NDOA: Zamani vs Siku hizi

hilo swala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo,ila itawezekana?amegundua kuwa hakupendi na anao uhuru wa kukuacha
utamzuiaje?

....Hapo hakuna ujanja Mkuu inabidi tu utoe uhuru wa mtu kuchukua 50 zake ili kuepusha balaa zaidi.
 
Reactions: Mbu
Klorokwini mwanasheria na hachewelewi kutafuta sababu akikirwa.
 
Reactions: Mbu
haswaaa babu hata maandiko yanasema tuishi nao kwa akili na zaidi tufikirie mara mbili zaidi yao kabla ya kufanya mamuzi......
 
hilo swala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo,ila itawezekana?amegundua kuwa hakupendi na anao uhuru wa kukuacha
utamzuiaje?

...lol...hilo la kuachana kwa vijisababu vya kijinga kwakweli halina ubishi kabisa...
ila kama Excellent alivyotanabahisha, ana uhuru wa kuacha/kudai kuachwa...utamzuiaje?!

..nahisi uhuru wa kuachana umekuwa mkubwa sana kwa kizazi hiki, au mwaonaje?
hili nalo limechangia wajameni, japo RITA nao wamekurupuka kusikojulikana wamekuwa wakali siku hizi,
hauwezi kupata cheti cha kuachana mpaka mpitie baraza la usuluhishi!!!
 
....Hapo hakuna ujanja Mkuu inabidi tu utoe uhuru wa mtu kuchukua 50 zake ili kuepusha balaa zaidi.
basi ndoa hazitadumu ila sijui itakwaje,mi naona cha msingi ni watoto kuwa na malezi kwa pande zote(baba & mama)ila
inaonekana kuna ugumu
 
Reactions: BAK
hilo swala la kuishi kwenye ndoa linatakiwa liwepo,ila itawezekana?amegundua kuwa hakupendi na anao uhuru wa kukuacha
utamzuiaje?

Just like that???

Kama ingewezekana na pia isiwe ni kuingilia uhuru wa mtu wa namna hiyo, tungependa kujua undani kabisa.....

If he or she made a mistake kwa kudhani kwamba anamependa huyo aliyekubali kuoana naye, leo anapomwacha, atamrudisha kwenye hali yake ya zamani? .....Kwa nini anajifikiria yeye peke yake?? She already ruined someone's life!

I can only understand kama kuna kosa kafanyiwa au tatizo jingine la msingi (medical or psychological)!!
 
Reactions: Mbu
Rushwa inaweza kupenya,mbali na hivo utawezaje kuishi na mtu ambaye sheria imembana ila hakupendi na anajilazimisha kuishi na wewe?au ndo kusema kukaa nimekaa ila moyoni nimesimama.
 
Uhuru umekuwa mkubwa na rate ya kuu-abuse pia imekuwa kubwa pia...Kama RITA wanataka usuluhishi itasaidia.

Binafsi ukinambia kuwa tuachane kwa sababu hunipendi tena lazima nikufungulie kesi ya madai....Huwezi kuharibu maisha yangu halafu ukaondoka salama kiasi hicho!!
 
Reactions: Mbu
babu DC kwa wtoto wa dotcom ukiwa realistic wanakuona umepitwa na wakati na ni mnoko.

...hahahaha, mueleze huyu mzee bana....haelewi dunia imebadilika!

hahahaha, wallahi leo nimesadiki kwamba wewe mkuu hujui yanayoendelea kwenye jamii yetu ya kisasa, khaaa?
mtu haoni hata haya kutamka hadharani aliolewa kuwafurahisha wazazi!...au asafishe jina tu naye kaoa/kaolewa!
e bana kuna vituko huku kwenye dot.com acha tu...

Achana na hao, unakuta mtu hamtimizii mkewe mahitaji yoyote, si mali wala hali...kwa kifupi amemtelekeza mkewe na familia, ila linapokuja suala la kumkabidhi mkewe haki yake ya kuachana, anakwambia yeye hatambui hilo neno kuachana. Wat iz zat sasa?
 
haya mambo mengine wakati mwingine yanakuwa km hangover ya ulevi ,haiwezi kuwa sababu tosha ya kuvunja kitu kikubwa km ndo lkn.
 
