Pre GE2025 Ndugai atoa hoja utaratibu kumwona daktari kwa Tsh. 10,000 ufutwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Screenshot 2025-03-15 094347.jpg
SPIKA Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ameishauri serikali kuangalia upya utaratibu uliopo sasa, katika hospitali nyingi za umma kuwa ni lazima mgonjwa kutoa Sh. 10,000 kwa ajili ya kumuona daktari.

Ndugai, alisema hayo juzi jijini hapa, wakati akichangia hoja kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), kilichofanyika jijini Dodoma.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Alisema, hivi sasa upo utaratibu ambao unatumika katika hospitali nyingi za umma, kwa wagonjwa kulazimika kutoa kiasi cha Sh. 10,000 ili wamwone Daktari.

“Hivi huu utaratibu wa lazima mgonjwa atoe Sh. 10,000 kwa ajili ya kumwona daktari, nini mantiki yake yaani kumwona mkuu wa mkoa ni bure kumwona waziri ni bure kwanini kumwona dakatari ni Sh. 10,000,” alihoji Ndugai.

Aidha, alisema kama inawezekana utaratibu huo uangaliwe upya, ili kuona viwango hivyo vinapunguzwa kutoa nafuu kwa wagonjwa ambao wamekuwa na uhitaji wa kuwaona madaktari, kwa ajili ya matibabu mbalimbali.

“Mtu anaumwa lakini hawezi kumuona Daktari hadi awe na Sh.10,000, hebu kama inawezekana basi viwango hivi tuone namna ya kuvipunguza ili tutoe unafuu kwa wananchi wanaohitaji kuwaona madaktari,” alisema.

Kadhalika, alisema hivi sasa katika vituo vingi vya afya vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali hususani vijiji ambako watu wengi wanatumia huduma ya kadi za bima ya afya ya jamii CHF, wanakosa huduma kutoka na serikali kutorudisha fedha katika vituo hivyo.

“Hivi sasa katika maeneo mengi ya vijijini kule ambako wanatumia sana kadi hizi za CHF, wanalalamika kukosa huduma kutokana na vituo kukosa fedha ambazo serikali ilipaswa kuzirudisha katika vituo hivyo,” alisema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Thomas Rutachunzibwa, akitoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao hicho, alisema kiasi hicho cha Sh. 10,000 kwa ajili ya kuwaona madaktari kinaenda katika mfuko mkuu wa serikali na siyo mfukoni mwa mtu.

“Fedha hizi zinakwenda kwenye mfuko wa mkuu wa serikali siyo mfukoni mwa daktari, lakini kama ulivyotoa ushauri wako mheshimiwa Ndugai, tutauzingatia kuona namna ya kupitia upya viwango hivi,” alisema Dk. Rutachunzibwa.

Kuhusu fedha zinazopaswa kurudishwa kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumia watumiaji wa kadi za Bima ya Afya ya Jamii (CHF), alisema ipo changamoto kidogo ya kimfumo ambayo inafanyiwa kazi na muda siyo mrefu hali hiyo itakuwa sawa.
 
SPIKA Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ameishauri serikali kuangalia upya utaratibu uliopo sasa, katika hospitali nyingi za umma kuwa ni lazima mgonjwa kutoa Sh. 10,000 kwa ajili ya kumuona daktari.

Ndugai, alisema hayo juzi jijini hapa, wakati akichangia hoja kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), kilichofanyika jijini Dodoma.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Alisema, hivi sasa upo utaratibu ambao unatumika katika hospitali nyingi za umma, kwa wagonjwa kulazimika kutoa kiasi cha Sh. 10,000 ili wamwone Daktari.

“Hivi huu utaratibu wa lazima mgonjwa atoe Sh. 10,000 kwa ajili ya kumwona daktari, nini mantiki yake yaani kumwona mkuu wa mkoa ni bure kumwona waziri ni bure kwanini kumwona dakatari ni Sh. 10,000,” alihoji Ndugai.

Aidha, alisema kama inawezekana utaratibu huo uangaliwe upya, ili kuona viwango hivyo vinapunguzwa kutoa nafuu kwa wagonjwa ambao wamekuwa na uhitaji wa kuwaona madaktari, kwa ajili ya matibabu mbalimbali.

“Mtu anaumwa lakini hawezi kumuona Daktari hadi awe na Sh.10,000, hebu kama inawezekana basi viwango hivi tuone namna ya kuvipunguza ili tutoe unafuu kwa wananchi wanaohitaji kuwaona madaktari,” alisema.

