Ndoa za kikristo hazifati maandiko ya kwenye biblia, zinafata sheria za viongozi wa makanisa

Actually Hakuna andiko ndani ya Biblia linalokataza kuoa mke zaidi ya mmoja badala utakuna na Hili andiko

“Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.”
— Kutoka 21:10 (Biblia Takatifu)

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
mbona hujamalizia mstari vizuri, malizia na watakua "mwili moja"

Mwanaume ni mwili moja na kila mwanamke ataekutana nae kimwili, iwe ni kwenye ndoa yenye baraka zake Mungu ama Nje ya ndoa akiwa na malaya, Kwa hio pale mwanaume anapokuwa mwili moja na mke wake bado haiondoi kwake kuwa mwili moja na wake wengine. hata sisi wanadamu tupo zaidi ya bilioni lakini Mungu yupo moja ila kila anaeungana roho yake Mungu hutengeneza roho moja, Ndivyo ilivyo hivi kwa wanawake wengi wakiolewa na mwanaume moja kila moja wao huwa ni mwili moja na mme moja.

Siongei maneno matupu bila maandiko ya biblia 1-wakorintho 6:16

Au hamjui ya kuwa hata yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja, Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.

Mwili mmoja lakini sio akili moja wala roho moja!

Hata hivyo mambo ya ndoa yanaenda kufutika siku za usoni.

Si vijana wa kiume au wakike wataokubali kufungiwa kwenye mahusiano ya kudumu yasiyo na lazima wala tija.
 
Ndoa, kama ilivyo dini ni utamaduni ambao hautaweza kusimama dhidi ya pingamizi za nyakati.
 
Kwani walioa Wanawake zaidi ya mmoja hawana michepuko?
Ishu ni kwamba anaongeza mke kitakatifu ama mchepuko kihuni, mwengine ni lazima aongeze mchepuko hawezi kuongeza mke
 
Ndoa zipo za aina 2 km sijakosea

Km itakua nmekosea pahala naomba kusahihishwa kwa lugha rafiki sio lugha chafu

Ni km hivi kuna ndoa za namna hii

  • Ndoa za kidini aidha kikristu au kiislam
  • Ndoa za kimila au mitala

Sasa hapo ndoa za kidini

Tutaanza kwa wakristu au wakristo, unaruhusiwa kuoa mke mmoja tu na ni marufuku kuachana nae hadi unatenganishwa nae na kifo ingawa wapo watu wanajiondoa kwenye hii ndoa kilazima baada ya kushindwana kabisa

Tukija kwa waislam unaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja yaan kuanzia mmoja hadi wanne ndio kikomo na pia unaruhusiwa kuacha na kuoa mwingine muda wowote unaotaka wewe, ni kuandika taraka na kuacha kesho unaenda kuchagua mwingine unamtafuna ukimchoka unamuacha

Mfano mzuri nna ndugu yangu, yeye ni muislamu ameshaoa na kuacha mara 15 mpaka sasa ana watoto 10 na kila mtoto ana mama yake

Ushaelewa?

Pia kuna ndoa za kimila, hizi ndoa hufungwa kwenye maboma au zinatambulika km Ndoa za bomani, sasa ndoa hizi za kimila ndio kufuru maana hakuna limit ya wake unaostahiri kuoa yaan wewe tu na ukwasi wako na kiborodinda chako km unaweza kuhudumia wanawake 10 chukua 10 waoe wazalishe wahudumie

Ushaelewa?

Kwa hio nahitimisha kwa kusema kwamba, mtoa mada ulitakiwa uhame aidha uhamie uislam au uhamie kwenye mitala yaan ndoa za kimila ili ukaishi unavyotaka wewe maana unaonekana wewe ni mzee tombatomba alimaarufu km kitombi unataka udunge dunge kila papuchi na hata ukipewa 10 kwa mkupuo hazitakutosha, uliza wanaofunga Ndoa za kimila yaan wamejitahidi sana wake watatu yaan hapo amejitahidi na huku sheria za kimila zinasema au zinamruhusu hakuna limit ya wake wa kuoa oa idadi yoyote unayoiweza wewe

Ushaelewa au nianze upya?
 
