amakyasya
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 3,480
- 918
Nililala nikaota mtu anasema eti Tanzania imetokana na Tanganyika na visiwa vya Zimbabwe na Pemba nikashangaa sana maana sikutegemea mtu kama yule kwa nafasi aliyo nayo katika mtaa wetu.
Ndoto ya pili niliota jamaa mmoja mtaa wa pili anamuita mwenzie gaidi ili mradi amchafulie kwa wana mtaa asipate uongozi. Baada ya baraza la mtaa kukaa kikao jamaa alishindwa kuthibitisha na hatimaye kuonekana mwehu tu.
Ndoto ya tatu nikaota familia fulani inawakataza familia jirani kwa kuweka ulinzi kwenye nyumba yao wakati wao wana ulinzi kwao masaa 24 na kila mtu mtaani anafahamu hivyo. Sijui lengo lao ilikuwa ni nini.
Ndoto ya nne nikaota mwalimu mkuu wa shule iliyopo kwenye kata yetu anawatangazia walimu na wanafunzi kwamba wanafunzi wanaokaidi amri za viranja wapigwe tu. Nikashtuka.
Ndoto zingine nimesahau, nikikumbuka ntaendelea kuwaletea hapa hapa. Je, wewe uliota nini? Hebu tupe nawewe ndoto yako.