SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 47,706
- 69,281
Bungeni kwenyewe anaona aibu kwenda kuwa back bencherAmekua sasa ,Nafikiri akiambiwa arudi kuwa spika atakataa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bungeni kwenyewe anaona aibu kwenda kuwa back bencherAmekua sasa ,Nafikiri akiambiwa arudi kuwa spika atakataa
Hawezi kataa kamwe, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Amekua sasa ,Nafikiri akiambiwa arudi kuwa spika atakataa
Wee anakataa sasa hivi atamfokea nani?Hawezi kataa kamwe, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Atawafokea anao waongoza. Au watu wa chini yake.Wee anakataa sasa hivi atamfokea nani?
Hii ni Afya,Ili nchi isonge mbele lazima iwe na wananchi wake wenye Afya inayotokana na Akili timamu,kumuona Dr ni kuiyumbisha Afya pia, maana kama huna hiyo hela,hutaangaika kumuona Dr.SPIKA Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ameishauri serikali kuangalia upya utaratibu uliopo sasa, katika hospitali nyingi za umma kuwa ni lazima mgonjwa kutoa Sh. 10,000 kwa ajili ya kumuona daktari.
Ndugai, alisema hayo juzi jijini hapa, wakati akichangia hoja kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), kilichofanyika jijini Dodoma.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alisema, hivi sasa upo utaratibu ambao unatumika katika hospitali nyingi za umma, kwa wagonjwa kulazimika kutoa kiasi cha Sh. 10,000 ili wamwone Daktari.
“Hivi huu utaratibu wa lazima mgonjwa atoe Sh. 10,000 kwa ajili ya kumwona daktari, nini mantiki yake yaani kumwona mkuu wa mkoa ni bure kumwona waziri ni bure kwanini kumwona dakatari ni Sh. 10,000,” alihoji Ndugai.
Aidha, alisema kama inawezekana utaratibu huo uangaliwe upya, ili kuona viwango hivyo vinapunguzwa kutoa nafuu kwa wagonjwa ambao wamekuwa na uhitaji wa kuwaona madaktari, kwa ajili ya matibabu mbalimbali.
“Mtu anaumwa lakini hawezi kumuona Daktari hadi awe na Sh.10,000, hebu kama inawezekana basi viwango hivi tuone namna ya kuvipunguza ili tutoe unafuu kwa wananchi wanaohitaji kuwaona madaktari,” alisema.
Kadhalika, alisema hivi sasa katika vituo vingi vya afya vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali hususani vijiji ambako watu wengi wanatumia huduma ya kadi za bima ya afya ya jamii CHF, wanakosa huduma kutoka na serikali kutorudisha fedha katika vituo hivyo.
“Hivi sasa katika maeneo mengi ya vijijini kule ambako wanatumia sana kadi hizi za CHF, wanalalamika kukosa huduma kutokana na vituo kukosa fedha ambazo serikali ilipaswa kuzirudisha katika vituo hivyo,” alisema.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Thomas Rutachunzibwa, akitoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao hicho, alisema kiasi hicho cha Sh. 10,000 kwa ajili ya kuwaona madaktari kinaenda katika mfuko mkuu wa serikali na siyo mfukoni mwa mtu.
“Fedha hizi zinakwenda kwenye mfuko wa mkuu wa serikali siyo mfukoni mwa daktari, lakini kama ulivyotoa ushauri wako mheshimiwa Ndugai, tutauzingatia kuona namna ya kupitia upya viwango hivi,” alisema Dk. Rutachunzibwa.
Kuhusu fedha zinazopaswa kurudishwa kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumia watumiaji wa kadi za Bima ya Afya ya Jamii (CHF), alisema ipo changamoto kidogo ya kimfumo ambayo inafanyiwa kazi na muda siyo mrefu hali hiyo itakuwa sawa.
Nikukosoe kidogo mkuu ni laki3!Serikali ndiyo inayochukua hiyo hela wanayoita ya kumuona daktari. Wengi huamini kwamba inaingia mfukoni mwa daktari lakini siyo.
Huyo huyo daktari anayedhaniwa kuchukua hiyo ada (hela ya kumuona daktari) hulazimika kulipia leseni ya udaktari kila mwaka TSH. 100,000/= ambayo nayo huenda serikalini.
Wakati huo huo hiyo leseni daktari hatumii kufanya biashara yoyote bali kutoa huduma (kutibu).
Hahaha! Unalipia leseni serikalini ili uruhusiwe kutibu watu wa serikali
Duh, pole sana kama ulikutana na hayo!Halaf madaktari wakiona mgonjwa dalili zake haponi au ashakata roho wanakuagiza dawa za bei juuu ili baadae wakaziuze hawa watu hawaogopi kabisa
Ndiyo ni laki 3 mwanzoni kabisa daktari anapojisajili, baada ya hapo atakuwa analipia laki 1 kila mwakaNikukosoe kidogo mkuu ni laki3!
