Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!
Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.
Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!
Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.
Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.
Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.