Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto nyingi huwa zinajirudia mara kwa mara cjui unanisaidiaje.
 

Eeeeh mwenyezi mungu niepushe na madhila hayo, namba 13 na 14 yaani zinaniandama sana, ila yatakwisha kwa uwezo wake Allah
 

Mi nimeota natembea kutoka kwenye nyumba ya ghorofa, nikiwa nipo ground floor naelekea kukaribia mlango wa kutokea kawaida tu. Ghafla hilo ghorofa likatikiswa na kuanguka kuanzia juu kuja chini ghorofa lote basi nikaanza kukimbia nikaribie kufikia lango la kutokea nje japo niliona kutoka ngumu sana na kuna nguzo fulani hapo karibu mapokezi nikataka niishirikirie na wakati huo nikiwa na mawazo kwamba hiyo nguzo inaweza kubaki isianguke waokoaji wakaja kunifukua hapo au ni-risk kwenda mlangoni nijaribu kutoka ( wakati huo juu kunaporomoka na hapo chini pana tetemeko kubwa ) nikiwa natafakari uamuzi gani wa kuchukua kati ya kushikilia nguzo au niruke nje nikastuka usingizini.

Baadae nikaota nipo na wenzangu jumla watatu tuna sanduku la mali za thamani sijui madini au dola. Tukawa tunapanga kuondoka tulipokuwa (porini kuja mjini) lakini tukawa tunabishana tunondoka huko porini vipi bila ulinzi wakati hilo pori lina majambazi waviziaji wengi sana au tufanyeje. Basi tukakubaliana kwanza kila mtu mwenye smart phone azime data kama kuna watu wanatufanyia tracking wasiweze kutuona. Baadaye tukapanga kuondoka lakini tukasita tukiwa na uhakika lazima kuna watu mahala watakuwa wametuwekea ambush, basi katika hangaika hangaika tukawa tumepata bastola lakini mbovu ukijaribu kupiga risasi mara inafyatua mara inagoma. Tukaanza kuulizana twende tusiende? wengine kati yetu wanasema twende wengine wanagoma wanasema usalama hautoshelezi, nikaamka.
 
Tafsiri ya ndoto ya pili
Inainyesha kwenye maisha kuna mpango mkubwa unataka kuufanya lakini unasita kuufanya unahofia hasara na maadui na usalama lamaana kabla ya yote jiwekee utayari wa kupambana kabla ya yoote unayotamani kuwekeza
 

Yaonyesha unafanya jitihada maishani lakini kuna vikwazo sharti uchukue hatua ya kutoka na kuwa huru kabiasa maadui wanaangusha uchumi wako
 
Moja ya thread za kipumbavu kuwahi kuziona for this year..
 
Hiyo namba 27 itakuwaje ukiota uko city mall ?
 
Mimi kutafsiri ndoto alinifundisha mzee wangu. Kwenye yote hayo umegusa moja tu, ishu ya kupanda mlima. Kupanda kwa shida au kuanguka mlimani, hiyo ni ndoto yangu kuu inayonipa mwelekeo wa mafanikio au anguko kimaisha na huwa hivyo kwa 100%.

Ndoto nyingine alonifundisha mzee wangu kuwa ni mbaya na ndiyo inayo determine siku itaishashe ni kuota una sex na mtu ambaye si mwenza wako. Au kuona uchi wa mtu flan ndotoni. Hatariii. Siku nikiota ndoto kama hiyo siku inayofata kuna kamkosi nitaupata 150% bila chenga.

Nyingi hapo ni porojo, umefananisha tu matukio (lugha ya picha). Soma ndoto za kwenye biblia zilizotafsiriwa na kina YUSUF, hazikuwa za kiramli kama hizo zako. Nitaiandaa mada ya tafsiri za ndoto, siyo huo uongo wako.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…