Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Vitabu vya historia vinatuambia kuwa kabla ya Hiroshima pamoja na Nagasaki kupigwa na pigo basi walikuwa wameshachapika vya kutosha, yaani kabla ya zile bomu mbili kushushwa kulikuwa na hali mbaya sana ndani ya Japani.
Raia wengi walifahamu kuwa Japani pamoja na Mfalme Hirohito hawatoboi mbele ya hasira ya Mmarekani wa washirika wake. Upande wa Uchumi, wajapani walikuwa wanapumulia respirator, kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa chakula, na maji safi ya kunywa.
Ukipata kukisoma kitabu cha The Rising Sun: The Decline and Fall of the Japanese Empire, 1939-1945, kilichoandikwa na John Toland kama una roho nyepesi utaishia kutoa machozi. Japani alichapika vibaya sana, kiburi na jeuri ambayo Mfalme Hirohito alikuwa nacho, kiliwanyoosha wajapani mpaka wakaimba Hallelujah.
Hofu ilijaa kila kona ya Japani, kipindi hicho wajapani walikuwa kama wapo kwenye Orchestra, wakati waliopo mitaa ya Ginza, Shitamachi, Sumida Toshima pamoja na Shinjuku zilipo Tokyo waliimba kwa sauti moja maumivu makali.
Osaka katika maeneo kama vile, Namba, Umeda pamoja na Higashiyodogawa walikuwa wakiimba sauti zao za majonzi. Kitabu cha Downfall: The End of the Imperial Japanese Empire kutoka kwa Bwana Richard Frank, ndani ya kitabu hiki Bwana Frank anaelezea kuwa mpaka Mfalme Hirohito anainamisha kichwa chini na kukubali kuwa ngoma imekuwa ngumu, lakini huko Yokohama pamoja na Kobe walichezea kichapo heavy, sehemu kama vile; Kannai, Naka-ku, Sannomiya, Motomachi, pamoja na Bandari ya Kobe.
Katika historia ya Japani, kuna jina linalobeba mkusanyiko wa heshima kubwa lakini pia linabeba fuko kubwa sana la hatia, urithi hadhi ya kifalme, na mtu hatari ambapo kwa wao wajapani walimpatia jina la yochui jinbutsu. Ili kumwelewa huyu mwamba lazima tufahamu historia yake; kwa maana ya kuzaliwa mpaka kuingia kwenye jeshi lakini pia ushawishi wake ndani ya serikali pamoja na ndani ya Jeshi, mpaka mshauri wa Mfalme Hirohito.
Kwa majina yake anaitwa Prince Fumimaro Konoe alizaliwa tarehe 12 Oktoba 1891 mjini Tokyo, katika familia ya Konoe, mojawapo ya koo tano za juu kabisa za kifahari (go-sekke) zilizokuwa karibu zaidi na ukoo wa kifalme kwa zaidi ya miaka 800. Hizi hazikuwa familia za kawaida za tabaka la juu; zilikuwa familia ambazo kihistoria zilitoa Regents (Sesshō na Kampaku) – watu waliotawala Japani kwa niaba ya Mfalme.
Kwa ufupi tu, damu ya Konoe haikubeba tu heshima, bali pia urithi wa kutawala kwa niaba ya mamlaka ya juu kabisa ya nchi. Nyakati hizo mtu ukianzisha ugomvi na mwanafamiia kutoka moja ya familia aidha Konoe, Kujo, Ichijo, Nijo au Takatsukasa, basi hiyo kesi yako imekuwa ngumu sana.
Dogo Fumimaro ni kama alianza maisha akiwa mbele ya muda, kabla ya mchezo kuanza tayari alikuwa na goal advantage. Dogo alikuwa akihudumiwa na Kotei Shiyonin wasiopungua wanne, huku zile kazi ambazo zinahitaji nguvu kama kubeba mizigo, kufanya usafi, dogo alipewa watu walioitwa Zotei ambao ndio walikuwa vibarua wa familia ya Konoe.
Kukua ndani ya familia ya namna hii kulimaanisha kitu kimoja muhimu: maisha ya mtoto yalikuwa yamepangwa kabla hata hajazaliwa. haikuwa tofauti kwa Konoe ambaye hakukulia katika mazingira ya kuchagua, wala kupewa nafasi ya kuchagua jambo, bali ya alitakiwa kurithi wajibu pekee. Alifundishwa tangu utotoni kwamba Japani haikuwa taifa la kawaida, bali dola takatifu; kwamba Mfalme hakuwa mtawala pekee wala binadamu wa kawaida, bali kiumbe kitakatifu; na kwamba utii haukuwa chaguo, bali wajibu wa kimaadili na wa kiroho.
Alifundishwa kuwa Mfalme Jimmu, hakuwa tu mfalme wa Japani bali alikuwa ana roho na maono ya kimungu, vivyo hivyo alifundishwa kuwa wafalme kama vile Taisho, Ninko, Kokaku, Sakuramachi, Nakamikado, pamoja na Momozono walikuwa ni zaidi ya wafalme wa Japani, walikuwa ni wawakilishi wa kimungu duniani.
Na dogo alimeza yote hayo maana hakuwa na namna nyingine chini ya utawala wa mzee wake **Prince Atsumaro Konoe.
