NDOTO: Rais Magufuli kutawala awamu moja tu...

NDOTO: Rais Magufuli kutawala awamu moja tu...

Wana Jf wenzangu......!!

Leo ni mara ya 3 nikitokewa na ndoto kuwa Rais wa JPM atakuwa kiongozi pekee atakayeliongoza Taifa kwa kipindi cha Miaka 5 tu na sababu pekee ni kwamba atapigwa chini katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama chake. Hii ni kutokana na makundi mengi ambayo yameanza kujipanga kwa kutumia mbinu mbalimbali ndani ya chama kwani wengi wao awapendezwi na aina ya utawala anaoendelea nao kwa sasa ndani ya chama na Taifa.

Ni hayo tu nimeona niwashirikishe....!!
Maccm haya majinga hayawezi kumpiga chini, na wala hatuhitaji yampige chini...sisi tutashughulika naye ni suala la muda tu!
 
Ajiandae kuota ndoto ingine tu. Ndimu mtalamba sana ila kutapika hamtaacha magufuli mbele kwa mbele mpaka 2020 mwambieni babu kuwa atasubiri sana kwa kuwa hakubaliki kwani ni mchafu. Jicki ambayo DJ na wenzake walimsafisha nayo haikutosha kumtakatisha. Watafute mbinu ingine labda itafaa
 
And LEAVE my president alone. Mwacheni kabisaaaa anyooshe nchi maana we were descending in a dangerous slope. And winning 2020 election is obvious
 
anavuruga economy na hana clue yupo yupo tu anasimamia fitna kati ya wateule wake na wapinzani.
 
Mtasema sana ila halitakuja. Mlisema jpm hawezishinda ila akashinda. Na wenye ndoto kama wewe walikuwepo na sasa wameshuhudia ni rais wa nchi. Tena sio rais tu bali rais bora africa
 
Kwenda huko. Kwa sasa hakuna makundi kwenye chama. Na pia kati ya maraisi waliotawala tanzania ukiondoa nyerere, huyu ndo anakubalika kuliko wote
Aende wp?.. [emoji1] [emoji2] [emoji23] [emoji23] .
Mchagulie Mji wa kwenda!!!
Acha kuendekeza Mahabaa, tujipe nafasi ya kupenda kufikiria kabla ya kuendekeza Mahaba.

Hitimisha hoja yako kw facts!!!
 
Mi nawashangaa sana watanzania. Tuna rais ambaye africa nzima akigombea urais anashinda. Then nchini kwake anaonekana kituko. Binafsi huwa naumia sana ninapoona mtu anambeza rais. Amefanya mangapi mazuri then mnakuja kumdisqualify kwa vitu vidigo sana. Ikumbukwe yeye si malaika, hivyo anaweza kukosea ama kufanya jambo ambalo wewe ama nyie hamkupendezwa nalo.
Hivyo vizuri tushirikishane mkuu japo tuvijue maana me sija viona
 
Wana Jf wenzangu......!!

Leo ni mara ya 3 nikitokewa na ndoto kuwa Rais wa JPM atakuwa kiongozi pekee atakayeliongoza Taifa kwa kipindi cha Miaka 5 tu na sababu pekee ni kwamba atapigwa chini katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama chake. Hii ni kutokana na makundi mengi ambayo yameanza kujipanga kwa kutumia mbinu mbalimbali ndani ya chama kwani wengi wao awapendezwi na aina ya utawala anaoendelea nao kwa sasa ndani ya chama na Taifa.

Ni hayo tu nimeona niwashirikishe....!!
Ata JK alitabiriwa kama ndoto yako chini upinzani mkali wa EL.Endelea kuota!
 
Swala hilo mzee ngumu hiyo ni ndoto tu na hakuna kitu kama hicho, jamaa anamaliza mihula yote miwili mzee,mimi na wewe inawezekana tusije piga kura lakini wanamama wengi watapiga na wazee wengi tu
 
Yeye ni mwenyekiti na sera ya chama chake ipo kwao wenyewe, hapo tunapiga ngebe tu lakini lazima aendeleee
 
Mi nawashangaa sana watanzania. Tuna rais ambaye africa nzima akigombea urais anashinda. Then nchini kwake anaonekana kituko. Binafsi huwa naumia sana ninapoona mtu anambeza rais. Amefanya mangapi mazuri then mnakuja kumdisqualify kwa vitu vidigo sana. Ikumbukwe yeye si malaika, hivyo anaweza kukosea ama kufanya jambo ambalo wewe ama nyie hamkupendezwa nalo.
Tuambie hayo makubwa alofanya mana wengine hatuyaoni
 
Ajiandae kuota ndoto ingine tu. Ndimu mtalamba sana ila kutapika hamtaacha magufuli mbele kwa mbele mpaka 2020 mwambieni babu kuwa atasubiri sana kwa kuwa hakubaliki kwani ni mchafu. Jicki ambayo DJ na wenzake walimsafisha nayo haikutosha kumtakatisha. Watafute mbinu ingine labda itafaa
kwa upande wangu nahisi laana iliyokuwa juu ya gadafi na hitler inawajia kwa haraka sana, kwasababu kabla hamjaingia kwenye vyeo tulivyowapa mlikuwa wapole, mlipopata mmekuwa na kiburi, dharau na roho ngumu na chungu. ni kwasababu mnajiona mmeshapata.

