Tunaposema maandiko ya biblia hayajakataza ndoa yenye mke zaidi ya mmoja ila ni maelekezo ya viongozi wa makanisa muwe waelewa.
haya sasa, hivi chukulia kijana wa kikristo mwenye miaka 25 kaoa halafu anaenda kukutana vitu hivi kwenye ndoa
-mke kaamua awe na mtoto mmoja tu baada ya hapo atatumia kinga za kuzuia mimba
-mke hana uwezo wa kuzaa (tasa)
-mke hana hamu tena ya tendo, labda mara 1 kwa mwaka.
-kapatwa na ugonjwa ama ajali isiyomruhusu kufanya tendo.
-mke kapandishwa cheo anahamishiwa bukoba kikazi wakati mme wake yupo dar na kukutana ni mara 1 kwa mwezi.
yaani hapo hakuna kuongeza mke na ndoa kuvunjika ni mpaka kifo ama umfumanie anachepuka (kitu ambacho ni aibu kwetu wanaume ).
suluhisho ni lipi hapo kwa hizi sheria za viongozi wa makanisa (sio maandiko) waliombana mwanaume awe na mke mmoja ?
Nilishamwambiaga Shetani sitachepuka hata itokee mke wangu ataninyima unyumba milele.Maana niliona wengi wanachepuka kwa kisingizio cha kunyimwa tendo la ndoa.
Hivyo mkuu,elewa siku zote ni mpango wa Shetani kuharibu ndoa za watu.Endelea kumuomba Mungu akupe msaada.na pia endelea kuwa mwaminifu ktk ndoa yako