Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Ntamhudumia kwa mahitaji yote kwa sababu hali yake inaniumiza sana
Pia husimdekeze. Exercise Tough Love.

Kama yuko Dar es salaam, mpeleke mbali na ambako hajulikani na hamjui mtu, sense of stigma inaweza trigger akarudia endapo atakua karibu na watu anaowajua na wenye uwezo wa kumpa alcohol.

Njiro Recovery iko Engutoto Arusha.
Life & Hope iko Bagamoyo.
Detroit Recovery iko Zanzibar.
 
Natumai wote hamjambo humu.

Nina ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, hapo awali alikuwa ni mtu smart na mpambanaji wa maisha, sijui kitu gani kimemkuta, anakunywa pombe muda wote hata kazi ameacha kwa sababu ya pombe...
ikiwa karidhia mwenyewe na kwamba yeye binafsi anawiwa kuacha pombe lakini anashindwa, ukimpeleka huko utakua umesadia sana, atapona kabisa na kua mtu mwema na mwenye afya njema furaha tele. Na hakika atakushukuru na kukuombea sana kwa Mungu.

Lakini kama ni wakulazimisha anaweza kwenda huko na kurudi akiwa ama mlemavu ama hana meno.

niliwahi mpeleka ndugu yangu huko sober alirudi taya zimepishana, meno yamepasuka, halafu anakithembe.
Mfano ukimwambia sema Simba yeye ansema Thimbwaa,
neno sasa anasema thatha....
na wakati alikuaga yuko vizuri tu.

yaani ndio tukapata tabu zaidi kwenye hali hiyo lakini bado ndio akawa anatoroka kwenda kwenye pombe na akifika apo kwenye kibanda cha pombe akinunua kile kikopo cha elfu2 anakibugia na kukikata kap maramoja chote ili tusimkute anakunywa.

so, kwa hiari yake mpeleke tafadhali tena mapema iwezekanavyo.

mara zote tumemkuta yuko chakari....
 
Pia husimdekeze. Exercise Tough Love.

Kama yuko Dar es salaam, mpeleke mbali na ambako hajulikani na hamjui mtu, sense of stigma inaweza trigger akarudia endapo atakua karibu na watu anaowajua na wenye uwezo wa kumpa alcohol.
....
Ni Arusha mkuu
 
ikiwa karidhia mwenyewe na kwamba yeye binafsi anawiwa kuacha pombe lakini anashindwa, ukimpeleka huko utakua umesadia sana, atapona kabisa na kua mtu mwema na mwenye afya njema furaha tele. Na hakika atakushukuru na kukuombea sana kwa Mungu...

Ilikuaje hadi akawa amepinda taya, meno yamevunjika na kua na kithembe?

Japo nimecheka sana
 
Mdogo wangu anapitia hio kitu


Pole sana.


Miaka mitano ijayo Tanzania itakua na alcoholics wengi kwa maelfu wenye umri mdogo 15-40.

Vijana pombe wameifanya ndio maji ya kunywa, Dawa ya nguvu za kiume, Dawa ya mawazo ya ugumu wa Maisha, Socializing identifier na alama ya ufahari na ujanja.

Ni adui anaewamaliza kwa kasi na kwa hatua huku anawaburudisha na kuwapumbaza.
 
Back
Top Bottom