Ndugu upande wa baba.. Una lipi la kuwaambia?

Ndugu upande wa baba.. Una lipi la kuwaambia?

Mwanamke ukimpenda kisawasawa, ukahakikisha yupo salama, na kuhakikisha hisia zake hazitoki kwako na kumfanya ajione salama mda wote katika uwepo wako, hayo mawazo ideas yote dhidi yao hutayaona.. Tatizo moja tu nafasi za wababa wanakaa wao na nafasi zao wanakaa wababa.. bangiii tupuu..

Tuna mitazamo mibaya dhidi yao, kwasababu ya nafasi zao kukaa sie na wao kukaa nafasi zetu

Neno moja kwao, nawapenda ni malango ya baraka kwenye maisha yetu
 
Ni kweli hawaeleweki?
Ni kweli wao wanadhani wana haki zote?
Ni kweli wao wanajiona daraja la kwanza?
Ni kweli hawaambiliki?
Sio familia zote,kwetu marehemu baba yetu alioa mke wa kwanza na akapata watoto 5 mkewe alipokufa akamuoa mama yetu tukazaliwa 10 lakini hao watoto wa baba walitupokea na kutusimamia sisi vizuri mno
 
Ni kweli hawaeleweki?
Ni kweli wao wanadhani wana haki zote?
Ni kweli wao wanajiona daraja la kwanza?
Ni kweli hawaambiliki?
Ndugu upande wa baba kwa jamii za patrilineal wanatambulika kama wazazi baada ya baba yako, ni walezi namba moja sambamba na baba yako, ndiyo walezi wako baada ya baba yako kufa au kushindwa kukulea ndiyo maana wanaonekana wakali kwa sababu wanalinda heshima ya ukoo, wanataka kukujengea msingi wao ukoo wao.

Ndungu upande wa mama ni wageni ndiyo wanaact too nice kwako kwa sababu siyo sehemu ya familia yao na hata ukipata tatizo wao siyo wa kwanza kulitatua wao ndugu yao ni dada yao tu. Hata baba yako akizinguana na dada yao wao watamfuata dada yao hawatakuwa na habari na watoto wake.
 
Huwa siangaliagi upande

Kuna ambao wapo upande wa baba ni wema na wapo Tayari kusaidiana na pia wapo wa upande wa mama pia

Kwahiyo ni kuchagua tu walio sahihi pande zote
 
Ndugu wa upande wa baba ni wale watu wanaohusiana nawe kupitia damu ya baba yako.

Katika utamaduni na jamii nyingi, hawa ndio wanaounda msingi wa ukoo au jina la familia.
Hawa hapa ni ndugu muhimu wa upande wa baba:

.Baba Mkubwa: Kaka wa baba yako

.Baba Mdogo: Mdogo wa kiume wa baba yako

.Shangazi: Dada wa baba yako (mkubwa au mdogo)

.Babu na Bibi: Wazazi wa baba yako

.Binamu: Watoto wa baba mkubwa, baba mdogo, au shangazi.
 
Huwa siangaliagi upande

Kuna ambao wapo upande wa baba ni wema na wapo Tayari kusaidiana na pia wapo wa upande wa mama pia

Kwahiyo ni kuchagua tu walio sahihi pande zote
Aisee kuna familia zina mvurugano mkubwa sana kwenye hili.. Ukiona ndugu wa pande mbili wote mnaenda sawa.. Mshukuru sana Mungu
 
Mwanamke ukimpenda kisawasawa, ukahakikisha yupo salama, na kuhakikisha hisia zake hazitoki kwako na kumfanya ajione salama mda wote katika uwepo wako, hayo mawazo ideas yote dhidi yao hutayaona.. Tatizo moja tu nafasi za wababa wanakaa wao na nafasi zao wanakaa wababa.. bangiii tupuu..

Tuna mitazamo mibaya dhidi yao, kwasababu ya nafasi zao kukaa sie na wao kukaa nafasi zetu

Neno moja kwao, nawapenda ni malango ya baraka kwenye maisha yetu
Shida maranyingi huanzia upande wowote pale mmoja anapomtendea mwenzake ndivyo sivyo..
Mtendwa anaweza kuvumilia na kuficha aibu ama matendo mabovu ya mwenzake lakini kamwe hataweza kuficha matokeo!
Ama mmoja anaposhindwa kabisa na kuamua kuitisha vikao vya kifamilia ... Moto huanzia hapo, maana hekima isipotawala hilo jambo litagusa mpaka wana ukoo
 
Vipi wale waliosaidiwa na ndugu kutoka upande wa mama baada ya kutelekezwa na ndugu kutoka upande wa baba, unawazungumziaje?
Ukikaa ukaelewa kwamba na wewe utafika wakati wako wa kutengeneza kitu kinachoitwa upande wa baba, utaelewa hajuna muda wa ku judge watu kwa mambo yaliyopita ambayo huenda hata msingi wake hauuelewi vizuri.
 
Hao watu nikipengele kingine. Baba alivofariki walinikalia kikao kwamba sasa naitaji kuoa. Niliwauliza maswali ambayo hadi leo hii waliamua kuniweka makamu mwenyekiti wa familia. Usije kumuogopa mtu maishani so long as unasema ukweli. Mimi niliwaambia ndio nimekubali na mke ntamtunza ila nawaomba mchango wa mahari hata robo ya mahari wanisaidie kila mtu akafyata mkia wakaenda kupambana na hali zao. Mara eti mahari "tutauza" ule uwanja wa kule upate mahari. Hapo ndo kabisa waliingia cha kike kwa hiyo kauli ya 'tutauza' niliwapa vidonge vyao hadi wengne miaka imepita zaid ya kumi hatusalimiani.
 
Hapo ndo kabisa waliingia cha kike kwa hiyo kauli ya 'tutauza' niliwapa vidonge vyao hadi wengne miaka imepita zaid ya kumi hatusalimiani.😂
 
Back
Top Bottom