Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

Hata ukiwaambia kuwa punguzeni hawakusikilizi kabisa mkuu.
Yaani na huku namie ni machinga najuaga biashara zilivyo.
Huko stendi vijana wauza matunda watajiajiri kwa wale tunaosafiri tu nakula matunda tutanunua kwa maringo makubwa sana.
Kuna muda unaambiwa kuwa chungwa sh 300 nawaangalia nawaacha wao wanajuaga kuwa wasafiri Hela zao ni nyepesi ama zinapatikana kiulaini ,hawajui kuwa wapo wanaosafiri kwa shida wanajua wote wana uwezo
 
Ushauri wangu kwenye hili suala ni kwamba,
Kwa kuwa stendi zote mabasi yanaposimama ni Mali ya serikali kupitia wakurugenzi wa halmashauri.
Hivyo Basi waagizwe Mara moja wahakikishe hizo hoteli zinajengwa pamoja na vyoo vizuri ambapo chakula kitakuwa kinauzwa katika mazingira reasonable standard na Bei nafuu na pia huduma ya choo kwa wasafiri iwe bure
Pia usalama uongezwe kwenye hizo stendi
Nimesafiri Sana hii nchi nimekutana na stendi za ajabu ajabu Sana huko mawilayani huduma za vyoo mbovu halafu unalipia
 
... kama hizo ndio bei acha kutumia hayo mabasi; tumia mabasi mengine yanayopaki sehemu zenye vyakula vya bei nafuu. Ni kwa jinsi tutawalazimisha kushusha bei zao za vyakula kwani watakosa wateja. Acha kulialia, uamuzi ni wako.
Wewe unaikosoa serikali kila siku halafu leo unakuwa kama serikali hiyo unayoikosoa. Una hisa kwenye hizo hoteli nini? Au hujui undani wa hizo hoteli? Zamani mabasi yalikuwa yanasimama stendi na kulikuwa na huduma nzuri tu. Baadae wakaingia ''wajanja'' wachache ambao walijenga hoteli mbugani na kupanga na wenye mabasi wawe wanapaki kwenye hizo hoteli. Walichofanya ni kuwapa madereva na wasaidizi wao chakula na vinywaji vya bure na posho juu. Hawakuwa na wasiwasi kwani bei ya vyakula vyao walipanga wanavyotaka kwa sababu hakuna ushindani. Baadae wenye mabasi nao wakajanjaruka wakaona wajenge zao na kupaki mabasi yao kwenye hizo hoteli. Sasa serikali imeamua utaratibu urudi kama zamani na magari yapaki stendi. Sasa kama wenye mabasi wanataka basi wanaweza kufungua hoteli maeneo ya stendi na waingie kwenye ushindani na wafanya biashara wengine.
 
Wenye hizi hoteli Kama KLM ndo wameua hoteli Kama LIVERPOOL kwa kuhongwa kwao vyakula vya bure ili wapeleke abiria huko.

Zamani njia ya Arusha-DSM ulikua unapita zako LIVERPOOL inachukua vimishikaki vyako viwili vitatu na vichips saafi unaendelea na safari.

Sa hivi Kusafiri imekua anasa kubwa Sana,unaandaa bajeti isopungua 20000 ya matumizi njiani,iwe wakati wa raha ama matatzo.

Kuuziwa chips vidogo Tena vimekaangwa vbaya vbaya na nyama liloungua kwa 7000 haikubaliki.Kuuziwa wali/ndizi nyama kwa 7000/10000 pasipo hazi haikubaliki.

Lazima hizi hoteli wabadilike maana malalamiko ya abiria humu mitandaoni na hata mtaani haswa wakati wa Kusafiri Ni makubwa na yanasononesha Sana.Ndo Mana abiria wengi siku hizi wanapiga dashi tu.

POLEPOLE NAKUPA BIG UP SANA WABADILIKE HAO,SI WANASINGIZIA HUDUMA YA CHOO CHA 300 NA KUWALANGUA WATU KWENYE CHAKULA.

Nachukua Sana
 
MIGAHAWA MABASI YANAPOSIMAMA:
1.Chips robo na kibawa cha kuku mchina shs 7,000/-
2. Wali kwa ng'ombe shs 5,000/-
3. Andazi shs 1,000/-
4. Chapati shs 1,000/-
5. Soda/maji 500ml shs 1,000/-
nb; Msalani ni bure.

Aya simama labda pale mombo njia panda;
1. Chips kwa kuku 3,000/
2. Wali kwa ng'ombe shs 2,500/-
3. Andazi, Chapati nk shs 300/500/-
4. Maji 500ml 500/- Soda 500/1000/-
nb; msalani shs 300/-


NB: Vaa barakoa, kaa mbali na mikusanyiko, osha mikono kwa sabuni au tumia kitakasa mikono.
 
