Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, nataka nimpeleke sober house

Natumai wote hamjambo humu.

Nina ndugu yangu amekuwa mlevi wa kupindukia, hapo awali alikuwa ni mtu smart na mpambanaji wa maisha, sijui kitu gani kimemkuta, anakunywa pombe muda wote hata kazi ameacha kwa sababu ya pombe.

Watu wengi wamenishauri nimpeleke sober house {Kwa kiswahili sijui inaitwaje}

Najipanga nimpeleke japo ni gharama lakini nitajitahidi kwa sababu hali yake inanihuzunisha sana, wahusika wameniambia anaweza kukaa huko wa muda wa miezi mitatu hadi minne, na atakuwa sawa kabisa.

Wenye uzoefu na sober house, unaweza kuwa ulimpeleka ndugu yako au kama una uelewa wowote je zinasaidia kubadilisha maisha ya waraibu wa mihadarati na kurudi kwenye hali zao za kawaida?

Nb.Maoni yenu ni muhimu,

Natanguliza shukrani za dhati.

Asanteni.🙏🙏
Mlete tunywe nae. Tutamfundisha unywaji bora usiwaze kabisa
 
Ameridhia kuiacha hiyo pombe?

Lazima aonyeshe namna gani hiyo pombe inamuumiza kwenye maisha yake ya kila siku na sasa anaamua bila kushurutishwa anaiacha.

Kama hajaridhia mtakuwa mnajisumbua tu.
Kabla ya kumpeleka ntamshirikisha, ye mwenyewe aliwahi kuniambia ataacha kwa hiari yake
 
Ilikuaje hadi akawa amepinda taya, meno yamevunjika na kua na kithembe?

Japo nimecheka sana
walimpiga wenzie alikua ana kaukorofi na kaubishi ka maudhi, alitandikwa vibaya sana karibu afe ila yeye alisema eti amepata ajali.

actually wale jamaa wa pale sober walikua wakitupatia taarifa zake ila yeye anageuza anatia uongo
 
Hii
Tafuta nguruwe ananyonyesha, kamua maziwa walau vijiko 2 vya chai!!! Mnunulie tungi alipendaro, anyweeeee mpaka alegee then mchanganyie yale maziwa kwenye kinywaji komojawapo akikisha anakunywa mpaka inaisha!! Baada ya hapo atatapika mpaka mashetani yooote na haji kugusa pombe tena milele na milele!!


NB: hili swala inabidi iwe siri yako na usije kumwambia mtu, kamwe usimwambie mtu
Hii haina madhara mkuu tusije kujaribu tukaua mtu🤔
 
[emoji445] Mwache Ale vitu , Maisha siyo haya bwana [emoji445][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
ni mlevi wa pombe aina gani na pia ni pombe tuh anatumia au anavuta na bangi na sigara
 
Weka kinyesi kwenye pombe bila yeye kujua lolote,,, shughuri atakayoipata Kila akiona chupa ya pombe au harufu ya pombe atakimbia! Onyo ufanye Siri asijue yeyote zaidi yako! Ukifanikiwa uje utoe mrejesho
 
Weka kinyesi kwenye pombe bila yeye kujua lolote,,, shughuri atakayoipata Kila akiona chupa ya pombe au harufu ya pombe atakimbia! Onyo ufanye Siri asijue yeyote zaidi yako! Ukifanikiwa uje utoe mrejesho
Unamaanisha kinyesi cha binadamu?
 
Back
Top Bottom