Pre GE2025 Ndugai atoa hoja utaratibu kumwona daktari kwa Tsh. 10,000 ufutwe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii ni Afya,Ili nchi isonge mbele lazima iwe na wananchi wake wenye Afya inayotokana na Akili timamu,kumuona Dr ni kuiyumbisha Afya pia, maana kama huna hiyo hela,hutaangaika kumuona Dr.
 
Nikukosoe kidogo mkuu ni laki3!
 
Halaf madaktari wakiona mgonjwa dalili zake haponi au ashakata roho wanakuagiza dawa za bei juuu ili baadae wakaziuze hawa watu hawaogopi kabisa
 
Hahaha! Unalipia leseni serikalini ili uruhusiwe kutibu watu wa serikali

Ndiyo, halafu mwisho ndiyo haya ya kuona kwamba anayechukua hela ya kumuona daktari ni daktari!
 
Halaf madaktari wakiona mgonjwa dalili zake haponi au ashakata roho wanakuagiza dawa za bei juuu ili baadae wakaziuze hawa watu hawaogopi kabisa
Duh, pole sana kama ulikutana na hayo!

Kama kweli wapo walioufanyia hivyo ni vyema ukawaripoti washughulikiwe.

Pia madaktari wameapa kukoa maisha ya mgonjwa kwa hiyo hata kama mgonjwa yupo mahututi hawatakiwi kuacha kumhudumia kwa kufanya kila wawezalo kuokoa maisha yake. Kwa hiyo hakuna daktari atakayemwagizia mgonjwa dawa za bei ghali kisa eti anakaribia kukata roho. Kama utagundua wanakufanyia hivyo basi mwishoni waambie wakurudishie dawa zako kama hazijatumika.
 
Kama Ndugai (mtu ambae amewahi kuwa Naibu Spika Kwa miaka 5, na Spika kwa miaka 5. Lakini pia ni mbunge wa muda mrefu).
Hajui hiyo pesa inayoitwa ya kumuona daktari huwa inakwenda wapi?
Na kazi yake ni nini?

Basi itoshe kusema tuna very long long safari.
 
Halaf madaktari wakiona mgonjwa dalili zake haponi au ashakata roho wanakuagiza dawa za bei juuu ili baadae wakaziuze hawa watu hawaogopi kabisa
Ungetumia neno baadhi, msg yako ingeleta uhalisia.
 
Serikali itoe maelezo ya kueleweka hizi fedha ni za nini? Ushauri wa daktari ni muhimu sana na unapaswa kutolewa bure. Kitendo cha kutoza kumwuona daktari kunasababisha watu kununua dawa bila utaratibu na kuwasababishia madhara wagonjwa!
 
Mdogo wangu alikuwa ICU ashafariki siku tatu alikuwa kwenye coma tunaagizwa dawa za bei kweli ngoja nikae kimya
 
Mdogo wangu alikuwa ICU ashafariki siku tatu alikuwa kwenye coma tunaagizwa dawa za bei kweli ngoja nikae kimya

Pole sana!

Naamini nia yao haikuwa mbaya bali ni katika juhudi tu za kumuokoa.
 
Iwe 1,000/=

Cc: Mahondaw
Mkuu nafikiri hata ikiwa hiyo 1,000 bado watu watalalamika tu.

Hata hivyo hiyo hela ya kumuona daktari ni sehemu ya wananchi kuchangia uendeshaji wa huduma za afya.

Labda lile suala la bima kwa wote likikamilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…