Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,970
Licha ya kwamba serikali yote ilishahamia Dodoma mwaka 2019 lakini bado kuna kundi limeibuka la kushinikiza serikali irudishwe Dares salaam!!
Ikumbukwe kuwa serikali imeanza kuokoa zaidi billioni 30 kwa mwaka baada ya kuachana na ofisi za kupanga Dar na sasa wamejenga ofisi za wizara zote Dodoma, licha ya ukweli wote huu bado kuna viongozi wakubwa tu ndani ya serikali wanataka serikali irudi Dar!
Ukichunguza akili za watu hao hazina tofauti na wanaoomba kazi serikalini na wanajaza fomu ya kwamba wako tayari kufanya kazi popote Tanzania lakini wakipangiwa tu vijijini wanaripoti na kuanza kuzunguka maofisini kuhonga ili wapewe uhamisho wa kurudi mjini na ukiangalia huyo hana chochote anachomiliki mjini wala Dar zaidi kwenda kushangaa V8 na magorofa ya wenzake.
Rais Samia shituka na utangaze asiyetaka kufanyia kazi Dodoma aache kazi na mara moja utangaze ajira za kuziba nafasi zao uone maelfu ya vijana watakaomiminika kuja kufanya Dodoma.