Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

hawa jamaa wanacheza na akili za watu, tulishaambiwa huo mkataba ni bogus treaty wanachopaswa kutuambia leo siyo ushawishi kazi iendelee ila watuambie kwa nini mwanzo walikubaliana kuwa mkataba huo ni bogus treaty na leo kwa nini umevuka na kutokuwa bogus treaty.
 
Yetu masikio mkataba utakaosoma sio utakao sainiwa hapo ndo tatizo
Yawezekana kweli ni mradi mzuri lakini inatia shaka kwamba Spika anaupenda mradi huu tangu miaka 5 iliyopita. Sababu kubwa; alifanyiwa presentation akiwa China kwa ziara nyingine, akaongozwa na balozi wetu. Hadi leo haelewi vingine yeye anataka bandari hiyo. Huku ni kukosa aibu kwa Watanzania.

Muhimu kabisa, tulistahili tuambiwe mkataba unaemaje? Suala siyo mradi, ni mkataba! Je, yeye Spika yuko tayari kutueleza mkataba unasemaje? Tamaa hii ni ile ya fisi aliye na njaa kali, na amekuwa akisubili mlinzi aondoke. Kweli mlinzi kaondoka sasa ni kampeni chakula kiliwe bila kujali kina sumu au la!
 
Duh kwani walikuwa wapi mzee akiwepo wamshauri?aisee kwakweli watu ni wanafiki sana...mzee angekuwepo wangeweza kufungua mabakuli? Unafiki dhambi mbaya sana natamani mwendazake angeamka kidogo aone ile praise n worship choir inachofanya ...bora mchawi kuliko mnafiki..
 
Yawezekana kweli ni mradi mzuri lakini inatia shaka kwamba Spika anaupenda mradi huu tangu miaka 5 iliyopita. Sababu kubwa; alifanyiwa presentation akiwa China kwa ziara nyingine, akaongozwa na balozi wetu. Hadi leo haelewi vingine yeye anataka bandari hiyo. Huku ni kukosa aibu kwa Watanzania.

Muhimu kabisa, tulistahili tuambiwe mkataba unaemaje? Suala siyo mradi, ni mkataba! Je, yeye Spika yuko tayari kutueleza mkataba unasemaje? Tamaa hii ni ile ya fisi aliye na njaa kali, na amekuwa akisubili mlinzi aondoke. Kweli mlinzi kaondoka sasa ni kampeni chakula kiliwe bila kujali kina sumu au la!
Kwa mashariti yale haikubaliki, ni afadhali ibaki hapo vitukuu watakuja kuijenga hio bandari sio, kuuzwa kama babu zetu walivyofanywa
 
Zaidi ya Timu ya JK, Magufuli na Ndugai Hakuna mtu mwingine mwenye uhakika na kilichopo kwenye huo mkataba uliokuwa unapendekezwa. Bahati mbaya wote inakuwa vigumu kuwaamini wanachosema. Suluhisho ni kuweka huo mkataba hadharani zaidi ya hapo hakuna cha kueleweka kuweza kujadiliwa.
Mmeshlipwa hela mje mtetetee ujinga??

Bandari ya Bagamoyo idea ni nzuri
Lakini kukopa dollars bilioni 20 Kwa mchina Kwa ajili ya bandari ni upumbavu..

Masharti ya mchina ni pamoja na kuiendesha hiyo bandari Hadi pesa yake irudi

Magufuli alikuwa sahihi kusema mkataba ulikuwa wa kipumbavu kabisa...

Tujenge bandari bila kukopa nchi yeyote
 
Tangu lini mtanzania umfundishe na umlee atafuata nyayo zako na maono yako? Nyerere aliwalea wangapi na angalia matokeo. It's genenis
 
mkataba wenye masharti uletwe bungeni ijadiliwe kwa niaba ya wananchi
 
Ndugai anaogopa kufukuzwa kwenye chama muda wowote CCM ina wenyewe
 
Yawezekana kweli ni mradi mzuri lakini inatia shaka kwamba Spika anaupenda mradi huu tangu miaka 5 iliyopita. Sababu kubwa; alifanyiwa presentation akiwa China kwa ziara nyingine, akaongozwa na balozi wetu. Hadi leo haelewi vingine yeye anataka bandari hiyo. Huku ni kukosa aibu kwa Watanzania.

