Watu wengi wanaamini Magufuli alikuwa mkali, binafsi nilikuwa namuona bado soft yaani ukali wake aufikii hata nchi za ulaya zinazo hubiri democracy kwenye kunyooshana huo ndio ukweli wenyewe.
Huko kwa mabeberu kama uelewi kwa maelezo na sheria basi utaelewa siku ukiingia kwenye 18 zao na utatia akili, ndio maana kila mtu yupo kwenye mstari mwenyewe.
Sasa watanzania (and this is unique to us only in the world), yaani watu wengi wana akili zao au mtazamo wao juu ya jambo fulani ata waeleweshwe vipi awataki kuelewa wakishajijengea premise ya ukweli wao wanao utaka ni ivyo tu.
Ndio kama hili sakata la bandari yaani Kakoko kalielezea kweli walipokwama na wachina. Kaelezea bandari ya Bagamoyo aina mjadala with or without wachina lazima ijengwe Dar ishafikia saturation point aiwezi kuwa expanded zaidi na mizigo ya nchi inayoitumia inazidi kuongezeka na itazidi kuongezeka.
Sasa unashangaa anaingia raisi mwingine anaanza na kuropoka majukwaani as if wenzake walizuia kwa makusudi wakati wametumia nguvu nyingi kwenye kuelimisha umma walipokwama na kusubiri hatma ya majadiliano kama vipi wajenge wenyewe huo ndio ulikuwa mkakati wa TPA.
Kwenye LNG ivyo ivyo kama ulisoma ile MoU iliyowahi kuwekwa hapa unaona kwanini J.K akutaka lawama za baadae ziwe zake ilikuwa mbovu mno.
Magufuli nae akutaka kuugusa kwa sababu wawekezaji awakuwa tayari kuubadilisha terms za kwenye MoU na ulikuwa na ‘stabilisation clause’ kumbuka hawa tayari wana exclusive right ya ku-exploit vitalu walivyofanyia exploration kukabaki na stalement kwenye majadiliano.
Kaingia Samia anaanza kupayuka nataka majadiliano yaishe soon, niliposikia tu nikajua hana facts, walisema December majadiliano yatakuwa yameisha kiko wapi.
Uzuri wa haya mambo Binafsi sasa hivi naanza kupata imani kuna watu wapo well trained kwenye maswala ya mikataba siku wakikutana na ‘bi Tozo’ wakimuelezea wanachogawa kama namuona akistuka “mtume ebu subirini kwanza, kabla amjasaini”.
Msingi wa upotoshaji ni mijitu ya ovyo kama Zitto na waropokaji au niite wadandiaji wa mambo wenye upeo mdogo kama waziri wa nishati yaani akianza kuongelea maswala ya mikataba his ignorance halafu mwenyewe anajiona wa maana kweli kweli kumbe bogus full of ujinga.
Ndio maana mimi siku nikiwa ata mwenyekiti wa mtaa nikikuta mtu katupa taka kiholela mtaani ntamuamsha ata usiku wa manane akaziokote yaani tuna tabia fulani za ujinga unique to us only bila ya kunyooshana kwa adhabu atuendi.