Ndugai asisahau, kadi yake ya CCM ndio inampa uspika, CCM wanaweza kuiondoa muda wowote na akawa raia wa kawaida tu

Kudhaminiwa na chama sio hoja, hoja ni matakwa ya mtu kuwa spika!! Kudhaminiwa na chama ndo hiyo backup ninayoisema lakini unaweza kugombea uspika hata kama huna chama!!
Yes. Wanaweza kumvua uanachama na ubunge lakini sio uspika. Kama kawakera sana wamwondoe kwa mtindo wa "Tundu Lissu" ila wasiwe wazembe tena kwenye kulenga shabaha
 
Hata Katiba hujui, halafu unabishana na sisi humu.
84.(7) Spika atakoma kuwa spika na ataacha kiti cha spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa mbunge kwasababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa bunge.

Ndugai akiondolewa uanachama wa ccm anakosa sifa ya kuwa mbunge and therefore hawi sifa ya kuwa spika kwasabau amechaguliwa miongoni mwa wabunge...

Umeelewa sasa nilichokuwa namaanisha, maana watu wengine mpaka muandikiwe kwa kirefu.
 
Mbona huwa anaapishia wabunge popote? Tena akiamua hata kama huna chama anakuapisha unakuwa mbunge
Nani atamruhusu , hivi wewe unaijua nguvu ya Rais.. Huyo speaker wako si anapigwa House Arrest anachaguliwa mwingine maisha yanaendelea.. watakwambia kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Utasema nini?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
84.(7) Spika atakoma kuwa spika na ataacha kiti cha spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa mbunge kwasababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa bunge.

Ndugai akiondolewa uanachama wa ccm anakosa sifa ya kuwa mbunge and therefore hawi sifa ya kuwa spika kwasabau amechaguliwa miongoni mwa wabunge...

Umeelewa sasa nilichokuwa namaanisha, maana watu wengine mpaka muandikiwe kwa kirefu.
Naaam, halafu anatulizwa safe house miaka miwili, nchi inasonga, hawezi kutishia usalama wa watu milioni 60 kwa tamaa zake na kukosa busara
 
Nani atamruhusu , hivi wewe unaijua nguvu ya Rais.. Huyo speaker wako si anapigwa House Arrest anachaguliwa mwingine maisha yanaendelea.. watakwambia kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Utasema nini?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Naaam, Naam, baelezee, baelezee papaa
 
Ule ushauri wake ndio unawafanya muanze kuona anyang'anywe kadi?
Hivi hii nchi akili tumezipeleka wapi?
Mbona hatuna uwezo wa tafakuri?
Kwanini tusitafakari ushauri wake?
Kwanini kila kauli itolewayo ionekane ni hujuma?
Kwani hata huyo Rais kinachompa sio kadi ya CCM?
Au Katibu Mkuu wa CCM, kinachompa cheo sio kadi?
Yaani hatutaki kupewa ushauri wa tahadhari juu ya mikopo?
Kwani nchi ngapi maskini zimeshazidiwa na mikopo?
Wewe ndio umenena vyema.
 
Siyo kweli hakuna takwa lazima uwe mwanachama
View attachment 2065562
Kwa mara ya kwanza nimegundua kwann mtu anasomea sheria

Siungi mkono mtoa hoja ila ukisoma vizuri utaelewa kwamba speaker lazima awe mwanachama wa chama cha sias, kwann?

1. Spika lazima awe ametoana miongon mwa wabunge
2. Au mtu mwenye sifa za kua mbunge

Tunakuja kwenye hoja, mbunge n nani? Sifa za kua mbunge n zipi?

Lazima udhaminiwe na chama cha siasa
 
Yaani huyo pimbi wenu wakitaka wamchomoe uspika wanacheza na vifungu vya katiba tu wanamng'oa kwenye vile vile vifungu vya katiba vinavyoweza kumtoa kwenye uspika....

Kuna kifungu kinasema akiwa ametoa habari za uongo... n.k yaani wakimtaka hatoboi.

