Nmetoka kuwaaga shemej zangu wawili na Mtoto mmoja wote wamerud mkoani asbuh ya kuamkia Jana.
Nilitaarifiwa na wife pamoja na ma mkwe kua Kuna shemeji yangu watakuja k'koo kufunga mzigo so watafikia kwangu, nikasema OKEY
Siku ya siku,
Nashangaa nampokea shemej yangu akiwa na mwanae (1yr) pamoja na mdg wake wa kike (20yrs), wakiwa binamu Yao WA kiume (17yr).
Wamekaa home almost wiki,sioni dalili yyt ya kwenda kufunga mzg k'koo Wala nini, nikaambiwa shemej anasubir atumiwe Ela na mumewe.
Nikahoji hao wengn vipi, nikaambiwa uyo WA kike kamsindkza dada ake kufunga mzgo, na uyo WA kiume kaja kuangalia vyuo vya kusoma mana matokeo yake ya form4 hayakua mazuri. Nikapiga Kimya.
Wamekaa almost mwezi na wiki 1, wife kaja kumuombea dada ake nauli anaomba arud mkoani, nikahoji mtu kaja kibiashara afu naul nimlipie Mimi
iyo vipi, akasema wamegombana na mmewe kaghairi kumpa nauli. Nikaona sio kesi, nikampa nauli akakate ticket aende.
Yule mdg wake nae kanifata anaomba nauli aende na dada ake. Nikamwambia mbona ghafla Sana, sikua na bajet iyo, Endelea kukaa nikipata nauli utarud mkoani. Kasema sawa.
Kesho yake Nashangaa shemej na mdg wake wote wamefungasha, nikaulza vp wee mdg SI unabaki, akasema "mama kantumia nauli,so na Mimi narud mkoani". Nikamtakia KILA la heri.
Yule binamu wa kiume, nafikiria wiki ijayo nimpe TU nauli nae arud mkoani maana sioni Cha maana kilichomleta mjini,maana ata vyuo alivyosema kaja kuangalia hajishughulishi navyo zaidi ya ubishi WA Simba na yanga.
Yote Kwa yote,
Wageni Ni baraka, Home Palichangamka Sana, Ila Wageni waje Kwa utaratibu na Kwa Sababu maalum.