Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Shoio jana nilisoma uzi wako saa tano usiku.Nikalala nikaamka saa kumi na nusu kufanya shughuli flani nikalala tena niliota ndoto moja ndefu sana kama ifuatavyo.
Kulikuwa na gharika kama la Nuhu watu wakawa wanasombwa na maji milima ikawa inajaa nyumba zinaanguka mawe yanaporomoka milimani.Mimi nikawa nakwenda upande wa juu hapajafunikwa.
Nikafika mahali watu wanaimba habari za mwokozi YESU kuwa watakao muamini gharika halikukumbi.
Mlango wa kuingilia nikakuta jamaa anasema mtu yeyote anayekula nguruwe atakwama kimiujiza ila mpaka atakaswe kwanza amkubali YESU atapona kufunikwa na maji.Si wongo mimi nilizuiwa mpaka nitakaswe
Ndoto ilikuwa ndefu sana inatisha mno.
Nikajiwa na wazo huenda nilivyosoma habari hizi kwenye huu uzi ubongo ulinasa mkanda ndio ukawa unajirudia
Looh maajabu ya MUNGU kwa binadamu
 
Uko sawa vidudu vya malaria vinatafuna chembe nyekundu za damu hivyo zinapungua ubongo unaweweseka lazima ndoto mbaya sije kujibu mapigo ya ubongo kukosa Oxygen
Aiseee.
Hizi ndoto bana ukizifuatilia kila unapoota shida.
Mie mandoto yakianza tu lazima kwanza nikapime malaria
 
Usiku wa jana nimeota nimepata watoto wawili kwa mke wangu wakitofautia kwa siku moja japo biashara ya kuzaa tushaifunga kitambo.
Mtoto wa kwanza nimeota kazaliwa saa 08:37hours na wa pili kesho yake saa na dakika zile zile. Nikawa nimewabeba wale watoto nikijiuliza na kutaka ushauri kwa watu kwamba hawa watoto niwaite pacha au?
Ndoto hii inaweza kuwa na maana yeyote?
 
Mleta Uzi ukimwambia ndoto ina maana gani anakuambia njoo inbox...Hamna maana ya kuanzisha Uzi sasa....ngoja nije nikuhadithie hukohuko inbox ili unijibu huko
 
Asante kwa somo,ila vipi naota napaa juu sana pia huwa niwapo huko juu kuna kiumbe nisicho kitambu au kukiona vizuri napale kinikaribiapo huwa napaa, nacho hujaribu kunifata ila hakifiki umbali nilipo,hii kitu imekuwa ikijirudia mara kwa mara,nini maana yake mkuu
 
Wakati wa kureply tuangalie urefu wa Uzi unakuta MTU anareply hadi kero
 
Uzi ni mrefu sana angalia namna ya kureply
Mie juzi nimemuota mo nipo nae kwenye Basi tunaenda nae shughukini ila tukashuka wote na akawepo kwenye shughuli ya kusheherekea ila sijui sherehe ya nini ila yakiswazi nikaamka
 
Mleta Uzi ukimwambia ndoto ina maana gani anakuambia njoo inbox...Hamna maana ya kuanzisha Uzi sasa....ngoja nije nikuhadithie hukohuko inbox ili unijibu huko
Itakua anatisha watu ili apate hela ama sio huyu ni mganga wa kienyeji
 
Itakua anatisha watu ili apate hela ama sio huyu ni mganga wa kienyeji
Sitishi watu kaka hii ni mambo ya siri ya mtu hivyo si vizuri kuyaweka hadharani ila waaulize waliokuja inbox kama kuna tatizo lolote wamekutana nalo
 
Nitaleta sehemu ya pili soon
 
Jamani kwa wale wote kwenye shida ya kutafsiriwa ndoto nawaomba waje inbox kwa msaada zaidi
 
Njoo inbox kwa msaada zaidi
 
Njoo inbox kwa msaada zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…