Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

Kuna hoja ameiwasilisha Polepole kwenye television (chanel 10) kipindi Cha papo kwa papo nakuungwa mkono na Mhe Waziri kwamba vmabasi badala yakwenda kwenye hoteli zenye hadhi na chakula salama wawapo safarini Basi mabasi hayo yasimame kwa muda mrefu stand watu wale chakula nakupata huduma nyingine.

Haya maamuzi ni maamuzi yanayosukumwa na watendaji ambao wanatumia mashangingi ya serikali na chama na ambao hawapandi bus kwenda popote. Leo hii vituo vya mabasi vinafahamika, havikujengwa kwa lengo lakutoa huduma ya chakula kwa abiria bali vimejengwa kama points zakusubirua abiria wapande na kushuka. Vituo hivi vina matundu machache sana yakujisaidia na huduma hii inagharamiwa huku kukiwa hakuna usafi Wala maji yakutosha. Standard yavituo vyetu haikidhi viwango vyakuhudumia abiria labda tuingie kwenye uwekezaji mpya wa kuvikarabati

Turudi kwenye gharama ya chakula, gharama ya chakula inategemea na eneo unapopata huduma. Inashangaza Leo hii uniambia gharama ya Serena hoteli ilingane na gharama ya mama ntilie kisa wananchi wamelalamika.

Kama tutataka kuweka usawa tufike pointi tujadiliane na watoa huduma, wale wamioiki wanaopenda wakae stand muda mrefu wajitangaze ili abiria wajue bus ili linasimama stand kwa ajili ya chakula na bus ili linasimama hotel binafsi kwa ajili ya chakula....abiria wachague watapanda gari gani lakini si kulazimisha watu wote waishi, wasafiri na kula kwa maelekezo ya Waziri.

Polepole umechemka acha siasa kwenye huduma, pokea kero wakabidhi vijana wa chama wazifanyie utafiti the waishauri serikali njia inayofaa siyo kumlazimisha Waziri atoe msimamo wa kisera kwenye media.....w
Unajua fair competition wewe??? Au una bwabwaja tu ????? Trade is an issue ya kuwa fair kwa seller na kwa customer na kuwa na choice.
Nchi za wenzetu unaposimama kwa hayo mahitaji kuna supermarket, kuna Mac Donald , kuna kfc, na nyinginezo, sasa hapa kwetu na mtu moja ame block wengine , hakuna choice
 
Stand inatakiwa kuwa na huduma zote zikiwemo choo, chakula na malazi sioni tatizo kama wakipita stand
... ni kwanini stendi hazina hizo huduma kwa sasa? Chama kinachotawala bado si kile kile toka uhuru?
 
Hakuna ndoto mkuu serikali ikiamua itakua tu,tena hao jamaa wa hovyo sana hawaruhusu hata watu kuingia na chakula ndani ya Bus. Pale ni udikteta mwanzo mwisho usipokula unakufa na njaa,bei ya chini chakula buku 8. Labda unywe chai au biskuti.
... kama hizo ndio bei acha kutumia hayo mabasi; tumia mabasi mengine yanayopaki sehemu zenye vyakula vya bei nafuu. Ni kwa jinsi tutawalazimisha kushusha bei zao za vyakula kwani watakosa wateja. Acha kulialia, uamuzi ni wako.
 
Pamoja na hayo lakini hii ni hatua nzuri kabisa. Wengi tumekuwa tunalalamika hapa mabasi yanatupeleka hoteli ambazo bei zao wanapanga bila kujali kwani wanajua hakuna ushindani na abiria hana sehemu nyingine ya kula. Wakihamia stendi watajitokeza watu wengi wataokajenga au kuimarisha hoteli za stendi kama zamani.
Imagine kwenye hzo hotel chips na nyama elfu Saba, ni Raia gani ana afford hyo hela, na hawana option ya kula chips kavu wakati kitaa chips ni bei nafuu. Hii ya kupita stendi itasaidia wasio na fedha kutokutumia gharama kubwa
 
Hizi ni ndoto za alinacha..mabasi kama KLM yaende kusimama kwenye vistendi vya ovyo ovyo..? Kila basi Liwe na hotel yake kama KLM anavyofanya
Klm hotel yao chakula kibaya chips elfu saba nyama haziivi, imagine chips zinalendemka ka mlenda. Nadhani serikali iwaonyooshe Hawa wamiliki
 
Sio kila kitu ni siasa unaweza kukuta wenye hotel ni wafadhiliwa chama tofauti na chama tawala
... Chama tawala kinatakiwa kitoe na kusimamia utekelezaji wa sera za kumsaidia mwananchi wa chini kupata huduma bora na nafuu na sio kauli za kisiasa za akina Polepole.
 