Muhimu kabisa, tulistahili tuambiwe mkataba unsaemaje? Suala siyo mradi, ni mkataba! Je, yeye Spika yuko tayari kutueleza mkataba unasemaje? Tamaa hii ni ile ya fisi aliye na njaa kali, na amekuwa akisubili mlinzi aondoke. Kweli mlinzi kaondoka sasa ni kampeni chakula kiliwe bila kujali kina sumu au la!
Huyu mtu lazima yuko under influence. Kuna kitu alitakiwa akisema hadharani ili wakisikie na apewe zawadi yake aliyoahidiwa miaka mingi. Lazima wanapewa shares. Ni spika asiye na busara. Kwa akili yake hana hasira na baya lolote? Hivi kweli mtu unaweza kuzaliwa ukipenda maovu kiasi hiki?

Naomba nimsingizie kwamba yuko na busara. Kwa busara yake hakuwa mtu sahihi wa kusimama bungeni kuanzisha jambo ambalo taifa liliaminishwa kwamba ni baya. Alistahili serikali ieleze kwa wema kabisa ni nini kimeboreshwa. sasa eti yeye tu kwa kufanyiwa presentation ndo taifa lote likubali? Mtu mwenyewe wa aina hii?

Rais Samia, VP Mpango (mchumi) tunusuru na ujinga huu.
 
Sifa kubwa ya mwanasiasa ni kuwa mnafiki na muongo, lakini ukiwa mnafiki wa kiwango cha juu unakaribia kuwa mchawi.
Ndugai ameeonyesha kiwqango cha hali ya juu cha unafiki na hii inatokana na kukosa hekima na busara.
ndugai alitakiwa kutumia mhimili wake wa bunge kujadili ule mkataba na kumshauri raisi lakini kuunga mkono kipindi kile na kuja kusema baada ya msiba ni unafiki wa hali ya juu na hatakiwi kusikilizwa na kiongozi aliyejaa hekima na busara kama Mama yetu mpendwa Samia.
 
Mwezi Juni mwaka 2019 palizuka mjadala mkubwa sana kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo-Bagamoyo Special Economic Zone (SEZ) ambao Wachina walitaka kuwekeza pale Bagamoyo zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 10 (Trilioni 23) ambazo zingetolewa na Wachina kwa zaidi ya asilimia 90. Wengi waliitaka Serikali kukubali na kuchukua maamuzi ya kuingia makubaliano ya kutekeleza mradi huo haraka iwezekanavyo.

Moja ya watu waliounga mkono na kupigia chapuo mno ujenzi wa Bandari hiyo kwa kutaja sifa kedekede za mradi huo alikuwa ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ambaye alinukuliwa Bungeni akishangaa kwanini Serikali inashindwa kufanya maamuzi ya ujenzi wa Bandari hiyo ambao ungegharamiwa na Wachina kwa kiwango kikubwa huku ikiwa Bandari kubwa zaidi ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Bwana Ndugai anasema alikwenda China na kukutana na hilo kampuni ambalo lilipanga kujenga hiyo Bandari ambapo anasema alichoambiwa na hao jamaa na namna mradi huo ulivyokuwa na faida nyingi alishangaa kwanini Serikali ilikuwa inajivuta kufanya maamuzi ya ujenzi wa Bandari hiyo.