Watu watapewa zabuni bana wachukue 200 200 mkuu ya usafi kama vipi nichukue iyo tenda nchi nzima sema baadaye kunatokeaga figisu ukishaboresha MTU mkubwa sirikalini anapachukua. Iyo inataokeaga kwa vyoo vingine hapa nchini.
Kuna MTU Wangu Wa karibu alikuwa anajikusanyia karibia 60k kwa siku akafanyiwaga figisu ujue akatolewa na waliosoma wamepewa dhamana ya madaraka ya wananchi wakayatumia lama wanavyojua
 
Watangaze zabuni kwa ajili ya mahotel kulisha abiria kama hujaona mahotel yakijitokeza na bei rafiki kazi ya serikali iwe ni kukagua ubora

Jambo hili ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii na hatua hii itakomesha rushwa waliyokuwa wanapewa madereva wa gari za abiria , waziri na mr polepole shikilieni hapohapo ili ugonjwa huu uishe sambamba na corona
 
Watanzania tunalalamika sana aisee...yakipita hotel binafsi tunalalamika, yakipita stand tunalalamika...do we even know what we want? au ndo bendera fuata upepo?
Kila mkoa now unajenga stand kubwa na za kisasa, nadhani its best wenye mahotel wa hamie huko, abiria wapate afforable & quality service coz ya ushindani wa watoa huduma at the same time serikali ipate kodi ya pango...Chukulia mfano stand mpya ya Dodoma ina space km loote.
 
We wa ajabu. Angalia uwekezaji uliofanyika kabla ya kusema maudhi yako
 
In free market huwezi fanya huo ijinga
 
Nimeanza kusafiri na wali wangu kwenye chombo, maji ya bei nafuu na juisi ya bei nafuu.

Hii ni mara ya pili sasa nafanya hivi, njiani natenga bajeti ya vingine ila si chakula wa kinywaji
 
nanyinyi hamueleweki , simlikuwa mnalalama kuwa kwwnye mahoteli ambako mabasi yanasimama vyakula bei mbaya
 
Vyakula lazima wauze ghali sababu huduma za vyoo Safi, maliwato, maji ya kutosha, hivi stand zetu zinaweza kuhudumia bus 10 KWA wakati mmoja?? KWA vyoo na huduma nyingine??? Inahitajika miundombinu na mikakati ya muda kuweza hii, lakini wakianza ghafla tu, magonjwa milipuko yatakuwa Mengi Sana. Watu wabebe vyakula kutoka majumbani kwao. Tena huko mastand KILA mtu alienda kula kivyake wataachwa naa bus KWA kuchelewa. TBS WAENDE wahakikishe ubora wa vyakula vya hayo mahoteli, na wahimizwe vyakula viwe visafi na vitamu
 
Kwani hizo hotel zinamudu vipi magari mengi kilichopo ni wizi wa kuibia abiria kama wangekuwa wanafanya kwa haki wasingekuwa wanahonga madereva ili wawaletee abiria
 
Pole pole hongera sana kwa hili mabasi yasimame siendi siyo kwa hawa walanguzi.uamuzi huu imechelewa sana.zamani ilikuwa hivyo tunasimama siendi.serikali nimejenga siendi karibu kila mkoa.hizo changamoto ndogo ndogo zitajirekebisha automatically.toa mwezi mmoja wa maandalizi then tuanze.kwanza hii inaakisi sera yetu ya chama ya kumjali mnyonge.mabasi yasimame siendi ya korogwe.mombo.gairo.dodoma.singida.igunga.nzega.kahama.nk.manufaa.ajira.unafuu.ushindani.uwannja mpaka kwa abiria kuchangia atakacho au anachokimudu kulingana na hali yake.stay blessed.
 
Inafahamika kwamba,Hawa wenye hotel ambazo mabasi yanasinama na vyakula kuuzwa ghali wamiliki wa hizo hotel Wengi wao Ni hao hao wenye makampuni ya mabasi.Mfano njia ya DAR-ARUSHA,Mwenye hotel za Kilimanjaro ndiye mmiliki wa mabasi ya Kilimanjaro.Mwenye hotel ya Dar Express ndiye mmiliki wa mabasi ya Dar Express n.k.Hawa wanalazimisha kutengeneza" Super Profit" kwenye Hizo hotel wanazomiliki kwa kuwa gari ikishasimama hapo,haisimami sehemu nyingine Tena kwa ajili ya vyakula,Hadi mwisho wa safari.
USHAURI WANGU:Hao wenye hotel zinazouzwa vyakula Bei kubwa,Serikali iwabane wajenge pia HOTEL ZA KUUZA VYAKULA KWA BEI YA WASTANI kwenye ENEO HILO HOLO moja. (e.g.wali Nyama na mbogamboga shs 3,000 kwa sahani badala ya sh 8,000 wanavyouza kwa sasa.Chipsi kavu na Robo kuku sh 4,000 badala ya sh 8,000 wanavyouza kwa Sasa.Andazi iwe sh 500 badala ya sh 1,000.Chai rangi sh 500 kikombe vs 1,000 wanavyouza Sasa n.k.) .Kwa Hiyo bus likisimama hapo,Abiria ataamua mwenyewe aingie hotel ya ghali au ya kawaida.HAPO TUTAKUWA TUMEPATA JIBU LA HILI TATIZO.
 
Hizi ni ndoto za alinacha..mabasi kama KLM yaende kusimama kwenye vistendi vya ovyo ovyo..? Kila basi Liwe na hotel yake kama KLM anavyofanya
Kuuza vyakula kwa 8000 ni hela nyingi bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…