Imagine kwenye hzo hotel chips na nyama elfu Saba, ni Raia gani ana afford hyo hela, na hawana option ya kula chips kavu wakati kitaa chips ni bei nafuu. Hii ya kupita stendi itasaidia wasio na fedha kutokutumia gharama kubwa
... uko sahihi na wadau wamelisemea kwenye post za juu. Tatizo isiwe kulazimisha kila mtu kula kwenye hizo hoteli za stendi (kwa stend ninazozifahamu). Badala yake kuwe na mechanism ya kuwawezesha abiria kuchagua.

Kwa mfano, uwepo utaratibu rasmi ambapo abiria kabla ya kukata tiketi anapewa taarifa ya mahali basi litakaposimama kwa ajili ya chakula na ikwezekana apewe MENU za hiyo hoteli well in advance ili awe na uchaguzi wa kukata au kutokata tiketi ya hilo basi! As simple as that!
 
Pole pole ahakikishe hilo swala linafanyiwa kazi, vyakula vibaya hafu very expensive, nyama ngumu ka jiwe
... baada ya kuondelewa kwenye iliyokuwa TFDA sasa suala la ubora wa vyakula ni la TBS; mojawapo ni kuhakikisha nyama inakuwa laini ili cariha aweze kutafuna bila shida. Ha ha ha!
 
... uko sahihi na wadau wamelisemea kwenye post za juu. Tatizo isiwe kulazimisha kila mtu kula kwenye hizo hoteli za stendi (kwa stend ninazozifahamu). Badala yake kuwe na mechanism ya kuwawezesha abiria kuchagua.

Kwa mfano, uwepo utaratibu rasmi ambapo abiria kabla ya kukata tiketi anapewa taarifa ya mahali basi litakaposimama kwa ajili ya chakula na ikwezekana apewe MENU za hiyo hoteli well in advance ili awe na uchaguzi wa kukata au kutokata tiketi ya hilo basi! As simple as that!
Mkuu hzo option ni kuchoshana tu hapo wamiliki wangetakiwa waweke Bei nafuu ya mtu ku afford, halafu chakula sio anasa ni basic needs, mtu anaweza kutaka Basi flani KWA uzuri ila Budget yake ikawa ndogo ya kula maana wengi hushinda na njaa. Hata hzo sehemu za kulia msosi vyakula huwa vibovu nyama mbovu chips zimekaa mda za baridi, halafu Bei juu. So ikipatikama sehemu za options ka stendi I'm sure 99% ya abiria wataenda kula chips za buku jero na mishikaki, kuliko kula chips mbaya zilizokaa mda mrefu halafu ghali.
 
... baada ya kuondelewa kwenye iliyokuwa TFDA sasa suala la ubora wa vyakula ni la TBS; mojawapo ni kuhakikisha nyama inakuwa laini ili cariha aweze kutafuna bila shida. Ha ha ha!
[emoji23][emoji23][emoji23] Hawa wa mabasi Mimi hunichefua kweli Yani na ma vyakula Yao bana michips mibovu, Hadi hukumbuka chips za mtaani tamu hafu Bei rahisi. Mimi nampongeza Pole pole kwa hili swala la kupelekewa mahoteli Yao na kutulazimisha na hivi wanajua abiria hatuna options Basi ni kututesa tu.
 
Mkuu hzo option ni kuchoshana tu hapo wamiliki wangetakiwa waweke Bei nafuu ya mtu ku afford, halafu chakula sio anasa ni basic needs, mtu anaweza kutaka Basi flani KWA uzuri ila Budget yake ikawa ndogo ya kula maana wengi hushinda na njaa. Hata hzo sehemu za kulia msosi vyakula huwa vibovu nyama mbovu chips zimekaa mda za baridi, halafu Bei juu. So ikipatikama sehemu za options ka stendi I'm sure 99% ya abiria wataenda kula chips za buku jero na mishikaki, kuliko kula chips mbaya zilizokaa mda mrefu halafu ghali.
... madam; hivi unajua stendi za nchi hii? Really? Kwamba migahawa ya stendi utapata huduma bora (vyakula na vyoo) kuliko private facilities? Please, rethink.
 
