Ndoto zinaweza kuwa mawazo yako, ndoto kutoka kwa Mungu, ndoto kutoka kwa shetani, ndoto kutokana na shughuli unazo zifanya
Ndoto ni njia nyepesi ya Mungu kuongea na watu wake, hivyo shetani kaiga hiyo njia ili aongee na watu
Ndoto ni ulimwengu halisi kuliko huu wa mwili, kila kitu kabla hakijatokea katika mwili kinaanzia kwanza rohoni ( ulimwengu wa roho)
Hivyo ndoto ikianza ujue ipo katika ulimwengu wa roho bado tu kutimizika katika ulimwengu wa mwili
Na sio kila ndoto lazima itokee,
Wakat mwingine unaweza jua ni Mungu kumbe siyo, hata shetani anaweza jifanya yeye ni mungu sasa usipo jua unaweza acha tuu
Unapoota ndoto yakupasa kuangalia hi ndoto ni ya kuangalia ni nzuri ama mbaya, mfano umeota labda nimepanda ndege naenda mahali fulani, huwez kemea hii ndoto, sababu ni hatua ya kuvuka mahali fulani. Hivyo ni kumuomba Mungu akufanikishe katika mahali fulani alipo kusudia
Umeota ndoto mbaya, labda mtu kafa, hii ndoto hii si ndoto nzuri halafu baada ya muda mtu anakufa
Kitu kikitokea ktk ulimwengu wa roho ni rahisi kuzuia kuliko kikija mwilini. Utaingia gharama kubwa zaidi
Sisi tumeumbwa na Mungu hivyo sisi ni miungu ya dunia hii, Mungu hawez fanya kazi bila sisi, sababu Mungu ni roho, kadhalika shetani hafanyi kazi bila kutumia mwili wa mtu sababu yy ni roho
Kama sisi tumeumbwa na Mungu na yeye ni Baba yetu, kuwa na uhakika una vinasaba vya uungu ndani yako, ndio maana ukikaa vzr na Mungu, unaweza ukakemea vitu vikatoka sababu Mungu anakaa na wewe ndani yako, unapotembea na yy anatembea unapokaa na yy ana kaa, Mungu anakuwa na wewe kila mahali,
Ni hivi kama umeona katika ndoto, kuwa umekufa, sio kuwa umekufa as kufa mwilini, umekufa rohoni, kila kitu chako kitakufa, unajua mtu akifa hawez miliki chochote, tuje katika hali halisi, mfu hawez ongea, hawezi fanya kazi, mfu anatengwa sababu si sehemu ya binadamu tena mahali pake kaburini, mfu hawezi shika hata pesa, mfu hawezi shirikiana na walio hai, hata pesa itajua huyu kafa hutozalisha kitu, kila kitu kitakufa cha kwako
Mtu aliye hai hachangamani na walio kufa, hata tukupende vipi ukifa tutakuzika tuu, wewe sio sehemu ya walio hai,
Ukiota walio kufa si nzuri pia, na uki endekeza eti nikafanye kama nilivyo waota utaandamwa na hizo roho.za mizimu, walio kufa wamekufa hawarud wakiwa hai,
Tuje mwisho kama wewe ni una uungu ndani yako jua kuwa unaweza kuumba kitu, sema tu ni madhambi yamezidi ndio maana watu wengi hawapo ktk nafasi zao katika ulimwengu wa roho,
Ndio maana kuna watu vinywa vyao vikitamka maneno mazur au mabaya usipo kuwa makini yanakupata yote, maneno ni roho, na roho ndio uzima wa kila kitu, tumia kinywa chako vzr kwa mambo mema, kujibu au kuumba jambo jipya,
Ukinena baya shetani anapata uhalali wa kulifanya liwe halisi, huko juu nimesema kuwa hawez fanya kazi hadi atumie mwili, au maneno yako,
Sasa hata mtu akikunenea neno baya hakikisha unabatilisha hilo neno hapo hapo lisije kukupata
Tuje ktk ndoto, ndoto mbaya una uwezo wa kuibatilisha isitokee
Mungu huwa hafanyi kitu bila kuwaambia watumishi wake kwanza, sasa ni wewe jinsi ya kuomba, ni wewe jinsi ya kulifanya litokee au lisitokee.
Kumbuka wewe umeumbwa na Mungu una uungu ndani yako kama shetani hajakuwahi
Hivyo kitu kikitokea 100%wewe wa kulaumiwa,.kwanini hukuomba? Kwanini hukuzuia kisitokee,
Hakikisha unakaa vizuri na Mungu
Mungu anapenda utii.
Ukimtii Mungu atakufunulia mambo mengi,
Mungu atusaidie tuwe watii mbele zake.
Kuna ndoto za moja kwa moja hazihitaji fasir na kuna ndoto za mafumbo. Hivyo omba kwa Mungu vzr