Ndoa yangu matatani baada ya mke wangu kudai nimemdhalilisha

spanerboy

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2020
Posts
697
Reaction score
1,526
Wadau naombeni ushauri wenu.

Niko kwenye hali ngumu sana ya ndoa yangu na sijui nifanye nini tena. Nimemkosea mke wangu kwa namna ambayo imefanya ajisikie kudhalilika mbele ya wafanyakazi wenzake. Maneno yamesambaa sana, jambo ambalo limemuumiza zaidi kuliko nilivyodhani.

Nilishaomba msamaha kwa unyenyekevu mkubwa na nikamwambia niko tayari kurekebisha makosa yangu, lakini amekataa kabisa kunisikiliza. Ameniblock kila sehemu, hataki mawasiliano yoyote na mimi, na hata watu wanaojaribu kumuomba anisamehe hawapewi nafasi. Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba amenihukumu bila hata kunipa nafasi ya kueleza upande wangu.

Najua kosa linaweza kuwa limevunja imani yake na siwezi kumlazimisha anisamehe, lakini bado nampenda na sitaki ndoa yangu ivunjike hivi hivi. Kwa sasa najiuliza nifanye nini — nimwache kwanza apoe kimya kabisa, au niendelee kutafuta njia ya kumuonyesha kuwa najutia kweli?

Naombeni ushauri wenu wadau, hasa waliowahi kupitia hali kama hii. Nifanye nini ili nisiharibu zaidi mambo?
 
Mpe muda atulie na hakikisha huendelei kumkwaza kwenye maeneo mengine ya mahusiano yenu.

Kama ulimdhalilisha kwenye umma wa watu, tafuta namna ya kumsafisha mbele ya umma pia na siyo kumuomba msamaha sirini peke yake.

Poleni kwa changamoto!
 
Wadau naombeni ushauri wenu.
Niko kwenye hali ngumu sana ya ndoa yangu na sijui nifanye nini tena. Nimemkosea mke wangu kwa namna ambayo imefanya ajisikie kudhalilika mbele ya wafanyakazi wenzake. Maneno yamesambaa sana, jambo ambalo limemuumiza zaidi kuliko nilivyodhani.
Nilishaomba msamaha kwa unyenyekevu mkubwa na nikamwambia niko tayari kurekebisha makosa yangu, lakini amekataa kabisa kunisikiliza. Ameniblock kila sehemu, hataki mawasiliano yoyote na mimi, na hata watu wanaojaribu kumuomba anisamehe hawapewi nafasi. Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba amenihukumu bila hata kunipa nafasi ya kueleza upande wangu.
Najua kosa linaweza kuwa limevunja imani yake na siwezi kumlazimisha anisamehe, lakini bado nampenda na sitaki ndoa yangu ivunjike hivi hivi. Kwa sasa najiuliza nifanye nini — nimwache kwanza apoe kimya kabisa, au niendelee kutafuta njia ya kumuonyesha kuwa najutia kweli?
Naombeni ushauri wenu wadau, hasa waliowahi kupitia hali kama hii. Nifanye nini ili nisiharibu zaidi mambo?
Fanya kufunguka zaidi kuhusu kosa lako upate ushauri,.. Au ulilewa Pombe ukachafua hali ya Hewa.?? Maybe
 
Kwanini umdhalilishe mkeo mbele ya wafanyakazi wenzake?
Hata kama alikua kakosea jambo,ungemsemesha akiwa peke yake,

Haijalishi umemdhalilisha vipi au amekukosea kipi,kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi wenzake is more than enough,

Kama huja zaa nae,achana nae,tafuta atakaye kuvumulia kwa kumdhalilisha mbele ya watu.
 
Atakublockluwa badae, akipunguza ghadhabu na hasira. Isije kuwa alikuwa anakutafutia gape akunyooshe maana dunia ya siku hizi ngumu sana kuwaelewa watu. Pole sana mkuu, kaza moyo ( hakuna mambo yasiyo soviwa labda mke awe hakutaki )
 
1. Kosa namba moja ni kwenu wote wawili kusababisha mambo yenu ya ndani yatoke nje ya chumba, hii imenifanya niamini kwamba ndo yenu inaishi zaidi kama cinema na kujikweza nje ya ninyi wawili.

2. Jambo la pili kama mwanaume ukisha muomba mkeo msamaha ndani hakuna sababu ya kuionyesha jamii kwamba ikuombee msamaha, sababu naona nikama hiyo ndoa inasaidiwa zaidi kuwepo na watu wa nje na sio kwa mapenzi yenu.

3. Tatu, una mwanamke mwenye kibri na anaependa sympathy kutoka kwa watu ili aonekane yeye ana power over you.

4. Nne, naona wewe unampenda zaidi mkeo kuliko yeye anavyo kupenda bro.
Ebu fanya mambo mengine kama mke hataki kukisikiliza wewe basi kausha na endelea na maisha.
 
Ulifanya nini hadi wafanyakazi wenzie wajue?bado hujasema vizuri ha

Kwanini umdhalilishe mkeo mbele ya wafanyakazi wenzake?
Hata kama alikua kakosea jambo,ungemsemesha akiwa peke yake,

Haijalishi umemdhalilisha vipi,kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi wenzake is more than enough,

Kama huja zaa nae,achana nae,tafuta atakaye kuvumulia kwa kumdhalilisha mbele ya watu.
Sawa Asante Mungu akubariki
 
Piga chini uyo mtu. Atakusumbua sana ata akikusamehe. Ameshajua weakness yako.

Pili, umeoaje mtu wa mbali. Distance relationship haifanyi kazi. Piga chini.

Tatu, kwenda kazini kwake na viatu vilivyichanika sio kumdharirisha bwana ndio uwezo wako. Piga chiniiiii.
 
Wadau naombeni ushauri wenu.
Niko kwenye hali ngumu sana ya ndoa yangu na sijui nifanye nini tena. Nimemkosea mke wangu kwa namna ambayo imefanya ajisikie kudhalilika mbele ya wafanyakazi wenzake. Maneno yamesambaa sana, jambo ambalo limemuumiza zaidi kuliko nilivyodhani.
Nilishaomba msamaha kwa unyenyekevu mkubwa na nikamwambia niko tayari kurekebisha makosa yangu, lakini amekataa kabisa kunisikiliza. Ameniblock kila sehemu, hataki mawasiliano yoyote na mimi, na hata watu wanaojaribu kumuomba anisamehe hawapewi nafasi. Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba amenihukumu bila hata kunipa nafasi ya kueleza upande wangu.
Najua kosa linaweza kuwa limevunja imani yake na siwezi kumlazimisha anisamehe, lakini bado nampenda na sitaki ndoa yangu ivunjike hivi hivi. Kwa sasa najiuliza nifanye nini — nimwache kwanza apoe kimya kabisa, au niendelee kutafuta njia ya kumuonyesha kuwa najutia kweli?
Naombeni ushauri wenu wadau, hasa waliowahi kupitia hali kama hii. Nifanye nini ili nisiharibu zaidi mambo?
I guarantee you; "Things will never be the same again, hata akikusamehe".
 
Back
Top Bottom