Kwanza maandiko mengi yanakandamiza wanawake. Halafu mjue Biblia kuna vitabu vingi tu havijaandikwa kwenye Biblia.
Km vitabu gan? Emu vitaje

Mimi najua wakatoriki wanatumia vitabu 73 ila waprotestant, wasabato, na wengineo wanatumia vitabu 66 tu sababu vitabu 7 wamevikataa hawavitumii
 
Nimekuuliza swali huko nyuma kuhusu kauli yako kwamba mwanaume kuoa wake wengi ni umalaya,

Nakuuliza upya tena, Kina Musa walikuwa malaya ??
Mkuu,hapa utashambuliwa sana,imani ya mtu katika dini fulani inaathiri sehemu ile ya ubongo inayoathiriwa na uraibu wa madawa ya kulevya..so una mlima wa kupanda ili watu wakuelewe.
Mimi nilishangaa sana kuja kusikia kwamba Italy ni nchi ya tatu kwa low rates za ufungaji ndoa.Waliotuletea haya mautaratibu,wao wenyewe yamewashinda huko!!
 
Hadi sasa sijaona kanisa linalofata maandiko kama yalivyo kwenye biblia, sheria zinazofatwa ni za viongozi wa makanisa zikiwemo sheria za utesaji za kulazimisha mapadre wasifanye sex maisha yao yote, ndizo hizi sheria iliwafanya kina Dokta slaa wakimbie upadri, waliobaki ndio hawa wengi wenye watoto wa siri mitaani na lundo la kesi za kulawiti watoto wa kiume
Uzi wako nimeupenda na nasema uko sahihi. Watu wakibisha wabishe tu maana ni haki yao. Maandiko yanasema siku za mwisho watu watawalazimisha wenzao wasioe!!
 
Sikuona haja ya kuandika kwa kurefu, by the way mkuu sijaelewa point yako hapa. Unamaamisha ndoa za kikristo hazifuati maandiko? Personalky nadhani ndoa zinafungwa kwa kufuata maandiko lakini wanandoa wanashindwa kutimiza maagizo yaliyotolewa kwenye maandiko ikiwa ni pamoja na kubunja viapo vya ndoa, kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, nk.
Unaonekana mgumu sana kuelewa, point ya mleta mada ni kwamba Suala la mke mmoja ni suala la kanisa wala si Mungu aliyetoa maagizo mwanaume kuoa mke mmoja, mleta mada akatoa mfano wa mtume Mussa alikuwa na mahusiano ya karibu na mungu lakini bado alikuwa na wake wengi.
 
Hata ibrahim alikuwa na wake wengi, hata Solomon aliyebarikiwa hekima alikuwa na wake wengi.

Viazi watakuja kusema "oooh hizo habari za agano la kale, tupo agano jipya sasa"

So Km agano la kale halina maana, habari zake ziondolewe kwenye mafundisho ya kanisa now.
 
Hizi ndoa za kikristo zimefikia mahala sasa tunaweza kuziita ndoa za kisheria kwasababu watu wanaona mahakamani kuna unafuu kuliko kufata sheria za ndoa za kikristo.

Usijidanganye kizazi hiki kwamba mke mwema anashushwa na Bwana, mwanamke unaweza kumchunguza mwaka mzima mkiwa kwenye uchumba na ukaona ndiyo hapa nimepata "Wife material".

Muoe sasa uone timbwili lake na makucha aliyoficha, hutakosa kuona rangi yoyote. Kiburi kitaanza kwa jeuri ya ndoa akiona kwamba wote mpo sawa, maana sheria za viongozi wa kanisa zimekubana ugandane naye mpaka kifo na huruhusiwi kuoa mke mwengine.