Gadafi alikuwa na kiburi sana, mavazi yake, kunyanyasa raia, kujilimbikizia utajiri, alikuwa anajiita king of africa. lakini alishushwa hadi korongoni. sisemi kwamba Tanzania itasambaratika kwa vita, bali nasema ata bila vita Mungu anao uwezo kuwasambaratisha ninyi wenye kiburi kwasababu mmenyanyasa nafsi za wengi mkijitumainia nafsi zenu na akili zenu. uhai wenu upo kwa Mungu. hivi, leo hii mkiondoka mtaenda motoni au mbinguni?

swali moja tu, mnajua aliyewapandisha ndiye mwenye nguvu ya kuwashusha? mnajua kuwa mnaumiza mioyo ya watz wanaolia na hawana kwa kukimbilia?mnajua kuwa kwasasa jinsi nchi ilipofikia hata chizi akigombea anaweza kuwaletea challenge? mnajua kuwa watu wanapata shida huku mtaani? mnajua kuwa huku mtaani kuna watu wenye akili kuliko ninyi ambao wanapima kila mnachofanya na wanashindwa kuwaelewa kama mna uwezo kuleta mafanikio?mnajua kuwa mmeigawanya nchi tayari kwa misingi ya ukanda hasa kwa kutumia huyo kijana mdogo anayehitaji msaada wa Mungu? je, mnamtegemea Mungu katika maisha yenu au mnategemea waganga na washirikina, sio washirikina ninyi, hamuendi kwa waganga ninyi?....kama mnaenda, msimtaje Mungu kwenye majukwaa yenu, tajeni mashetani yenu.

mmejikweza juu kuliko hata mlivyotarajiwa, ni kwasababu hamkutarajia katika maisha yenu kama mtafika hapo mlipo, Mungu amewafikisha na mmemsahau. mnaendesha uongozi bila hekima bali milipuko na masifa ili mpate sifa mbele za watu. Mmekwisha kupata thawabu yenu, kilichobaki ni Mungu kuwashusha, na jambo hilo laja haraka sana kama msipotubu.

ajishushaye atakwezwa, ajikwezaye atashushwa. Neno la Mungu latuonya, unyenyekevu tujivike, Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema. Kiburi chenu ndio anguko lenu, na kila mtu duniani atajua kuwa ni Mungu amewashusha. mark my words, labda mtubu na kurudi katika njia sahihi, la sivyo, ninawaonya kwa Jina la Yesu Kristo.
 
~naota kama atapunguza wajumbe wa NEC has a wale ambao anaona wako against ili wale wa kanda wabakie wengi zaidi ili iwe rahisi kufaulu....
 
kwa upande wangu nahisi laana iliyokuwa juu ya gadafi na hitler inawajia kwa haraka sana, kwasababu kabla hamjaingia kwenye vyeo tulivyowapa mlikuwa wapole, mlipopata mmekuwa na kiburi, dharau na roho ngumu na chungu. ni kwasababu mnajiona mmeshapata. swali moja tu, mnajua aliyewapandisha ndiye mwenye nguvu ya kuwashusha? mnajua kuwa mnaumiza mioyo ya watz wanaolia na hawana kwa kukimbilia?mnajua kuwa kwasasa jinsi nchi ilipofikia hata chizi akigombea anaweza kuwaletea challenge? mnajua kuwa watu wanapata shida huku mtaani? mnajua kuwa huku mtaani kuna watu wenye akili kuliko ninyi ambao wanapima kila mnachofanya na wanashindwa kuwaelewa kama mna uwezo kuleta mafanikio?mnajua kuwa mmeigawanya nchi tayari kwa misingi ya ukanda hasa kwa kutumia huyo kijana mdogo anayehitaji msaada wa Mungu? je, mnamtegemea Mungu katika maisha yenu au mnategemea waganga na washirikina, sio washirikina ninyi, hamuendi kwa waganga ninyi?....kama mnaenda, msimtaje Mungu kwenye majukwaa yenu, tajeni mashetani yenu.

mmejikweza juu kuliko hata mlivyotarajiwa, ni kwasababu hamkutarajia katika maisha yenu kama mtafika hapo mlipo, Mungu amewafikisha na mmemsahau. mnaendesha uongozi bila hekima bali milipuko na masifa ili mpate sifa mbele za watu. Mmekwisha kupata thawabu yenu, kilichobaki ni Mungu kuwashusha, na jambo hilo laja haraka sana kama msipotubu.

ajishushaye atakwezwa, ajikwezaye atashushwa. Neno la Mungu latuonya, unyenyekevu tujivike, Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema. Kiburi chenu ndio anguko lenu, na kila mtu duniani atajua kuwa ni Mungu amewashusha. mark my words, labda mtubu na kurudi katika njia sahihi, la sivyo, ninawaonya kwa Jina la Yesu Kristo.
Mabaya ya rais ni yapi. Mniambie labda na mm nitashawishika kutomwamini
 
Back
Top Bottom