Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Natumai mmeamka vyema. Humu mu wazima wa afya na mambo yako vizuri kwa upande wenu.

Niko hapa kuomba ushauri wa jambo moja. Kuna ndoto moja nimeota leo. Hapa navyoandika nimetoka kuamka nikiifikiria maana yake bila kupata usahihi wa nini inamaanisha au ni ndoto tu ya kawaida.

Nitatumia majina ambayo siyo rasmi hapa. Mimi naitwa juma na nina mpenzi wangu anaitwa Amina. Inaanza tukiwa tumekaa watatu kuna kitu tuna discuss .Na wote ni wanafunzi wa chuo.lakini nyumba inaonesha ni kwa wazazi wangu ndo sehemu iliyokuwa tunafanya hyo kazi.

Lakini ikatokea tumemaliza tulikuwa watatu wanawake wawili na mwanaume peke angu.Baada ya kumaliza kila mtu ilipaswa kuendelea na mambo yake . Lakini ghafla baada ya kutaka kila mtu aendelee na mambo yake nikagundua kwa kazi nayotaka kuifanya mda huo kuna kitu nimepungukiwa .

Na nilichopungukiwa nikakumbuka kuna rafiki yangu mmoja anacho hcho kitu. Kwa hyo anaweza kunisaidia. Nikatoka nje kwa dhumuni la kutaka kumpigia huyo rafiki yangu john ambae anaweza nisaidia hcho kitu. Na huyo john ni mtu wanaefahamiana na huyo mpenzi wangu ambae ni Amina na anamjua kuwa ni shemeji yake.

Baada ya kupiga simu yake ikawa inaita na akapokea mwanamke ambae kwa sauti nilitambua ni ya Amina. Nikashangaa nikamuuliza mbona umepokea wwee simu ya john . Akajibu ameninunulia . Nikaduwaa nikamuuliza kivipi na laini unayo wewe. Hakujibu ikabidi nirudi ndani nilipomuacha kwa sababu nilitoka nje kwenda kumpigia huyo john.

Baada ya kufika ndani ndoto inaonesha naanza kumgombeza kuhusu hyo simu hali ya kuwa sikumbuki mpaka saa hii nilikuwa namuuliza maswali gani. Ikatokea amenijib vibaya. Nikamtoa sehemu nilipokuwa kwa dhumuni la kwenda kuongea vizuri chumbani. Huku akilini mwangu nikiwaza kumnyoosha kwa kitu alichokifanya . Kiukweli kiliniuma sana hcho kitendo.

Kweli chumbani nilifanya nilichokidhamiria kwa sababu nilimpiga mpaka akawa anavuja damu puani, masikioni, machoni na sehemu zingine za kichwa. Nikawa nimepagawa pale sielewi cha kufanya. Ikabidi nimtoe pale nje nakuta ambulance ndo inaingia kumchukua .
Inamchukua na kuondoka nae lakini na gari la polisi linaingia kwenda kusomewa mashtaka ya mauaji. Kiukweli kizimbani inaonesha nahukumia maisha kwenda kuozea jela.

Sasa msaada wenu wanajamvi natumai kuna wajuzi mnafahamu mambo mengi. Nisaidieni nijue ina maana gani hii ndoto. Inaniumiza sana . Nisaidieni jamani nijue

Nitawashukuru sana.
 
Inaonyesha unamuwazia John vibaya kuhusu Amina, acha hizo mambo utakuja kufa bure..jitahidi kuwaza maisha zaidi ya mapenzi kwani nae Amina ana mipango yake pia.
 
Ndoto ni mrejeo wa mawazo yako hakuna sijui nini inamaanisha. Punguza kuwaza ngono na wanawake wanawake.

We tangu lini ambulance ukafungua mlango ukakuta nje, hujapiga simu wala kutoa taarifa ya msaada. Ndoto hazina implication yoyote
 
Ndoto yako ni balaa sielewi mtu unawezaje kukumbuka ndoto kwangu ni janga hua wet dreams tu zinabaki kwenye kumbukumbu nyingine zote zinapotea na kila siku naota
 
FB_IMG_16466380710272486.jpg
 
Kuwaza mapenzi na pesa una ni upumbavu ndio matokeo ya ndoto za kijingajinga tafuta pesa pimbi we
 
Habar wakuu

hapa nimetulia nimekumbuka ndoto niliyoitoa asubuhi ya leo, kwamba natokwa na usaha mwingi sana kwenye sikio la kulia
yani usaha unatoka kama maji nakimbilia nje kwa nje nimesimama pembeni nimeinamisha shingo usaha unamwagika nikamuona jirani yetu mbaba anasema hapo hujainama vizuri kaa chini.

Naomben tafsir ya kutokwa usaha wakuu najua wapo wanakfahamu
Asanten
 
Tafsiri gani ndoto ni ndoto hakuna cha ziada hapo. Sasa mtu umewaza usaha usaha unategemea usiote.

Au unataka tukwambie ule usaha ni utajiri wako utakua unamwagika kama usaha ndio ufurahi
 
Back
Top Bottom