Dogo ni wazi alizaliwa na ule msemo Born with a silver spoon in one’s mouth. Mshua wake alikuwa anaitwa Prince Atsumaro Konoe, alikuwa mwanasiasa mashuhuri sana ndani ya Japani lakini pia Prince Atsumaro Konoe ndio alikuwa ni Rais wa Baraza la Mabwana (House of Peers) kwa wajapani walikuwa wanapewa heshima ya kuitwa jina la Kizoku-in, ambapo ndio lilikuwa ni Bunge la Japani.
Kifo chake cha Januari mosi ya mwaka 1904 kilimfanya na kumlazimu dogo Fumimaro, akiwa bado kijana wa miaka 13 pekee, kurithi nafasi hiyo ya kifahari. Hapo ndipo Konoe alipoanza mapema sana kuishi maisha ya mamlaka, heshima, na maamuzi mazito. Kuingia ndani ya jumba lenye watu takribani 251, dogo alianza kuitwa mheshimiwa kabla hajafika hata miaka 15, janja nadhani ndio anashikilia rekodi ya kuingia bungeni akiwa na umri mdogo zaidi.
Elimu ya Konoe katika Chuo Kikuu cha Kyoto ilimtofautisha na wahafidhina wengi wa kifalme. Kyoto haikuwa tu chuo cha elimu; kilikuwa kitovu cha fikra huru, kulikuwa na mjadala wa falsafa, na tafakuri ya mustakabali wa Japani katika dunia inayobadilika kila sekunde. Konoe alijifunza siasa, historia za kimataifa, na falsafa za Magharibi huku akiwa na ndoto ya kutumia elimu hiyo kuja kubadilisha vitu ndani ya taifa lake. Alivutiwa na mawazo ya utaifa, lakini pia aliona wazi jinsi mfumo wa kimataifa ulivyowabagua Waasia haswa Wajapani.
Mwaka 1919, akiwa bado kijana wa miaka 28 tu, Konoe alipata shavu na kuteuliwa kuwa sehemu ya Ujumbe wa Japani katika Mkutano wa Amani wa Paris baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia. Dogo akiwa na miaka 28 akaingia kwenye ukumbi wa Hall of Mirors. Tukio hili lilikuwa la kihistoria katika maisha yake, kwani alipata kuwa timu moja na watu kama Baron Makino Nobuaki, Chinda Sutemi, pamoja na Saionji Kinmochi ambaye alikuwa Waziri Mkuu wakati huo.
Na kwa upekee kabsa Saionji Kinmochi ndio alipewa jukumu la kumtazama dogo janja na kuwa mwalimu wake, ebu chukua picha yaani mentor wako ni Waziri Mkuu? Tena Kamanda wa Jeshi? Ahh we.
Konoe alishuhudia kwa macho yake mwenyewe jinsi mataifa ya Ulaya yalivyo na madharau huku wakipinga wazo la usawa wa rangi lililopendekezwa na Japani bila sababu yoyote.
Hii ilimwacha na maumivu makubwa ya kisaikolojia: Japani ilishinda vita upande wa washirika, lakini ilikataa kutambuliwa kama ameshinda na kumiliki maeneo ambayo yameshindwa vita, wazo ambalo lilizungumzwa kwa lugha lugha nyepesi sana na Saionji Kinmochi ila Waingereza na Wamarekani wakaona hawawezi kuacha Japani kujiona ameshinda kizembe kwenye vita vya ubaguzi wa rangi.
Na Uingereza aliona ni hatari kwake kwani ndio alikuwa ameanza kushika hatamu kuwaambukiza makaburu roho chafu huko Afrika Kusini.
Uzoefu huu ulimgeuza Konoe kuwa mzalendo mkali, lakini pia mtu aliyekosa imani na diplomasia ya Magharibi, janjaro alikosa kabsa imani na mataifa Uingereza pamoja na Marekani. Ndani yake, wazo la Japani yenye nguvu, inayojitegemea, na inayotawala Asia lilianza kuchukua miziz kuanzia usiku wa tarehe 13 Februari. Hapa ndipo mbegu za sera zake za baadaye zilipopandwa.
Aliporudi Japani, Konoe alichukua rasmi kiti chake katika House of Peers, na kufikia miaka ya 1930 alikuwa tayari mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika siasa za kifalme, baadhi ya wanahistoria wa masuala ya siasa walidai dogo aliondoka na kijiji., ukimpa muda wako azungumze na wewe basi atahakikisha umeelewa darasa.
Masao Maruyama aliwahi kunukuliwa akisema “Konoe alikuwa na sauti ya kawaida ila yenye kubeba uzito sana kwa wawakilishi ndani ya House of Peers”.
Haikuwa kazi rahisi kwake, yaani Dogo aliweza kushika masikio ya watu kama Yoriyasu Arima aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Uvuvi pamoja na Maeda Toshisada aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano. Mwamba Konoe Kuanzia 1933 hadi 1937, alihudumu kama Rais wa House of Peers, nafasi iliyomweka katikati ya mfumo wa maamuzi ya dola, karibu kabisa na Mfalme Hirohito.
Kwa Konoe ilikuwa ni sawa na kumpa dulla ubwabwa maharage na chai ya rangi mchana wa saa saba subiria usingizi tu!
Kitendo cha kuwa kichwa cha House of Peers, Konoe ilikuwa ni GG/+2 kwake, na bado alikuwa anaonekana ni mtu wa heshima, msomi, na mwanasiasa wa daraja la juu asiye na doa lolote la vita. Lakini pia alikuwa tayari amefungwa kikamilifu ndani ya mfumo wa kifalme, mfumo ambao baadaye ungemfanya awe mfungwa wa maamuzi yake mwenyewe bila yeye mwenyewe kufahamu.