Rushwa inaweza kupenya,mbali na hivo utawezaje kuishi na mtu ambaye sheria imembana ila hakupendi na anajilazimisha kuishi na wewe?au ndo kusema kukaa nimekaa ila moyoni nimesimama.

Sidhani kama kuna sababu ya kumlazimisha mtu ila kama anataka kuvunja ndoa bila sababu ya msingi basi alipe gharama ya uamuzi wake....Alipe fidia ili aone uchungu kwa uamuzi aliouchukua!

Hii iitasaidia watu kufikiria mara mbili mbili kabla ya kukimbia kula viapo vya ndoa!
 
Reactions: Mbu
leo anapomwacha, atamrudisha kwenye hali yake ya zamani? =asiyekupenda haogopi kukukalisha kwenye magogo.
Kwa nini anajifikiria yeye peke yake??=mana hakupendi tena.
 
Rushwa inaweza kupenya,mbali na hivo utawezaje kuishi na mtu ambaye sheria imembana ila hakupendi na anajilazimisha kuishi na wewe?au ndo kusema kukaa nimekaa ila moyoni nimesimama.

kama ilivyo rushwa ya kufanikisha mume anapata cheti chake cha kuachana, mke anaweza vile vile kuongeza dau hiko cheti kisitoke,...unafanya mchezo na u dot.com wewe?
 
kesi utashinda,ataendelea kuishi na wewe ila atamegwa,halafu wewe ndo umpe talaka
 
leo anapomwacha, atamrudisha kwenye hali yake ya zamani? =asiyekupenda haogopi kukukalisha kwenye magogo.
Kwa nini anajifikiria yeye peke yake??=mana hakupendi tena.

Ngoja wanasheria waje watusaidie,

Ila sheria ya ndoa nasikia ya mwaka 1971 anampa mtu uhuru wa kukataa kutoa talaka...Mtu wa namna hiyo simpi talaka na atakayemuoa namufungulia kesi mahakamani!!

Kama alienda kwa mganga wakamwambie aolewa kwanza ili kuondoa mikosi na baada ya hapo arudi kwenye biashara zake, ...hapo inabidi mtu abebe mzigo wa maamuzi yake!!
 
Imetokea amerubuniwa na kigogo au mwenyewe uwezo,sidhani kama hapo atasikia maumivu
 
Reactions: Mbu
basi ndoa hazitadumu ila sijui itakwaje,mi naona cha msingi ni watoto kuwa na malezi kwa pande zote(baba & mama)ila
inaonekana kuna ugumu

...Pia labda kuanzishwe kitengo cha kuzinusuru ndoa ili kabla ya kuachana kuwe na watu tuseme kutoka baraza la usuluhishi ili kwa kipindi cha miezi 12 wajaribu kuwasuluhisha wahusika ili kuinusuru ndoa husika, hili labda litapunguza idadi ya ndoa zinazosambaratika kila mwaka.
 
kesi utashinda,ataendelea kuishi na wewe ila atamegwa,halafu wewe ndo umpe talaka

Kaka mtu wa namna hiyo huwezi tena ukwa na amani naye...Ila mkiamua kuwa kama wanyama, basi huwezi kujua in advance nani atashinda....Mie niko tayari kuijaribu hiyo marathon!

Talaka hapati, na ataendelea kukaa kwangu na kutii masharti ya hapo nyumbani.....!!
 
Reactions: Mbu
kama ilivyo rushwa ya kufanikisha mume anapata cheti chake cha kuachana, mke anaweza vile vile kuongeza dau hiko cheti kisitoke,...unafanya mchezo na u dot.com wewe?
Mke ameshinda kwa dau,basi imekula kwake,mme akishinda mke atarudhi nyumbani ila sarakasi na skendo kama kawaida.
 
Ni vigumu kuzuia ndoa kuparaganyika...Tatizo ni sababu za ndoa kuvunjika na wingi wa ndoa zinazovunjika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…