Azimio la wabunge pia linaweza likamchomoa
 
Kuna watu wanamdanganya eti anaweza kutikisa Urais wa Samia .. wasindanganye, siku anaanza ndio siku anafutiwa uanachama, ubunge wake unakoma, na uspika unakoma
Yule mgonjwa bora wammwage tu mfyuuu zake
 
Ule ushauri wake ndio unawafanya muanze kuona anyang'anywe kadi?
Hivi hii nchi akili tumezipeleka wapi?
Mbona hatuna uwezo wa tafakuri?
Kwanini tusitafakari ushauri wake?
Kwanini kila kauli itolewayo ionekane ni hujuma?
Kwani hata huyo Rais kinachompa sio kadi ya CCM?
Au Katibu Mkuu wa CCM, kinachompa cheo sio kadi?
Yaani hatutaki kupewa ushauri wa tahadhari juu ya mikopo?
Kwani nchi ngapi maskini zimeshazidiwa na mikopo?
Akili zako umetoka milembe.
Upi ushauri alotoa kama bandari ya bagamoyo alisema rais alidanganywa kua haufai na wakati jpm anaukataa aliufyata, unategemea kua ndukai ana utimamu hapo alipo.
Kwani hyo bandari tungejenga kwa hela za ndani?
Si mkopo?

Sasa leo kananyanyua pua na kusema nchi itauzwa?

Arudi ubungo kibangu kwa hawara yake mjinga mkubwa
 
Viongozi wajifunze kuridhika na nyadhifa zao sababu kinachoonekana hapo ni kujipendekeza kwa wananchi kwamba anafaa kuwa Raisi wakati watu wanaangalia matendo yako mfano mzuri ni JPM watu waliridhishwa na matendo yake.Kwenye upande wa kinga ya bunge Raisi any time anaweza kuvunja bunge akiona mwenendo wake hauridhishi,Raisi ndio mwenye kiti wa chama wa huyo mpingaji akimvua uanachama hatakiwi kuwemo hapo bungeni sababu ubunge nao unakuwa umeondoka.
 
Ule ushauri wake ndio unawafanya muanze kuona anyang'anywe kadi?
Hivi hii nchi akili tumezipeleka wapi?
Mbona hatuna uwezo wa tafakuri?
Kwanini tusitafakari ushauri wake?
Kwanini kila kauli itolewayo ionekane ni hujuma?
Kwani hata huyo Rais kinachompa sio kadi ya CCM?
Au Katibu Mkuu wa CCM, kinachompa cheo sio kadi?
Yaani hatutaki kupewa ushauri wa tahadhari juu ya mikopo?
Kwani nchi ngapi maskini zimeshazidiwa na mikopo?
Tatizo sio ushauri tatizo ni namna alivyouwasilisha kwa dharau na kejeli kwa Rais Samia na taifa kwa ujumla,shida ndio ilipoanzia hapo.
 
Viongozi wajifunze kuridhika na nyadhifa zao sababu kinachoonekana hapo ni kujipendekeza kwa wananchi kwamba anafaa kuwa Raisi wakati watu wanaangalia matendo yako mfano mzuri ni JPM watu waliridhishwa na matendo yake.Kwenye upande wa kinga ya bunge Raisi any time anaweza kuvunja bunge akiona mwenendo wake hauridhishi,Raisi ndio mwenye kiti wa chama wa huyo mpingaji akimvua uanachama hatakiwi kuwemo hapo bungeni sababu ubunge nao unakuwa umeondoka.
Bora jpm kuliko mgonjwa wa ukoma na mdudu.

Hafai mwasherati alimkimbia mkewe kaenda kuishi kwa kimada msewe huku akibugia viroba hadi alipotolewa huko
 
Tatizo sio ushauri tatizo ni namna alivyouwasilisha kwa dharau na kejeli kwa Rais Samia na taifa kwa ujumla,shida ndio ilipoanzia hapo.
Dharau gani?
Is that healthy?
Ndio namna ya kurun nchi?
Juzi mama alikopa 1.3T?
Kuna siku itapigwa mnada?

Hapo kuna dharau?
Wabongo bana!
Mnapenda nidhamu ya woga sana.
Mnapenda kunyenyekewa.
 
Kuna watu wanamdanganya eti anaweza kutikisa Urais wa Samia. Wasidanganye, siku anaanza ndio siku anafutiwa uanachama, ubunge wake unakoma, na uspika unakoma
Kwa mujibu wa katiba, mtu yeyote anaweza kugombea uspika na kuchaguliwa. Ni kweli anaweza kuvuliwa uanachama na kupoteza ubunge lakini hawezi kupoteza uspika. Vile vile hata ikilazimishwa apoteze uspika anaweza kugombea tena uspika kama raia huru au kudhaminiwa na chama kingine na wabunge kama wanampenda watamchagua tena kuwa spika.
 
Too academic
 
Back
Top Bottom