali yangu kiafya bado haija kaa sawa.ndoa inazidi kuniumiza msaada wenu tafadhali.
Brother pole mi na wewe tupo kwenye same boat! Pitia nyuzi zangu HIV karibuni... Nimeumizwa mpaka Basi na nakuona tu na wewe unatakavyopitia mule mule kama hautakua strong.

Kikubwa fahamu mwanamke akitaka lazima litimie hata ufanyaje... Let her gooo!!! Ukimuomba Mungu anajibu ila si kwa haraka mpaka analolitafuta huyo mkeo limfike
 
Kitu cha kufanya
1. Pambana na afya yako kwanza na usiwaze kitu chochoteee.

2. Kubaliana na hali
Yaani hapa amini kabisaa hauangalii bongo movie ni kweli kabisaa liko kwako.

3. Usijilaumu hata kidoogo
Kwa namna yoyote ile epuka kujilaumu japo sababu zinaweza kuja zenye mashiko.

4. Jiepushe na visasi.
Kwa njia yoyote ile usijidanganye kulipa kisasi aseee. Thamani yako ni kubwa ukilinganisha na ya kwake kwa sasa, hivyo kitendo cha kupata watoto na yeye hiite we ni kidume.

5. Tafuta hela kwa uhuru.
Huyo kasaidia ukombozi wa uhuru nawe tafuta ukomboe kipato chako.

Mwisho kabisa japo si kwa muhimu.
Hivi kimoyomoyo haufurahi kuachwa huru?
Huo ni ukombozi. Ulioa kwa kuwa una kazi kazi imeondoka imeondoka na ilivyokuja navyo hivyo jipange upyaa
 
Asante kaka,nimeanza kuukali uhalisia
 
Daah nimesoma hii ni ya muda imeniuma sana pole sana ila nadhan ulipata muafaka
 
Nashukuru kwa kunifariji mkuu,yaan kumpoteza mtu uliyemthamin na kushea mambo mengi inaumasana
Assert namba moja duniani ni AFYA YAKO, kwa sasa pigania afya irudi kwenye mstari,na hilo ukifanikiwa jikite kuinuka tena kiuchumi. Wallah nakuhakikishia hiyo vita hutaiweza kamwe na hutashinda ukiipigana sasa ambapo afya ni mgogoro na kiuchumi umeyumba... Pole sana..
 
Ukijions una matatizo pitia huku ... ndio utaona ya kwako HAMNA KITU
 
Habari wana JF wote kwa ujumla, bila ya kupoteza muda naomba kuja kwenye mada husika. Mimi ni kijana wa miaka 35,ndoa yanagu mpaka sasa inamiaka 5 tuu. Katika kipindi chote hichi tumeishi kwa furaha na upendo mkubwa tumebahatika kupata watoto 2.

Mke wangu ni mtumishi chuo kikuu(mwalimu)na mimi ni unga unga mwana pangu pakavu baada ya kampuni fulani ya mawasiliano niliyokua nafanya kazi kufungiwa na serikali kwa madai ya kukwepa kulipa na kuhujumu uchumi hivyo kesi bado iko mahakamani lakini sijawahi kukosa rizik japo kipato changu ni kidogo ila upendo na furaha viliendelea kushamiri.

KUANZA TATIZO
Mambo yalianza kua mabaya ktk ndoa yangu pale tuu mke wang alivyohamishwa kikazi na kuja hapa Dar ktk chuo kikuu fulani mwaka huu mwez 3 hivyo mimi niliendelea kubaki mkoni kwa lengo la kujipanga ili nihamie dar ili niwe karibu na familia yangu.

Ifahamike kua uhamisho wake haukua wa malipo kutokana na yy ndo aliomba kuhamishwa hivyo alipofika hapa Dar alifikia kwao maana yeye ni mzaliwa wa hapa dar.

Baada ya miezi 2 kupita mimi pia nikatoka mkoani na kuja hapa Dar,ila nilifikia nyumban kwetu kwa wazazi wangu (Mkuranga)
Harakaki za kutafuta nyumba zikaanza,kwa bahati mbaya wakati sijalipia nyumba nikafiwa na mzazi wangu(baba) chakushangaza mke wangu hakuweza kufika msibani kwa madai ya kukosa ruhusa kazini.