Maandiko yapo wazi kabisa huwezi kumuacha mpaka kifo ama afanye uashareti nje ya ndoa, lakini hakuna sehemu wamekataza kuongeza mke! Kuhusu kuoa wake wawili hapa ndipo tulipoingizwa cha kike hasa kwetu Waafrika.

Watu wanakuja na utetezi wa mistari ile ya kila mwanaume awe na "Mke wake", hivi nitoe mfano tu mtu ana wake watatu;

~ Mke wa kwanza sio "Mke wake"?
~ Mke wa pili sio "Mke wake"?
~ Mke wa tatu sio "Mke wake"?

Hata kwa mwanaume mwenye mke moja, naye huyo moja ni mke wake.

Yesu pia aliongelea tu kuhusu kutoa talaka hakuzungumzia chochote kuhusu kukataza kuongeza mke. Wakati huo aliokuwepo kulikuwa na wa Israel wengi tu wenye mke zaidi ya mmoja kama mababu zao akina Musa walioleta Amri 10 za Mungu.

Kuna hii hoja nyingine ya "Mwili moja" inatafsiriwa vibaya ili kuendana na sheria za viongozi wa makanisa wanaobana mwanaume asioe mke wa ziada.

Mwanaume ni mwili moja na kila mwanamke ataekutana nae kimwili, iwe ni kwenye ndoa yenye baraka zake Mungu ama nje ya ndoa akiwa na malaya. Kwahiyo pale mwanaume anapokuwa mwili moja na mke wake bado haiondoi kwake kuwa mwili moja na wake wengine.

Hata sisi wanadamu tupo zaidi ya bilioni lakini Mungu yupo moja ila kila anaeungana roho yake, Mungu hutengeneza roho moja. Ndivyo ilivyo hivi kwa wanawake wengi wakiolewa na mwanaume moja, kila mmoja wao huwa ni mwili mmoja na mme moja. Siongei maneno matupu bila maandiko ya biblia 1-wakorintho 6:16;

"Au hamjui ya kuwa hata yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja, Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye."

Madhara yake siku hizi wakristo wengi hawana muda na sheria za viongozi wa makanisa wanakimbilia kuyamaliza mahakamani ili kuoa mke mwengine.

kumbana mwanaume kuwa na mke moja matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona michepuko imekuwa kawaida sana siku hizi.
Baada ya kuandika "maoni yako binafsi" hebu sasa jenga hoja zako kwa kunukuu maandiko kifungu kwa kifungu. Mwanamume mwenye mtazamo wa aina hii hatoshi kuwa mume wa ndoa. Acha kufuata mkumbo huku huelewi ni nini unachokitaka. Watu wenye mitazamo ya hovyo namna hii ndio mnaizika taasisi ya ndoa na kufanya ionekane ni ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia.

Nasikitika kukuarifu kwamba hujajua kweli bado, jibidiishe katika kumtafuta Mungu kwa kusoma neno lake nawe utaishi.

Amina
 
Hata ibrahim alikuwa na wake wengi, hata Solomon aliyebarikiwa hekima alikuwa na wake wengi.

Viazi watakuja kusema "oooh hizo habari za agano la kale, tupo agano jipya sasa"

So Km agano la kale halina maana, habari zake ziondolewe kwenye mafundisho ya kanisa now.
Mwanangu umeongea point, hamna agano jipya bila agano la kale
 
Hata ibrahim alikuwa na wake wengi, hata Solomon aliyebarikiwa hekima alikuwa na wake wengi.

Viazi watakuja kusema "oooh hizo habari za agano la kale, tupo agano jipya sasa"

So Km agano la kale halina maana, habari zake ziondolewe kwenye mafundisho ya kanisa now.
Tutajie wake wa Abrahamu sie viazi.
 
