Ndugu Nape pokea mchanganuo wangu wa dola 9 billioni alizokula Magufuli


HONGERA SANA SANA PIA WATAKUKATALIA NIA YA NAPE SIO KUJUA NIA YAKE NI KUMCHAFUA JPM KABISA NA UBAYA VIONGOZI WAPO KIMYA WALIOKUWA WANAMSAPOTI MAKUFULI SIJUI KWANINI HAWAINUI MDOMO NA KUSEMA PILI MKAGUZI WA MAHESABU ATAKAPOCHUNGUZA HATASEMA UKWELI ATAVURUKA KWA KUFUATA MATAKWA YA WACHACHE
 
Waew mshenzi tu, aliitangqzia dunia kuwa hakopi anajenga kwa pesa yake. Mbona una mahabaaa ya kipambaf???usijitoe ufahamu wewe
 
Unavyojenga nyumba yako kwa hela ya uliyotoa benki.
Hapo unakuwa umetumia hela yako au ya benki?
Hoja ni kuwa jpm, alikuwa akiwaaminisha watu kuwa hakopi pesa bali ni pesa zinatotokana na makusanyo yetu, na ndio maana alikuwa akiulizwa inakuwaje sasa mbona deni la taifa linazidi kukua, anakuwa mkali!!kama una pesa yako inayojitoshereza utakwenda bank kuchukua mkopo wa kujenga nyumba?
 
Tutakuwa tumepigwa Bilioni 9 tumiradi twenyewe ndo huto tu SGR, kabwawa ka Rufiji, tundege, tuflyover kweli? afadhali wao na JK walikopa Bilioni 7 wakaanza kukwetua uwanja wa ndege wa Dar na kumwaga mchanga na kokoto pale kwenye m-flyover wa TAZARA.
Tuchunguze tu!
 
Mkuu sio in bilions ni milions$$$
 
Ndugu yangu NAPE,
Rais Magufuli kafa,whatever he was it has gone with him, like a candle in a wind.Magufuli was not a dictator neither a sadist, Nothing.
HATRAGE Wont take you anywhere,Learn to to forgive and forget ,its good for your health.
Forget there is no Comeback.
 
Ingependeza ungejibu hoja moja moja. Na me mi sio Nape.
1. Been Saanane yuko wapi? Tungependa apatikane ahojiwe kuhusu aliyosema juu ya PhD ya Magufuli, na sio apotezwe.
2. Tungependa kujua kwanini cag Prof Assad alisitishwa kazi kabla muda wake haujaisha. Na je I'll 1.5T aliyosema haionekani (= imeibiwa) ilienda wapi?
3. Tungependa kujua kina nani walimpiga risasi Tundu Lissu. Uchunguzi uliofanyika kubaini waliefanya huo uhalifu? CCTV camera zilizokuwa kwenye makazi ya Lissu na viongozi wengine nani vamezificha?
4. Tungependa kujua David Mwangosi yuko wapi?
5. Tungependa kujua mwaka 2019 Tanzania kulikua na covid19 au ugonjwa haukuwepo? Je ni kweli sample za mapapai, oil chafu etc zilipatikana na covid19?
6. Tungependa kujua kwanini audit ya miradi/mashirika eg atcl haikufanyika? Je taratibu za manunuzi ya umma zilifuatwa?
7. Etc etc.
 
Wewe huelewi.Uchunguzi ufanyike kwanini mikopo ilichukuliwa kimya kimya huku tukidanganywa ni fedha za ndani.Issue sio miradi iliyoanzishwa bali nini kimejificha hadi kupelekea mikopo ya gizani?

Hapakuwa na nia ovu kukopa kwa siri?
 
Wewe huelewi.Uchunguzi ufanyike kwanini mikopo ilichukuliwa kimya kimya huku tukidanganywa ni fedha za ndani.Issue sio miradi iliyoanzishwa bali nini kimejificha hadi kupelekea mikopo ya gizani?

Hapakuwa na nia ovu kukopa kwa siri?
Nakuunga mkono hata tumiradi twenyewe tunaonesha tumepigwa. we Bil 9 tumiradi twenyewe tu-bwawa na tu-SGR, tuflyover na tundege tundege tu?
 
Usijumlisha inferiority complex yako na watu wengine, we sema ningependa kujua(wewe kama wewe).
 
Nakuunga mkono hata tumiradi twenyewe tunaonesha tumepigwa. we Bil 9 tumiradi twenyewe tu-bwawa na tu-SGR, tuflyover na tundege tundege tu?
Ndo hivyo yaani jamaa alikuwa msanii sana ila kwa ambao hawakumjua aliwadanganya kwa gia ya wanyonge.
 
Huna akili kabisa.

Mkopo utalipwa na sisi kwa kodi zetu
Wewe ni mmoja wa watu wa hovyo wa taifa hili. Unayemtetea alimaanisha kuwa tunaweza kufanya miradi hii wenyewe kwa fedha zetu wenyewe kupitia kodi kwa sababu sisi ni nchi tajiri!! aliposema "fedha za ndani" alimaanisha kile kile kinachosemwa bungeni kama "makusanyo". JPM alimaanisha fedha tunazo za miradi hii (kwa makusanyo ya kila mwaka mpaka miradi kukamilika). Kumbe hatukuwa na fedha ndio maana akakopa ili tulipe kutoka kwenye makusanyo!!

"Fedha za ndani" ilikuwa ni propaganda iliyoweza kuwanasa wasio werevu. Waliaminishwa tutatumia kodi zetu kufanya miradi, baadae wanaamini kuwa mikopo itarejeshwa na kodi zetu wenyewe na hizo ndio "fedha za ndani". Maana mpya mliyopata maboya ni kuwa alimaanisha "hatutajenga kwa misaada". Hivi pamoja na ujinga wako, unaamini mtu angekujengea miundombinu yote hii kwa "misaada"??

Siku watu kama ninyi mkipungua katika nchi hii - ndio tutaanza kusonga katika nchi hii. Wewe ni kielelezo sahihi kwanini tunakwama!
 
hawa wote walibanwa magoda kipindi kile kwelikweli...sasahv naona kaoxygen kanapita kwenye boxa zao,maneno kibao!! Walikuwa wapi muda ule.
 
Si uache CAG afanye kazi yake?

Hakuna usukuma kwa sasa, nchi iko mokono salama syo ile ya fisadi wa kisukuma
Unakakumbuka kale kamkataba ka Jana Kati ya TANESCO NA WAHINDI, hicho ndio watanzania mnakitaka,msidhani kumkashifu Magu, wasukuma kutawasaidia kitu,wanaulaumu mwezi ili wote mtizame juu mkija kushusha macho chini nyama yote itakuwa imevuja umebaki mchuzi๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
 
Huna akili kabisa.

Mkopo utalipwa na sisi kwa kodi zetu
Mkopo ni mkopo tu; sio hela za ndani. Mkopaji unaweza ukashindwa kulipa ukasamehewa au ukapunguziwa deni na/au ukarahisishiwa masharti ya kulipa au ukafilisiwa kabisa. Utaweza kudai umetumia hela zako (sio za ndani) ukimaliza kulipa deni.

Hela za ndani ni akiba iliyotokana na malipo ya mauzo yako ya bidhaa na huduma.

Kukopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo hadi kwenye mabenki ya biashara na kutangazia umma kuwa tunatumia hela zetu za ndani ni kauli ya kisiasa - propaganda.
 
Na yeye tutampima kwa pesa ile Jimbo anayopewa Mbunge.
Tangu awe Mbunge kasaidiaje jamii.
Chuki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