Habari za muda huu wana JF.
Niende moja kwa moja kwenye mada, ndoto ni jambo la kawaida kwa mwanadamu yoyote, lakini si kila ndoto ni yakupuuza (Ninavyoamini mimi).
Usiku huu, kuna ndoto nimeota, ila nahisi ni kama maono fulani, maana nimepewa location halisi na majina ya watu halisi (Maarufu nisio kuwa nawafahamu) ila baada ya kuamka nikaserch kwenye mtandao, hao watu wapo...na shughuli zao ni hizo hizo kama nilivyoota.
Tafadhali, hii kitu sio ya kupuuza, kuna kundi kubwa la watu linapotea katika eneo hilo kwa sababu ya kafara inayofanywa na mtu mmoja kwa makosa yake aliyoyoyafanya huko nyuma zaidi ya miaka kumi imepita.
Mshana Jr my bro, nahisi huu ni uwanja wako pengine una jambo unaweza nifafanulia, na wengine pia mnakaribishwa.
Kabla sijaeleza story nzima kuhusu hii ndoto, naomba nijue kuhusu hii kafara ina maana (Katika ulimwengu wa roho) gani, na ipo kweli.
Huyo muhusika aliwahi uwa mtu...alidhani ni mtu wa kawaida, ila baada ya kufanya hilo tukio alijiingiza kwenye maagano makubwa sana. Maagizo nayoyatekeleza kila baada ya muda fulani ni kama ifuatavyo[emoji116]
Anaambiwa achongeshe kajeneza kadogo (Kazuri) ni kama toy tu hakafai kuingiza hata binadamu labda fedha na vitu vingine vidogo.
Ndani ya hilo jeneza aweke kitambaa cheupe, halafu ajichange kidoleni ahakikishe tone moja tu limedondoka kwenye hicho kitambaa...na baada ya hapo aweke na vito (Madini/Fedha), dhamani yake isipungue, Milioni moja (1,000,000Tzs).Akisha kamilisha hivyo vitu..usiku wa manane Ana end a kuweka hilo eneo ambalo ni makutano ya barabara,
Wakati huo huo hata dakika haiishi hivyo vitu hutoweka na yeye akishuhudia.
Baada ya hapo, ndio kilichonifanya nije hapa, hutokea ajali za kutisha sana hilo eneo, na haipiti miezi mitatu lazima jamaa afanye hiyo kafara.
Tafadhali naomba kujuzwa maana ninachokishangaa kwa nini niletewe majina ya eneo halisi na sijawahi kufika (Ila lipo kweli) na majina ya wahusika na yapo kweli huyo anaefanya hilo jambo...anatambulika kama mtumishi anajiita (Kuhani...) Naomba kujuzwa nahisi nimeoteshwa kuokoa roho za watu zinazopotea bila hatia.
Wale wa kubeza sioni kama hapa ni sehemu sahihi, ni issue serious inahitaji majibu na utekelezaji wa haraka sana.
Karibuni kwa maoni[emoji120]