Hizi ndoa za kikristo zimefikia mahala sasa tunaweza kuziita ndoa za kisheria kwasababu watu wanaona mahakamani kuna unafuu kuliko kufata sheria za ndoa za kikristo.

Usijidanganye kizazi hiki kwamba mke mwema anashushwa na Bwana, mwanamke unaweza kumchunguza mwaka mzima mkiwa kwenye uchumba na ukaona ndiyo hapa nimepata "Wife material".

Muoe sasa uone timbwili lake na makucha aliyoficha, hutakosa kuona rangi yoyote. Kiburi kitaanza kwa jeuri ya ndoa akiona kwamba wote mpo sawa, maana sheria za viongozi wa kanisa zimekubana ugandane naye mpaka kifo na huruhusiwi kuoa mke mwengine.

Maandiko yapo wazi kabisa huwezi kumuacha mpaka kifo ama afanye uashareti nje ya ndoa, lakini hakuna sehemu wamekataza kuongeza mke! Kuhusu kuoa wake wawili hapa ndipo tulipoingizwa cha kike hasa kwetu Waafrika.

Watu wanakuja na utetezi wa mistari ile ya kila mwanaume awe na "Mke wake", hivi nitoe mfano tu mtu ana wake watatu;

~ Mke wa kwanza sio "Mke wake"?
~ Mke wa pili sio "Mke wake"?
~ Mke wa tatu sio "Mke wake"?

Hata kwa mwanaume mwenye mke moja, naye huyo moja ni mke wake.

Yesu pia aliongelea tu kuhusu kutoa talaka hakuzungumzia chochote kuhusu kukataza kuongeza mke. Wakati huo aliokuwepo kulikuwa na wa Israel wengi tu wenye mke zaidi ya mmoja kama mababu zao akina Musa walioleta Amri 10 za Mungu.

Kuna hii hoja nyingine ya "Mwili moja" inatafsiriwa vibaya ili kuendana na sheria za viongozi wa makanisa wanaobana mwanaume asioe mke wa ziada.

Mwanaume ni mwili moja na kila mwanamke ataekutana nae kimwili, iwe ni kwenye ndoa yenye baraka zake Mungu ama nje ya ndoa akiwa na malaya. Kwahiyo pale mwanaume anapokuwa mwili moja na mke wake bado haiondoi kwake kuwa mwili moja na wake wengine.

Hata sisi wanadamu tupo zaidi ya bilioni lakini Mungu yupo moja ila kila anaeungana roho yake, Mungu hutengeneza roho moja. Ndivyo ilivyo hivi kwa wanawake wengi wakiolewa na mwanaume moja, kila mmoja wao huwa ni mwili mmoja na mme moja. Siongei maneno matupu bila maandiko ya biblia 1-wakorintho 6:16;

"Au hamjui ya kuwa hata yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja, Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye."

Madhara yake siku hizi wakristo wengi hawana muda na sheria za viongozi wa makanisa wanakimbilia kuyamaliza mahakamani ili kuoa mke mwengine.

kumbana mwanaume kuwa na mke moja matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona michepuko imekuwa kawaida sana siku hizi.
Changamoto yako ya ndoa haiwezi kubadilisha maandiko ya biblia wewe pambana na hali yako!

So kweli kuwa ndoa za Kikristo hazifuati maandiko ila tunapokutana na Changamoto kwenye ndoa huwa tunatafuta maandiko ili tujifariji tunapoyakosa ni lazima tulalamike kama mtoa madam anavyofanya.
 
Mkuu, uhusiano wako na Mungu ni personal i.e hauhitaji mtu mwingine akupe approval.

Wewe kama umesoma biblia na ukaona hakuna sehemu inakataza ndoa za wake wengi, fanya uoe.

Hata kwenye Uislamu kuna baadhi ya madhehebu yanatakaza ndoa za wake wengi.
 
Back
Top Bottom