Siku chache baada ya Ndugai kupigia chapuo mradi huo, Rais Magufuli wakati huo aliibuka na kutaja mambo ya ajabu ajabu na hovyo ambayo alinukuliwa kuwa ni kichaa tu ndiye angeweza kukubali yaliyowekwa na hao Wachina kama masharti ya uwekezaji wa ujenzi wa Bandari hiyo. Masharti hayo yalikuwa ni, kwa miaka 33 hakuna TRA kufika hapo kukusanya kodi, baada ya kuanza mradi huo, nchi yetu isingeruhusiwa kuendeleza Bandari yoyote nchi nzima, kuwapa ardhi yetu na kuwapa guarantee ya miaka 99 bila ya kuwauliza chochote, kuwapa fidia ya kuchimba Bandari hiyo na mengine mengi ambayo yaliwashangaza wengi sana.

Baada ya Rais Magufuli kueleza masharti magumu ya mradi huo wa Bandari ya Bagamoyo, mjadala wote wa ujenzi wa Bandari hiyo ulikufa na hakuna aliyepata hamu tena ya kusikia ukijengwa hasa kwa namna ulivyokuwa na masharti magumu na ya ukichaa.

Sasa siku chache baada ya kifo cha Rais Magufuli, Bwana Ndugai ameibuka tena Bungeni na hoja hiyo ya ujenzi wa Bandari hiyo huku akiendelea kuupigia chapuo mradi huo na zaidi akisema Rais Magufuli alidanganywa na wasaidizi wake na kwamba masharti aliyoyataja wala hayakuwa ya kweli na mengi alishauriwa vibaya na wasaidizi wake.

Hoja hii ya Ndugai kudai kwamba Rais alidanganywa na wasaidizi wake kuhusu masharti yale magumu waliyotoa Wachina inazua maswali mengine mengi ya msingi. Kama Rais alidanganywa, kwanini yeye Ndugai kipindi kile kile asingemuomba Rais na kwenda kusahihisha hapo anaposema Rais alidanganywa? Kwanini asubili Rais amefariki ndipo aibuke kutaka mradi uendelee kisa Rais alidanganywa?

Zaidi Bwana Ndugai anapigia debe mradi huo kwa kile anachosema fedha karibu zote za mradi zitatolewa na Wachina huku akisema Wachina walimwambia wanatushangaa kwanini hatuchukui maamuzi ya ujenzi wa mradi huo sasa na haraka kabla ya hao Wachina hawajastaafu kwenye hiyo kampuni. Kwa lugha rahisi Ndugai anashinikiza mradi huu ufanyike haraka kana kwamba yeye kuna kitu kinakwama mradi usipofanyika. Unaweza kudhani ni kama Ndugai amepewa chochote kitu na Wachina kuhakikisha mradi huu unatekelezwa na usipotekelezwa yeye mission yake inakufa.

Mimi namshangaa zaidi yeye, hivi ni toka lini Mataifa haya yakaweka fedha zao Mabilioni mengi hivi kama hawajaona faida yao? Ndugai anataka kusema mradi huu una manufaa sana kwetu kuliko wao? Kwamba Wachina wanaona tunakosa faida sisi kuliko wao? Well!

USHAURI WANGU KWA SERIKALI KUHUSU MRADI HUU

Kwanza, mpaka sasa Serikali imeweka fedha nyingi sana kwenye uboreshaji wa Bandari zetu kuu 3 za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga na karibu Bandari zingine zote nchi nzima kwahiyo mradi huu sio mgeni au kwamba hatuna kabisa kiasi cha kwamba tunahitaji sana huo, nchi hii ni moja ya Mataifa machache duniani imebarikiwa Bandari nyingi na za kutosha sana kwahiyo hatuna haja ya kukurupukia kitu kama vile hatunacho kabisa wakati tunacho. Tunahitaji kujiridhisha.

