eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Akitoa salamu zake mbele ya raisi samia kwenye sherehe za wafanyakazi, spika wa bunge job ndugai amesema mwanza ingependeza kama wangeacha kuezeka nyumba zao kwa masufuria, akisema
"mwanza kunapendeza lakinni kwanini mnafunika nyumba zenu na masufuria? ,Ingependeza kama mngeezeka nyumba zenu na mabati ya kijani".
Hii ni dharau kubwa sana kwa mtu mkubwa kama spika kutoa dharau kwa watu ambao kipato chao ni kidogo na ndiyo maana nyumba zao wameezeka na mabati ya sufuria. Kweli viingozi wetu wakipata uwezo mkubwa wa fedha wanasahau kabisa kwamba kuna wengine hawana uwezo kama wa kwao .
Wewe unatetea nini? Last December nimepita kutoka Arusha mpaka Singida. Kufika Singida, nyumba ziko na mabati ya blue, kijani, kijivu, damu ya mzee nk.
Sasa uchumi wa Singida unauzidi wa Mwanza?
Wasukuma mjiongeze, Mwanza ina rasilimali na vitu vingi kuliko Singida, lkn watu wake wamejitahidi sana. Nyumba zao pale mjini ni shidaa. Utaipenda yani. Hivyo Mwanza hawana sababu ya kujitetea.
😁😀😁