Sikua na neno maana bado nilikua kwenye majonzi,baada ya msiba kumalizika nilinza kujisikia homa kali na kulazwa hospitali,baada ya vipimo niligundulika ni Covid 19,

Mungu alisaidia nikaruhusiwa na kuendelea na matibabu nyumban. Wakati naendelea na matibabu mawasiliano na mke wangu yalikua ya tabu sana,simu za zilikua hazipaikan kwa madai mtoto wetu mdogo ameharibu simu yake hivyo ilinibidi niwe namtafuta mama mkwe kuongea na mke wangu

Hali ya kimawasiliano ilizidi kua mbaya zaid kadri siku zinavyozidi kusonga mbele,akawa hanitafuti,mpaka mimi nimtafute yeye, upendo wake kwangu ulikua umepungua sana kwangu. Maana hata kunijulia hali imekua vigumu kwake. Kibaya zaid alinza kufuta account namba yake ya wasapu na kuwa online kupitia Facebook nilivyomuuliza mbona nakuona online ushanunua simu nyingine?alinijibu kua ni ya ndugu yake wanaishi karibu pia namjua huyo mtu.

Nilimuomba namba ya simu anayoitumia ya huyo ndugu yake akanipa. Chaajabu sasa nikipiga ile namba anapokea muhusika wa ile simu na ananimbia yy yuko mbali kidogo na mke wangu.

Hii hali ilinishangaza sana kwan mda ambao nachat na mke wangu Facebook ndo mda huo nimepiga simu baada ya yy kunipa hiyo namba na kaniambia ndo anaitumia kwenye hiyo simu,

Niliendelea kuvumilia hii hali kwakua sikua na jinsi maana bado naendelea na matibabu. Hapa juzi kanitumia ujumbe kupitia Facebook anasema tuachane yy amechoka na maisha ya ndoa hivyo anahitaji kua single,haoni faida ya kua kwenye ndoa. Kwa kwel moyo wangu wote ulikua unawaka moto kwa maumivi makari sana

Kwakua bado naumwa halafu nakutana na changamoto kama hii. Ilinibidi nimtafute kwa kumpigia simu kupitia kwa mama ake akampa simu nikaongea nae.

Nilimuuliza kwan kipi kibaya ambacho nimekufanyia mpaka umefikia maamuz hayo ya kutaka tuachane?alinijibua kua yy amechoka na kudharauliwa hapo kwao maana inaonekama kama mimi nimemdamp tuu hapo kwao,

Nilimuuliza kwan hujui hali yangu ya kiafya kwasasa? Akanijibu kua anajua ila hayo ndo maamuzi aliyaamua kwan kichwa chake hakiko sawa,pia kazin kwake pia hajapandishwa mshahara hivyo hayuko sawa. Baada ya kuniambia hiyo alinikatia simu.

Ifahamike kua kipindi hiki chote ninachoumwa kaja kuniona mara moja tuu mpaka sasa ni mwez umekata hajaja kuniona.
Na mda huu yuko likizo haend kazin.

Naombeni ushauri wenu na mawazao nini nifanye kuinusuru ndoa yangu?hali yangu kiafya bado haija kaa sawa.ndoa inazidi kuniumiza msaada wenu tafadhali.
Yani unafiwa na baba mzazi mkeo anashindwa kuhudhuria msiba? Baba mkwe ni baba na mwajiri yeyote anamchukulia hivyo so bro sikushauri uendelee na huyo mwanamke maana Hana upendo kwako
 
mkuu pole sana, mambo ya ndoa sometimes amua mwenyewe
 
Kaka kosa kubwa ni kumwacha muda mrefu mkeo kwa wakwe hii inagharimu ndoa nyingi.
 
cha muhimu sana usijevunja ndoa utakaribisha mikosi maishani. Mimi baada ya kuvunja ndoa ilifuata mikosi non stop kila ninachogusa hakiendi kafibia mwaka mzima
 
Maisha ni mwalimu mzuri sana, hana likizo, hachoki kukufunza, wakati wowote unapokasirika, unapokwazika, fungua macho uone, tega sikio usikie kwasababu wakati huo lyf linakuambia jambo, usikivu na utizamaji ni juu yako

Robert Kiyosaki
 
sorry nje ya maada, hivi ni kweli corona inatesa kiasi hicho, kwa sisi tulio vijijini tunaishi kama tupo jerusalem kwa kweli tunasikia tu radioni .
Pole sana mkuu jifunzi kumuacha aende kikubwa tu ushapata watoto ingawa sinauhakika kama na hao watoto ni wako kweli au alikubambikizia ila ishi kwa kuamini kuwa tulizaliwa mara moja na tutakufa mara moja , piga moyo konde wewe ni wathamani zaidi ya huyo mke wako, Taraka ni jambo la muhimu kwa maisha yako ya baadaye, Bwana Yesu akuponye ninakuombea
 
Wanawake tunadanganyana sana mwanaume akifilisika
But the future is uncertain Mungu atakupa wa kufanana nae in future pole sana mkuu muache aende
 
Wadau wameshasema mengi,ila kwa dhani nimechukua sekunde 30 kufumba macho na kuomba Mungu akupe afya na ukakutane na mkono wake.All the best
 
Back
Top Bottom