Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikwambie kitu jamaa, acha kazi chukua hela halafu njoo nikwambie kitu!!!Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.
Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.
Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Hakikisha anakuingizia hiyo hela kabla hujaacha kazi yako. Akigoma eti mpaka uache kazi achana nayeMara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.
Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.
Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Huyu mtu ni muoga wa biasharamkuu mbona unakosa uaminifu hata kwenye ideas?.uaminifu na ukweli ni kitu muhimu na cha kwanza kwenye kila kitu iwe biashara au ajira....wizi, utapeli, uongo-uongo hautakufikisha mbali..ni jambo la muda mfupi tu lenye hasara kubwa mbeleni.
Vijana wa Tz tujifunze kuwa honest kwa mafanikio sustainable na yenye baraka za Mungu.
Nimekuewlewa mkuu, ila sasa huo sio uamuzi wangu. Msimamo wake ni kwamba acha kazi, fanya biashara nitakupa mtaji. La sivyo endelea na kazi yako.
Wazee wa fursa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nkopeshe laki moja nkupe ushauri HEAVY utakao badiri kurasa za maisha yako[emoji3166][emoji855]..
hii ni Sirius hakuna ushauri mzuri unaopatikana bure na kiwepesi hivi, ndiomaana humu hakuna anaekushaur vyamaana zaidi ya upuuzi na starehe[emoji3166].
Kunjua muhamala huo nkupe ufunguo wa akili[emoji3166].
Halafu yaani umeongea point, maana ananiambia I have to learn to take risks. Anasema nikikataa nikaja kupoteza kazi yangu nisimwombe tena hiyo hela! I have to decide now!
In fact hata alijoke kwamba kwani wewe ulipokuwa unamchumbia shemeji angekutalia kwa kuwa ana mtu halafu aje akufuate baadae kwa kuwa mtu wake amemwacha ungekubali kumchukua?🤣🤣🤣
Nilitaka niandike hili jambo, nikaona nipitie kwanza isijekua tayari kuna mtu ameshaandika.
Kwa mtu asiye na uzoefu wa biashara, hatakiwi kukurupuka, idea nyingi zitakuja na kwa kuwa ana pesa, atapenda aijaribu kila moja, kuja kutahamaki pesa yote imekata.
Anunue bond za muda mrefu kama za 100M kisha 80 M aweke fixed ya mwaka. 20 M aanze kufanyia mradi mdogo.
Hasi mwaka uishe, atakua ameshapata uzoefu na uelekeo wa biashara, ataqeza kuchukua kiasi kwenye ile 80M bila kuathiri makubaliano ya fixed account. Hii itampa uwezo wa kupanua biashara kulingana na mahitaji.
Wakati huo 100M inaendelea kumpa interest kama kawaida.
Ushauri wangu, fanya biashara kati ya hizi
1.Fungua duka la vifaa vya Ujenzi hutajilaumu.
2.Fanya biashara ya vinywaji Soda,bia,na maji, unakuwa Wakala ,unafungua bonge la Depot yako.
3.Fanya biashara ya Mazao,nenda maeneo ya boda, mfano Tunduma jenga Godown lako, linaweza kula km Million 40,zinazobaki unakuwa mtaji wako wa kukusanyia Mazao vijijini,then unakuwa unakuwa unawauzia wafanyabiashara kutoka nchi Jirani.Biashara hii inalipa sana.
4.Nunua mashine kubwa ya kukoboa mpunga,pesa inayobaki nunua mpunga wako na kukoboa,then unauuza,pia unakuwa unawakobolea na watu wengine, aisee bonge la biashara.
5.Jenga Lodge sehemu nzuri,then fanya biashara Wewe mwenyewe, utakuja kunishukuru.
6.Nunua Semi trailer, kwaajili ya kubebea mizigo ya wafanyabiashara ndani ya Mwaka unanua nyingine.
Dunian Kila kitu ni fursa aisee,no free lunchWazee wa fursa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Weka TB za BOT za miaka 20 au 25 unavuna 2.7m kila mwezi hiyo unajibana unawekeza mdogo mdogo. Mambo yakikaa sawa yakisha materialize unauza kwenye secondary market then una re-invest elsewhere
5.Jenga Lodge sehemu nzuri,then fanya biashara Wewe mwenyewe, utakuja kunishukuru.