Kadhalika, alisema hivi sasa katika vituo vingi vya afya vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali hususani vijiji ambako watu wengi wanatumia huduma ya kadi za bima ya afya ya jamii CHF, wanakosa huduma kutoka na serikali kutorudisha fedha katika vituo hivyo.

“Hivi sasa katika maeneo mengi ya vijijini kule ambako wanatumia sana kadi hizi za CHF, wanalalamika kukosa huduma kutokana na vituo kukosa fedha ambazo serikali ilipaswa kuzirudisha katika vituo hivyo,” alisema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Thomas Rutachunzibwa, akitoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao hicho, alisema kiasi hicho cha Sh. 10,000 kwa ajili ya kuwaona madaktari kinaenda katika mfuko mkuu wa serikali na siyo mfukoni mwa mtu.

“Fedha hizi zinakwenda kwenye mfuko wa mkuu wa serikali siyo mfukoni mwa daktari, lakini kama ulivyotoa ushauri wako mheshimiwa Ndugai, tutauzingatia kuona namna ya kupitia upya viwango hivi,” alisema Dk. Rutachunzibwa.

Kuhusu fedha zinazopaswa kurudushwa kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumia watuamiaji wa kadi za Bima ya Afya ya Jamii (CHF), alisema ipo changamoto kidogo ya kimfumo ambayo inafanyiwa kazi na muda siyo mrefu hali hiyo itakua sawa.

Serikali ndiyo inayochukua hiyo hela wanayoita ya kumuona daktari. Wengi huamini kwamba inaingia mfukoni mwa daktari lakini siyo.

Huyo huyo daktari anayedhaniwa kuchukua hiyo ada (hela ya kumuona daktari) hulazimika kulipia leseni ya udaktari kila mwaka TSH. 100,000/= ambayo nayo huenda serikalini.

Wakati huo huo hiyo leseni daktari hatumii kufanya biashara yoyote bali kutoa huduma (kutibu).
 
Hili nalo ni jema mamlaka husika ilichukue!, wagonjwa tupate nafuu.
 
Naunga mkono hoja lakini suluhisho ni bima ya Afya
 
Tayari ameanza kuwa mpole na kuyaona na kuyaishi maisha ya mtanzania ambaye kipato chake mara zote hakina uhakika.
Hizi dalili za kugeuka mpigania haki za binadamu hutokea sana kwa wastaafu wote.
Mara mafao yanapoanza kukata na kule Serikalini walikokuwa wameajiriwa, connections zinapoanza kukata na kujikuta akiingia mahali hatambuliki tena ....Utasikia mstaafu anavyogeuka kiwa mkosoaji na mlalamishi kwa Serikali au sheria mbovu alizosimamia kutungwa na kuzisimamia akiwa kwenye nafasi nyeti na hazimhusu kwa wakati huo.

Kufupisha, Ndugai acha madaktari wapate ujira wao halali wa SHS 10000 tu kuwaona, nadhani wewe kwa nafasi yako unamudu hivyo usilalamike na kuomba sheria zibadilishwe sasa, ungefanya kazi hiyo ulipokuwa kiranja wa watunga Sheria....Sisi wengine tuliishazoea kwa hiyo ...Hapa Kazi Tu!. 🤓
 
“Hivi huu utaratibu wa lazima mgonjwa atoe Sh. 10,000 kwa ajili ya kumwona daktari, nini mantiki yake yaani kumwona mkuu wa mkoa ni bure kumwona waziri ni bure kwanini kumwona dakatari ni Sh. 10,000,” alihoji Ndugai.
 
Ndio maana watu wanaishia Maduka ya dawa sababu ya gharama kama hizi
 
Serikali ndiyo inayochukua hiyo hela wanayoita ya kumuona daktari. Wengi huamini kwamba inaingia mfukoni mwa daktari lakini siyo.

Huyo huyo daktari anayedhaniwa kuchukua hiyo ada (hela ya kumuona daktari) hulazimika kulipia leseni ya udaktari kila mwaka TSH. 100,000/= ambayo nayo huenda serikalini.

Wakati huo huo hiyo leseni daktari hatumii kufanya biashara yoyote bali kutoa huduma (kutibu).
Hahaha! Unalipia leseni serikalini ili uruhusiwe kutibu watu wa serikali
 
Back
Top Bottom