Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Natumai wote hamjambo humu.

Nina ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, hapo awali alikuwa ni mtu smart na mpambanaji wa maisha, sijui kitu gani kimemkuta, anakunywa pombe muda wote hata kazi ameacha kwa sababu ya pombe.

Watu wengi wamenishauri nimpeleke sober house {Kwa kiswahili sijui inaitwaje}

Najipanga nimpeleke japo ni gharama lakini nitajitahidi kwa sababu hali yake inanihuzunisha sana, wahusika wameniambia anaweza kukaa huko wa muda wa miezi mitatu hadi minne, na atakuwa sawa kabisa.

Wenye uzoefu na sober house, unaweza kuwa ulimpeleka ndugu yako au kama una uelewa wowote je zinasaidia kubadilisha maisha ya waraibu wa mihadarati na kurudi kwenye hali zao za kawaida?

Nb.Maoni yenu ni muhimu,

Natanguliza shukrani za dhati.

Asanteni.🙏🙏
 
Pole sana mkuu.

Tungepata wasifu wa ndugu yetu kwanza, umri wake, jinsia, ana familia (au ameoa au kuolewa?), elimu, na aina ya pombe.

Kwasababu unaweza kuta kama ameoa, kumbe mke wake ndio anamchanganya hadi anaamua kulewa, kwahiyo ata akitoka sober, anakutana na tatizo lile lile.

Huo ni mfano tu.
 
Sober House inasaidia kama na yeye ameridhia kubadilika, kama umemlazimisha hawezi kubadilika.... wenyewe wanasema ni rahisi kumbadili mtumiaji wa cocaine au heroine lakini sio wa Pombe au Sigara, sababu Pombe sio illegal na inapatikana kila sehemu muda wowote kwa bei nafuu....

Nadhani kabla ya Sober House mpeleke kwanza akaonane na therapist, lazima kuna jambo linamtatiza hadi kudondokea kwenye ulevi, afix kwanza jambo hilo.
 
Pole mkuu, pambana umsadie pombe ya namna hiyo mwishoe ni mauti!
Anyway watakuja hapa watakwambia kuna dawa za kienyeji sijui....

wengine watakushauri umpeleke akaombewe.....

Wengine watakudhihaki......

Pole mkuu usichoke awe ndugu wa kuzaliwa au mzazi kufikia hatua hiyo ya ulevi inauma sana
 
Pole mkuu, pambana umsadie pombe ya namna hiyo mwishoe ni mauti!
Anyway watakuja hapa watakwambia kuna dawa za kienyeji sijui....

wengine watakushauri umpeleke akaombewe.....

Wengine watakudhihaki......

Pole mkuu usichoke awe ndugu wa kuzaliwa au mzazi kufikia hatua hiyo ya ulevi inauma sana
Asante mkuu
 
Sober House inasaidia kama na yeye ameridhia kubadilika, kama umemlazimisha hawezi kubadilika.... wenyewe wanasema ni rahisi kumbadili mtumiaji wa cocaine au heroine lakini sio wa Pombe au Sigara...
Ulichoandika hapo futa heroine, hauwezi kubadili mtu anaetumia heroine akaacha. Only 10% Ndo wanaacha lazima 90% wanarelapse.
 
Natumai wote hamjambo humu.

Nina ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, hapo awali alikuwa ni mtu smart na mpambanaji wa maisha, sijui kitu gani kimemkuta, anakunywa pombe muda wote hata kazi ameacha kwa sababu ya pombe...
Pole ndugu, kwenye familia zetu changamoto ni nyingi ikiwa ni pamoja na uliiyonayo,ukipata ushauri wa kukusaidia usiache kutushirikisha na sisi,huenda hata wengine watakuja PM.
 
Hakuna dawa ya maalumu ya kuacha ulevi wa pombe.
Njia kuu ya kuacha pombe ni kuacha pombe kupitia tafakuri halisi ya hasara na madhara kwa mhusika mwenyewe.

Bahati mbaya ni kuwa mlevi hawezi kulazimishwa kuacha pombe, bali aamue yeye kwa hiari yake.
Kunywa kistaarabu😎
 

Attachments

  • CastleLagerandGlass2016.jpg
    CastleLagerandGlass2016.jpg
    14.8 KB · Views: 1
Pole ndugu, kwenye familia zetu changamoto ni nyingi ikiwa ni pamoja na uliiyonayo,ukipata ushauri wa kukusaidia usiache kutushirikisha na sisi,huenda hata wengine watakuja PM.
Sawa mkuu tuko pamoja
 
Back
Top Bottom