Ndugai: Toka Magufuli aage Dunia, umuhimu wa Dodoma unafifishwa kwa makusudi kabisa

Ndugai: Toka Magufuli aage Dunia, umuhimu wa Dodoma unafifishwa kwa makusudi kabisa

Licha ya kwamba serikali yote ilishahamia Dodoma mwaka 2019 lakini bado kuna kundi limeibuka la kushinikiza serikali irudishwe Dares salaam!!
Ikumbukwe kuwa serikali imeanza kuokoa zaidi billioni 30 kwa mwaka baada ya kuachana na ofisi za kupanga Dar na sasa wamejenga ofisi za wizara zote Dodoma, licha ya ukweli wote huu bado kuna viongozi wakubwa tu ndani ya serikali wanataka serikali irudi Dar!

Ukichunguza akili za watu hao hazina tofauti na wanaoomba kazi serikalini na wanajaza fomu ya kwamba wako tayari kufanya kazi popote Tanzania lakini wakipangiwa tu vijijini wanaripoti na kuanza kuzunguka maofisini kuhonga ili wapewe uhamisho wa kurudi mjini na ukiangalia huyo hana chochote anachomiliki mjini wala Dar zaidi kwenda kushangaa V8 na magorofa ya wenzake.
Rais Samia shituka na utangaze asiyetaka kufanyia kazi Dodoma aache kazi na mara moja utangaze ajira za kuziba nafasi zao uone maelfu ya vijana watakaomiminika kuja kufanya Dodoma.
 
Kwani yeye ni nani asiambiwe ukweli?

Kwa hiyo akitaka kukuchukulia bwana yako kwa kigezo hicho itakulazimu ukae kimya siyo?!
Ikulu ambayo as now iko functioning properly ni Ikulu ya magogoni... Dodoma bado wanajenga
Bank Kuu kwa maana ya infrastructure zote bado ni Dar
Jeshi kwa maana ya equipments za ulinzi vipo Dar
Airport inayoingiza ndege zote toka nje ni dar
Bandari iko Dar
Coorporate zote kubwa ziko Dar, dodoma n wana rooms tu na wafanyakazi wachache
Private companies zote kubwa zipo Dar
Embassies zote zipo Dar, mbali na kupewa viwanja vya bure Dodoma
Vyama vya siasa vyote isipokuwa CCM makao yao makuu yapo dar
Mashirika mengine ya kimataifa ILO, UNESCO, UNDP etc yapo dar

Sasa bwana Ndugai unataka mji mkuu uje Dodoma kwa ajili ya mnada wa nyama jumamosi? Au kwa soko la Ndugai ambalo wafanyabiashara wamesusa , au Stendi ya mabasi ya mabilioni ambayo inatumika kwa silimia 34, Au kwa kipi haswa
 
MAGOGONI MODERN TAARAB
wametoa Album Mpya ina Ngoma Sita zote Kali
1.Mtu na akili yako unahoji tozo na Mkopo
2.Stress za 2025
3.Serikali ya Mpito
4. Watakao kusumbua ni Shati ya Kijani wenzio
5.Kuna Mawaziri Mmeanza Makundi Makundi yenu
6.kuna watu nitawapumzisha Wakajiandae 2025

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani lazima Spika awe na Mama ?

Spika wa nchi ya kidemokrasia sio lazima kuwa pamoja na Rais kwenye kila kitu

Unajua maana ya checks and balances? Unajua maana ya mihimili tofauti? Umeenda shule ????
Kidemokrasia eeh

IMG-20220104-WA0022.jpg

IMG-20220104-WA0023.jpg
 
Ndugai Leo akae na daktari maana lolote linaweza kutolea!
 
"....wakati fulani Dodoma ilikuwa mchaka mchaka wa hakika kuelekea kuwa Mji mkuu wa Serikali ki vitendo na hata ulipokuwa unawaangalia Viongozi wakuu wa Serikali ulikuwa unaona nyuso za haja za kulimaliza hilo mapema kabisa."

"...sasa hivi kila warsha na kongamano ni Dar!"

"...hii siyo sawasawa kabisa Dodoma ni Mji na makao makuu ya Nchi ki sheria na hata hao wanaofanya kampeni za kufifisha safari hiyo wanapoteza muda wao bure tu."

"...ndugu zangu wapende ama wasipende Dodoma ni lazima wataishi kwa sababu Bunge lilishatunga sheria na kamwe haiwezi kubadirika."

Amesema Ndugai.
Tatizo lilianzia huku
 
Licha ya kwamba serikali yote ilishahamia Dodoma mwaka 2019 lakini bado kuna kundi limeibuka la kushinikiza serikali irudishwe Dares salaam!!
Ikumbukwe kuwa serikali imeanza kuokoa zaidi billioni 30 kwa mwaka baada ya kuachana na ofisi za kupanga Dar na sasa wamejenga ofisi za wizara zote Dodoma, licha ya ukweli wote huu bado kuna viongozi wakubwa tu ndani ya serikali wanataka serikali irudi Dar!

Ukichunguza akili za watu hao hazina tofauti na wanaoomba kazi serikalini na wanajaza fomu ya kwamba wako tayari kufanya kazi popote Tanzania lakini wakipangiwa tu vijijini wanaripoti na kuanza kuzunguka maofisini kuhonga ili wapewe uhamisho wa kurudi mjini na ukiangalia huyo hana chochote anachomiliki mjini wala Dar zaidi kwenda kushangaa V8 na magorofa ya wenzake.
Rais Samia shituka na utangaze asiyetaka kufanyia kazi Dodoma aache kazi na mara moja utangaze ajira za kuziba nafasi zao uone maelfu ya vijana watakaomiminika kuja kufanya Dodoma.

Sukuma gang kazini
 
Back
Top Bottom