Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

... huko kwenye hoteli za stendi nako bei itapanda. Tena wamepewa monopoly ndio balaa kabisa; wanajua basi ipende, isipende itakuja hapa not only bei lakini huduma zitakuwa mbovu ajabu.

Muhimu mkata tiketi ataarifiwe mapema hoteli ambayo basi litasimama kwa ajili ya chakula ili aamue kukata ya basi hilo au lingine. Hii itaondoa monopoly na nguvu ya kuamua itakuwa imerudishwa kwa abiria hivyo hoteli zitashindana both in terms of price and QoS.
Kutakuwa na ushindani. Na kukiwa ma ushindani bei na huduma zitakuwa rafiki. Kumbuka mabasi yakiwa yanasimama stendi basi mfanya biashara yoyote ana uhuru wa kufungua huduma kwenye eneo husika. Tunarudi kule kule kwenye kanuni yetu. Supply itakuwa kubwa na demand ndogo hivyo bei na huduma zitakuwa nzuri. Sasa hivi wanapotupeleka kwenye hizo hoteli zao ndiyo wanatupiga bei wanayotaka tena kwa kuringa. Umezaliwa lini? Zamani wakati mabasi yanasimama stendi huduma zilikuwa nzuri na bei pia.
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.

Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.

Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.
Unafahamu huduma zinazotolewa kwenye vituo binafsi?? Kwa uchache kule kuna huduma za vyoo visafi na maji ya kutosha. Maliwato na sehemu Safi ya kula. Huduma zote hizo ni bure. Hata usiponunua chakula BADO utapata huduma za vyoo na maliwato bure kabisa, mnategemea Bei iwe ya chini?? BADO stand zetu za mikoa hazina miundo mbinu ya kutosha kuweza kuhudumia mabasi ya safari za mbali kwaa huduma za chakula Safi. Nashauri watu wangehimizwa kubwa vyakula majumbani mwao Kama hawawezi kununua vyakula vyaa Ile Bei. Otherwise tutasababisha magonjwa ya milipuko. Hivyo vituo vya una vibireshwe kwanza
 
... LATRA iweke classification kwenye haya mabasi; yatambulike from the beginning kabla msafiri hajakata tiketi kwamba hili ni la kusimama stendi muda mrefu na hili ni la private hotels kama ilivyo Daraja la 1, la 2 na la 3. Unajua kabisa nikipanda basi hili mahala pa kula ni Stendi ya Kibaigwa, hili ni private hotel, n.k.

Pia bus owners walazimishwe kuwa taarifu abiria kabla ya kukata tiketi, jina la hoteli ambalo basi husika linatarajia kusimama kwa ajili ya chakula na sio utashi wa dereva anawapeleka sehemu za ajabu ajabu analizo na maslahi nazo.
Point
 
Mabasi yasimame kwenye stendi kubwa za wilaya na mikoa kwa ajili ya kula na kujisaidia. Kwa kusimama kwa ajili ya kula angalau nusu saa liwe stendi na iwe basi limetembea si chini ya masaa 6 toka kuondoka alfajiri. kwa kisimama kwa ajili ya kuchimba dawa ni kwenye stendi zingine zote zenye huduma hio ni angalalu zisimame mda wa robo saa. Pia wapunguze bumps njiani na spidi iongezwe angalau spidi 100/hrs. Kwenye zebra waweke madaraja ya kukatisha barabara kwa chini.
 
Hizo hotel waweke bei reasonable maisha ya watz yanafahamika na si KILA anaesafiri anaenda kwenye raha, wengine wamakurupushwa awakujipanga nauli tu ya kukopa au kuchangiwa mfano chips sahani 7000 Ina kipi cha ziada.
 
Mabasi yasimame kwenye stendi kubwa za wilaya na mikoa kwa ajili ya kula na kujisaidia. Kwa kusimama kwa ajili ya kula angalau nusu saa liwe stendi na iwe basi limetembea si chini ya masaa 6 toka kuondoka alfajiri. kwa kisimama kwa ajili ya kuchimba dawa ni kwenye stendi zingine zote zenye huduma hio ni angalalu zisimame mda wa robo saa. Pia wapunguze bumps njiani na spidi iongezwe angalau spidi 100/hrs. Kwenye zebra waweke madaraja ya kukatisha barabara kwa chini.
Nani atakekaa kumonita hizo dakika Basi limekaa na kama ujuavyo sheria au katazo lolote ni fursa kwa wasimamizi wa sheria au katazo hilo.
Muhimu wamiliki wa mabasi wawe royal
 
Bei elekezi ya nini kwani bei za vyakula vya kitanzania haijulikani?, wamejenga hotelier maporini huko ili abiria wakose alternative.Dawa ni kuwalazimisha wanapoweka vyakula vya nyota 5 waweke na vya kawaida. Chakula ni huduma ya lazima kama kuchimba dawa. Hatari ya kupaki standin ni wizi kwenye mabasi na wakiweka vyakula vya bei za kawaida ndo matajiri nao watahamia huko🤣
 
Bei elekezi ya nini kwani bei za vyakula vya kitanzania haijulikani?, wamejenga hotelier maporini huko ili abiria wakose alternative.Dawa ni kuwalazimisha wanapoweka vyakula vya nyota 5 waweke na vya kawaida. Chakula ni huduma ya lazima kama kuchimba dawa. Hatari ya kupaki standin ni wizi kwenye mabasi na wakiweka vyakula vya bei za kawaida ndo matajiri nao watahamia huko[emoji1787]
Hoteli za stand zina weza hudumia magari mangapi at ago? Ina hitajika miundombinu mipya kabisa sio siasa
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.

Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.

Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.
Tatizo ni aliyependekeza,angependekeza wa upande mwingine ndiyo hoja ingekuwa na mashiko.
 
Kuna hoja ameiwasilisha Polepole kwenye television (chanel 10) kipindi Cha papo kwa papo nakuungwa mkono na Mhe Waziri kwamba vmabasi badala yakwenda kwenye hoteli zenye hadhi na chakula salama wawapo safarini Basi mabasi hayo yasimame kwa muda mrefu stand watu wale chakula nakupata huduma nyingine.

Haya maamuzi ni maamuzi yanayosukumwa na watendaji ambao wanatumia mashangingi ya serikali na chama na ambao hawapandi bus kwenda popote. Leo hii vituo vya mabasi vinafahamika, havikujengwa kwa lengo lakutoa huduma ya chakula kwa abiria bali vimejengwa kama points zakusubirua abiria wapande na kushuka. Vituo hivi vina matundu machache sana yakujisaidia na huduma hii inagharamiwa huku kukiwa hakuna usafi Wala maji yakutosha. Standard yavituo vyetu haikidhi viwango vyakuhudumia abiria labda tuingie kwenye uwekezaji mpya wa kuvikarabati

Turudi kwenye gharama ya chakula, gharama ya chakula inategemea na eneo unapopata huduma. Inashangaza Leo hii uniambia gharama ya Serena hoteli ilingane na gharama ya mama ntilie kisa wananchi wamelalamika.

Kama tutataka kuweka usawa tufike pointi tujadiliane na watoa huduma, wale wamioiki wanaopenda wakae stand muda mrefu wajitangaze ili abiria wajue bus ili linasimama stand kwa ajili ya chakula na bus ili linasimama hotel binafsi kwa ajili ya chakula....abiria wachague watapanda gari gani lakini si kulazimisha watu wote waishi, wasafiri na kula kwa maelekezo ya Waziri.

Polepole umechemka acha siasa kwenye huduma, pokea kero wakabidhi vijana wa chama wazifanyie utafiti the waishauri serikali njia inayofaa siyo kumlazimisha Waziri atoe msimamo wa kisera kwenye media.....w
Naona Ndg yangu Beatrice ema hujui biashara au weye hujasafiri. Hoteli unazozisema zote zinamilikiwa na wenye mabus, siyo wawekezaji wenyeji wa eneo husika, mathalani Korogwe. Yes, ni monopoly pricing; yes, Polex2 is right - wewe msafiri unataka fastfood, na fastfood dunia nzima ni cheap. I suspect wamiliki wa hoteli hizi wengi ema ni Chadema au ni sympathisers wa Chadema. Kwa hiyo sitashangaa na weye ukilichukulia kisiasa.
 
Polepole yuko sahihi wakifanya hivyo kwenye stand kutakuwa na hotel nyingi zitakazoshindana ubora
Nimeanza kuamini haya malalamiko yameanzishwa na kina Polepole na kundi lake. Stendi ya Msamvu inaweza kulisha wasafiri zaidi ya 10000 wanaopita pale kwa siku?
 
Nimeanza kuamini haya malalamiko yameanzishwa na kina Polepole na kundi lake. Stendi ya Msamvu inaweza kulisha wasafiri zaidi ya 10000 wanaopita pale kwa siku?
Stand inatakiwa kuwa na huduma zote zikiwemo choo, chakula na malazi sioni tatizo kama wakipita stand
 
Bei elekezi ya nini kwani bei za vyakula vya kitanzania haijulikani?, wamejenga hotelier maporini huko ili abiria wakose alternative.Dawa ni kuwalazimisha wanapoweka vyakula vya nyota 5 waweke na vya kawaida. Chakula ni huduma ya lazima kama kuchimba dawa. Hatari ya kupaki standin ni wizi kwenye mabasi na wakiweka vyakula vya bei za kawaida ndo matajiri nao watahamia huko🤣
Wewe una akili kuliko Polepole.
 
Chanzo cha vyakula vibovu na vya gharama , ni kutokana na wenye hzio sehemu kuhonga madereva wa mabasi na hivyo kupata uhakika wa wateja kilazima ,
Kuvunja vyunja hii ni rahisi sana , kila basi lieleze watasimama wapi kwa ajili ya chakula kabla ya safari au wakati abiria anakata tiketi .mabasi yanayosimama sehemu ghali yatakosa abiria na hizo hotel pia zitakosa wateja , mabasi yanayosimama sehemu nzuri yatapata abiria na hoteli hizo pia zitapata wateja, hii itasawazisha Bei za vyakula Mara moja .
 
Hizi ni ndoto za alinacha..mabasi kama KLM yaende kusimama kwenye vistendi vya ovyo ovyo..? Kila basi Liwe na hotel yake kama KLM anavyofanya
Hakuna ndoto mkuu serikali ikiamua itakua tu,tena hao jamaa wa hovyo sana hawaruhusu hata watu kuingia na chakula ndani ya Bus. Pale ni udikteta mwanzo mwisho usipokula unakufa na njaa,bei ya chini chakula buku 8. Labda unywe chai au biskuti.
 
Kwa hiyo unataka kudhania kuwa wakiwa wanakaa stendi ili kupata chakula hawatakula bure? Tumia akili bro kabla ya kutetea upuuzi.
Utakaaje stendi kula wakati mnaondoka asubuhi na safari ni Zaid ya masaa 12, hata ukila asubuhi lazima mchana utasikia njaa unajua pole pole akili Hana
 
Back
Top Bottom