Ungetumia neno baadhi, msg yako ingeleta uhalisia.Halaf madaktari wakiona mgonjwa dalili zake haponi au ashakata roho wanakuagiza dawa za bei juuu ili baadae wakaziuze hawa watu hawaogopi kabisa
Serikali itoe maelezo ya kueleweka hizi fedha ni za nini? Ushauri wa daktari ni muhimu sana na unapaswa kutolewa bure. Kitendo cha kutoza kumwuona daktari kunasababisha watu kununua dawa bila utaratibu na kuwasababishia madhara wagonjwa!SPIKA Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ameishauri serikali kuangalia upya utaratibu uliopo sasa, katika hospitali nyingi za umma kuwa ni lazima mgonjwa kutoa Sh. 10,000 kwa ajili ya kumuona daktari.
Ndugai, alisema hayo juzi jijini hapa, wakati akichangia hoja kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), kilichofanyika jijini Dodoma.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alisema, hivi sasa upo utaratibu ambao unatumika katika hospitali nyingi za umma, kwa wagonjwa kulazimika kutoa kiasi cha Sh. 10,000 ili wamwone Daktari.
“Hivi huu utaratibu wa lazima mgonjwa atoe Sh. 10,000 kwa ajili ya kumwona daktari, nini mantiki yake yaani kumwona mkuu wa mkoa ni bure kumwona waziri ni bure kwanini kumwona dakatari ni Sh. 10,000,” alihoji Ndugai.
Aidha, alisema kama inawezekana utaratibu huo uangaliwe upya, ili kuona viwango hivyo vinapunguzwa kutoa nafuu kwa wagonjwa ambao wamekuwa na uhitaji wa kuwaona madaktari, kwa ajili ya matibabu mbalimbali.
“Mtu anaumwa lakini hawezi kumuona Daktari hadi awe na Sh.10,000, hebu kama inawezekana basi viwango hivi tuone namna ya kuvipunguza ili tutoe unafuu kwa wananchi wanaohitaji kuwaona madaktari,” alisema.
Kadhalika, alisema hivi sasa katika vituo vingi vya afya vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali hususani vijiji ambako watu wengi wanatumia huduma ya kadi za bima ya afya ya jamii CHF, wanakosa huduma kutoka na serikali kutorudisha fedha katika vituo hivyo.
“Hivi sasa katika maeneo mengi ya vijijini kule ambako wanatumia sana kadi hizi za CHF, wanalalamika kukosa huduma kutokana na vituo kukosa fedha ambazo serikali ilipaswa kuzirudisha katika vituo hivyo,” alisema.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Thomas Rutachunzibwa, akitoa ufafanuzi wa hoja zilizotolewa na wajumbe wa kikao hicho, alisema kiasi hicho cha Sh. 10,000 kwa ajili ya kuwaona madaktari kinaenda katika mfuko mkuu wa serikali na siyo mfukoni mwa mtu.
“Fedha hizi zinakwenda kwenye mfuko wa mkuu wa serikali siyo mfukoni mwa daktari, lakini kama ulivyotoa ushauri wako mheshimiwa Ndugai, tutauzingatia kuona namna ya kupitia upya viwango hivi,” alisema Dk. Rutachunzibwa.
Kuhusu fedha zinazopaswa kurudishwa kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumia watumiaji wa kadi za Bima ya Afya ya Jamii (CHF), alisema ipo changamoto kidogo ya kimfumo ambayo inafanyiwa kazi na muda siyo mrefu hali hiyo itakuwa sawa.
Mdogo wangu alikuwa ICU ashafariki siku tatu alikuwa kwenye coma tunaagizwa dawa za bei kweli ngoja nikae kimyaDuh, pole sana kama ulikutana na hayo!
Kama kweli wapo walioufanyia hivyo ni vyema ukawaripoti washughulikiwe.
Pia madaktari wameapa kukoa maisha ya mgonjwa kwa hiyo hata kama mgonjwa yupo mahututi hawatakiwi kuacha kumhudumia kwa kufanya kila wawezalo kuokoa maisha yake. Kwa hiyo hakuna daktari atakayemwagizia mgonjwa dawa za bei ghali kisa eti anakaribia kukata roho. Kama utagundua wanakufanyia hivyo basi mwishoni waambie wakurudishie dawa zako kama hazijatumika.
Akili alikuwanazo tangu akiwa CCM ndiyo maana wakamfurusha u spika.Mheshimiwa John Ndugai una akili sana baada ya kuacha/kuachishwa Uspika. Shikilia hapo hapo.
Mdogo wangu alikuwa ICU ashafariki siku tatu alikuwa kwenye coma tunaagizwa dawa za bei kweli ngoja nikae kimya
Mkuu nafikiri hata ikiwa hiyo 1,000 bado watu watalalamika tu.