... madam; hivi unajua stendi za nchi hii? Really? Kwamba migahawa ya stendi utapata huduma bora (vyakula na vyoo) kuliko private facilities? Please, rethink.
Kila stendi zina vyoo na vitu vingi tu vinavopatikana KWA urahisi kuliko hzo gharama. Hafu watanzania wengi maisha ni ya chini wewe ka uko vizuri mshukuru Mungu, watu wanapiga msosi wa buku, sasa kwenda kumwambia mtu atoe elfu kumi kasoro kisa chips ambazo sehemu nyingine buku jero. So usidharau stendi zetu ambazo zinatumiwa na watu daily, ka stendi ya makumbusho ni ya daladala na Ina kila kitu sembuse stendi za mkoa, na mabasi yakianza kusimama kituoni automatic biashara za msosi zitataradadi, na kuinua hata uchumi wa wajasiriamali wadogo kuliko kwenda huko porini na kunyonya watu maskini, ikiwa stendi Raia wengine watafaidika
 
Dah! Ila binadamu bwana tuna mambo!

Malalamiko si yamekuwa yakitolewa humu humu 'repeatedly' kwamba hoteli ambazo mabasi husimama chakula ni ghali sana, hakuna value for money na hakuna options? Kwa hiyo mabasi yatakiwe kuimama sehemu zinazowafaa wananchi wote.

Sasa malalamiko yamefanyiwa kazi, kabla hata utekelezaji haujaanza, waja tunalalamika tena? Eti kwa nini mapendekezo ya walalamikaji yamefanyiwa kazi. Duh!

Kwa hili polepole yuko sahihi sana na amekuwa very efficient. Kama kuna wa kulaumiwa kwenye hilo, basi ni waliolalamika ambao sasa wamepewa wanachotaka kisha wanalalamika tena.

Ni vyema tukawa tunajiridhisha kuwa tunataka nini au hatutaki nini kabla ya kuomba, vinginevyo kama kila ambacho mtu hupewa (hata kama kaomba) analalamika, mwishowe mfanya maamuzi huchanganyikiwa na kuamua chochote ili iwe vyovyote na chanzo cha tatizo la namna hiyo ni 'consumers'.

Mwisho wa siku kulalamika wakati mwingine nayo ni tabia, kuna mtu vyovyote itakavyokuwa tu, atalalamika na kulaumu, yaani ni sehemu ya maisha yake.
Hata Mimi nimeshangaa hii kitu watu wamelalamika Leo inakuja wanataka yaleyale
 
Sasa stend zetu nyingi kwa uzoefu wangu hazina hoteli Zina vibanda vya mama lishe ambao wengine wanapika wanapojua na kufanya kuleta vyakula stend kwa kutumia vikontena vidogo vya plastiki ambapo atakuwa na mdada mdogo wa kusambaza chakula hukona huko hapo stend
Hoteli za stand zina weza hudumia magari mangapi at ago? Ina hitajika miundombinu mipya kabisa sio siasa
 
Pamoja na hayo lakini hii ni hatua nzuri kabisa. Wengi tumekuwa tunalalamika hapa mabasi yanatupeleka hoteli ambazo bei zao wanapanga bila kujali kwani wanajua hakuna ushindani na abiria hana sehemu nyingine ya kula. Wakihamia stendi watajitokeza watu wengi wataokajenga au kuimarisha hoteli za stendi kama zamani.
Ni kweli mkuu hata Dada na mama zetu watajipatia ajira. Kule unakuta wana maslahi nako.
Sawa vyoo huwa ni visafi na huko stendi watu watachukua tenda za vyoo so usafi utakuwa Wa kuzingati sana kwa hali ya juu sana.
Wasitutishe sana.
Kinachoniboaga kilo ya mchele tena grade A ya kyela ni buku afu huko wanauza eti buku tano yaani na kodi sio kuwa ni kubwa kama huku dar ama sijui wapo ama eneo hakuna ghaarama kulipata.
Wangefanya bei za kawaida isingewatokea puani.
 
Sasa stend zetu nyingi kwa uzoefu wangu hazina hoteli Zina vibanda vya mama lishe ambao wengine wanapika wanapojua na kufanya kuleta vyakula stend kwa kutumia vikontena vidogo vya plastiki ambapo atakuwa na mdada mdogo wa kusambaza chakula hukona huko hapo stend
Kwanj unapokulaga kule unajuaga jikoni kukoje mkuu.
Ishu hawa jamaa wangefanya bei reasonable.
Mie huwa nawajibu mbona mnafanya bei kama vile mko mgodini ama Sie ni watalii.
 
Back
Top Bottom