Ajiandae kuota ndoto ingine tu. Ndimu mtalamba sana ila kutapika hamtaacha magufuli mbele kwa mbele mpaka 2020 mwambieni babu kuwa atasubiri sana kwa kuwa hakubaliki kwani ni mchafu. Jicki ambayo DJ na wenzake walimsafisha nayo haikutosha kumtakatisha. Watafute mbinu ingine labda itafaa
kwa upande wangu nahisi laana iliyokuwa juu ya gadafi na hitler inawajia kwa haraka sana, kwasababu kabla hamjaingia kwenye vyeo tulivyowapa mlikuwa wapole, mlipopata mmekuwa na kiburi, dharau na roho ngumu na chungu. ni kwasababu mnajiona mmeshapata.
Gadafi alikuwa na kiburi sana, mavazi yake, kunyanyasa raia, kujilimbikizia utajiri, alikuwa anajiita king of africa. lakini alishushwa hadi korongoni. sisemi kwamba Tanzania itasambaratika kwa vita, bali nasema ata bila vita Mungu anao uwezo kuwasambaratisha ninyi wenye kiburi kwasababu mmenyanyasa nafsi za wengi mkijitumainia nafsi zenu na akili zenu. uhai wenu upo kwa Mungu. hivi, leo hii mkiondoka mtaenda motoni au mbinguni?
swali moja tu, mnajua aliyewapandisha ndiye mwenye nguvu ya kuwashusha? mnajua kuwa mnaumiza mioyo ya watz wanaolia na hawana kwa kukimbilia?mnajua kuwa kwasasa jinsi nchi ilipofikia hata chizi akigombea anaweza kuwaletea challenge? mnajua kuwa watu wanapata shida huku mtaani? mnajua kuwa huku mtaani kuna watu wenye akili kuliko ninyi ambao wanapima kila mnachofanya na wanashindwa kuwaelewa kama mna uwezo kuleta mafanikio?mnajua kuwa mmeigawanya nchi tayari kwa misingi ya ukanda hasa kwa kutumia huyo kijana mdogo anayehitaji msaada wa Mungu? je, mnamtegemea Mungu katika maisha yenu au mnategemea waganga na washirikina, sio washirikina ninyi, hamuendi kwa waganga ninyi?....kama mnaenda, msimtaje Mungu kwenye majukwaa yenu, tajeni mashetani yenu.
mmejikweza juu kuliko hata mlivyotarajiwa, ni kwasababu hamkutarajia katika maisha yenu kama mtafika hapo mlipo, Mungu amewafikisha na mmemsahau. mnaendesha uongozi bila hekima bali milipuko na masifa ili mpate sifa mbele za watu. Mmekwisha kupata thawabu yenu, kilichobaki ni Mungu kuwashusha, na jambo hilo laja haraka sana kama msipotubu.
ajishushaye atakwezwa, ajikwezaye atashushwa. Neno la Mungu latuonya, unyenyekevu tujivike, Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema. Kiburi chenu ndio anguko lenu, na kila mtu duniani atajua kuwa ni Mungu amewashusha. mark my words, labda mtubu na kurudi katika njia sahihi, la sivyo, ninawaonya kwa Jina la Yesu Kristo.