Binafsi natamani sana kila eneo lililopitiwa na bahari liwe na Bandari kubwa na ya kisasa ili kuinua uchumi wa nchi yetu na watu wa maeneo hayo lakini tunahitaji umakini mkubwa sana kuingia mikataba hii mikubwa (grand project) ya matrilioni mengi mno. Sipingi mradi huu mkubwa wa uwekezaji wa Bandari kwa ukanda wa Bagamoyo lakini tunahitaji umakini sana kwani tunafahamu makampuni makubwa kama haya hayawezi kuweka hela nyingi kiasi hiki sehemu kama hawajaona faida na interests zao zaidi.

Serikali sasa inatekeleza miradi mikubwa ya ukarabati na uboreshaji wa Bandari zetu zote kuu za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga na zote za maziwa yetu Makuu pale Victoria, Tanganyika, Nyasa na nyingine nyingi. Matrilioni mengi yamewekwa kuboresha Bandari zetu, kwangu ni bora Serikali iendeleze zaidi hizi zilizopo ambazo tuko nazo na umiliki wote kuliko kuingia ubia na mikataba hii mikubwa na haya makampuni ambayo tunajua mengi yamekuwa yakiangalia zaidi faida zao wao kuliko zetu

Kama tunataka kuingia hii mikataba ya grand project kubwa namna hii basi mikataba yake iwe wazi na ikaguliwe kwa umakini kwa kila kipengele na iwe kweli yenye manufaa kwetu kama nchi na sio kuingia mkenge wa mikataba mibovu itakayogharimu vizazi vyetu na vijavyo huko mbele.

Tusiingie mkenge wa kutekeleza hii miradi kwa msukumo wa mtu au watu fulani ambao inawezekana wana interests binafsi kwenye miradi hii. Ndio maana nasema Bwana Ndugai asitake kutupeleka jalalani na kutuingiza mkenge, tujiridhishe kwa umakini sana then tufanye maamuzi. R.I.P JPM

ASANTE JOHN
 
Sina uhakika Ila Maghufuli alitaka hao wachina wamsupport kwenye SGR badala ya bandari , istoshe isingempa sifa yyte sababu ni idea za Mzee wa msoga. Nao wakaingia mitini baada ya kuona SGR haina manufaa na ni complete loss hasa kwenye operations zake ukilinganisha na Bandari, Sina uhakika Sana Ila JPM alipiga U-Turn.

Ukweli ni kuwa jiwe hakutaka kuingiliwa ndo mana wasaidizi wake walimsupport ili wapate pa kula, Ndugai yupo sahihi ,mradi uangaliwe upya. Pengine Yule mchina aliyeenda chato alikuja na mission yake ya kummaliza jiwe. Nawaza Tu lakini
 
Sidhani kama kuna haja ya kujiuliza kuhusu ndugai na matendo yake.

Kiongozi kama yeye anatakiwa kutawaliwa na hekima na busara kitu ambacho nina wasiwasi nacho hasa nikikumbuka matendo yake.
Kwanini hakutumia bunge lake kujadili huo mkataba na kumshauri Magu? Kwanini sasa ndio anashauri?

Naamini kabisa Mama yetu Raisi Samia hawezi kuchukua ushauri wa watu kama hawa ambao hawaaminiki na hawana msimamo.
 
Mnafik yule
Mzee mzima ovyoo kabsaa
 
Nasikia tena anataka aruhusiwe kununua mabehewa ya treni kama shares zake! Huyu ni tatizo! anaamini ni kama anavyoegesha mabasi yake kampuni fulani vile na kuletewa nauli ya abiria? Kama huyu ni spika anayewaongoza wanaopiga makofi, basi tuko kiwango cha ufahamu duni sana!
 
Jalalani leo ni neno tata. Usisahau alikotolewa Prof kabudi nako ni almaarufu kwa jina hilo hilo.
 
Jalalani leo ni neno tata. Usisahau alikotolewa Prof kabudi nako ni almaarufu kwa jina hilo hilo.
Nje ya mada, kama Kabudi alitoka jalalani si inamaanisha Kabudi ni takataka? Kama UD ni jalalani si inamaanisha waliopo pale ni takataka?
 
Back
Top Bottom