Ndugu wengi wenye uwezo mkubwa kipesa hawatakagi mazoea na ndugu wenye uwezo mdogo kiuchumi

Ndugu wengi wenye uwezo mkubwa kipesa hawatakagi mazoea na ndugu wenye uwezo mdogo kiuchumi

Mtu mwenye kipato kikubwa anatumia muda mwingi kukitafuta, hana muda wa kupoteza kupiga zogo za sungura na fisi...huku akijua 'time is money' muda mwingi yuko bize
 
Hamjamuelewa mtoa mada
Ishu ni kwamba mwenye pesa hata akiona nduguye hohehahe kampigia atataka kujua nani kampa namba...ikitokea kuna kashuhuri wanajifanyaga wanasahau kualika wale wenye hali ya chini kumbe ni kadharau wanajua hata ukija utachangia nn?? Hata kama ni zawadi kama anapelekewa ndugu maskini basi itakua ni cheap sana mtu anasema aah yule hizi zitamfaa.

Kuna ndugu yangu nilimsikia mwenyewe etii alikataa maids wasivae suti akasema wee unavowaona wale wana sehemu ya kuhifandi suti!! Wakishavaa kwenye sherehe watavaa wapi tena!!!! Jamani ni dharau sanaaaaa tena mbayaaa.
 
Kuna levo ya maisha ukiwa nayo tabia inabadilika hadi aina ya marafiki nao wanabadilika
 
Kazi ipo mi niko tofauti naweza kusema kuna kaka zangu Wana Ela Sana,Ila mi nakomaa kivyangu na simuombi mtu najua kila mtu ana sahani yake hapa duniani ,na huwa nasimamia kile ninachokiamini
Wewe mimi kabisa......
 
Ni roho za kichoyo na ushamba

Eti kwasababu upo busy ndio hutaki wageni! Kwani nyumbani kwako ni ofisini?

Saidia ndugu acha visingizio tena kwa hii bongo watu wengi wamefika hapo walipo kwa kusaidiwa...
 
Kazi ipo mi niko tofauti naweza kusema kuna kaka zangu Wana Ela Sana,Ila mi nakomaa kivyangu na simuombi mtu najua kila mtu ana sahani yake hapa duniani ,na huwa nasimamia kile ninachokiamini
Maskini jeuri.
Umaskini mbaya sana
 
Kuna kitu kinanikera sana wabongo wengi waliojaliwa vipato wanapenda sana kuabudiwa na kutukuzwa huu ni uzwazwa wa chuo kikuu
 
Nimekua niki-observe hili swala kwa mda mrefu kidogo na kwenye familia nyingi tofauti, utakuta ndugu wenye uwezo mkubwa kipesa wanawatenga ndugu wenzao wasio na pesa kinamna flani, sio kwamba wanawatenga kabisa..hapana..misiba na sherehe za harusi watahudhuria, michango watachangia, ila mazoea na ndugu wengine wenye kipato cha chini hawataki kabisa..mazoea kama ya kupiga story zisizo na kichwa wala miguu kwa lisaa lizima, friendly gossip, kutaniana na kucheka pamoja, kutembeleana cku ambazo si za sikukuu (yani cku za kawaida), kujuliana hali etc

Wakati ndugu wengi wasio na uwezo mkubwa kiuchumi wako more friendly, mtapiga story lisaa lizima, mtacheka na kutaniana, mtatembeleana akija kwako utamkaribisha fresh, atakula msosi na kushiba, ukienda kwake atakukaribisha vizuri. utakula ushibe, tena ndugu asie na uwezo atakuomba ww uende kwake umtembelee...mm kwa mtazamo wangu huu ndo undugu halisi.

Especially ndugu wengi wenye uwezo mkubwa wa kipesa wanaoishi dar ndo wana tabia hizo, ndugu mwenye uwezo mkubwa kipesa hata akikuruhusu umtembelee na akikukaribisha msosi wake unaona hii karibu haitoki rohoni, hii nimei-observe kwenye familia nyingi.

Hakuna ndugu wapumbavu kama wale wenye uwezo wa kifedha wanaowatenga ndugu zao wenye kipato cha chini alafu siku wakipatwa na matatizo wanakimbilia kwa ndugu zao wenye kipato cha chini.

Nakumbuka miaka ya nyuma baba yangu mkubwa kipindi Ana pesa familia yake ilijitenga na sisi kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha, uchumi walijitenga sana na sisi hata kutembeleana ilikuwa shida pia walikuwa wanatuona sisi kama wachawi

Ila tangu mzee magu aingie madarakani ile bomoa bomoa na walivyobomolewa nyumba yao wakawa hawana pakwenda ndo Mara ya kwanza walikimbilia nyumbani kwetu
 
Back
Top Bottom