Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Sikushangai mkuu,unajua Kwenye hv vituo vyetu vya kutafuta elimu ndo sehemu peke ya kujichanganya na kujijenga kuwa mtu wa kuona fursa kila sehemu ya kuwekeza....Ila kuna ndugu zetu wale tunawaita wasongolisti/vipanga hawa bhna wakiwa chuo/shule wao ni kusoma tu 24 hrs hawataki kuangalia upande mwengine ,mwsho wa sku wanamaliza chuo ukiwapa ata ML 500 hakuna watakachofanya ktk uwekezaji zaidi hasta tu.

Na ndo hawa wanaokufa kwa mawazo wakikosa ajira...au wanazeekea Kwenye ajira na kufa na kisukari.

Mleta mada ni sampuli ya hao watu .

Tuwafundishe watoto wetu SoMo la uwekezaji na kujitegemea ktk financial issues....tusiwaaminishe kwenye kusoma na kuajiriwa.
 
Chukua 200m wekeza kwa kununua treasury bonds za miaka 25 za 100m. Unazinunua tofauti kwa interval ya miezi sita.
Kwa Tsh 100m uliyonunua treasury bond ya miaka 25 utakuwa unalipwa faida kila baada ya miezi sita 7.95m. Kwa hiyo kama utanunua za 100m kwa 25yrs mara mbili ukatofautisha miezi sita utakuwa kila baada ya miezi mitatu unagema 7.95m ambapo kwa mwaka mzima unagema jumla ya 31.8m x 25 years.
Kwa maana hiyo 200m kwa miaka 25 inakufanya ugeme zaidi ya 700m...
Hiyo milioni sabini inasalia wekeza kwenye huduma ya miamala kwa njia ya simu.
Unaweza fungua sehemu mbili ukawezekeza 20m kwa kila sehemu kwa kuanzia.
2m sehemu yenye mzunguko mzuri unaweza pata hadi 3m commission. 1.5m unaweza tumia kwa matumizi kama wafanyakazi, mlinzi na pango ukabaki na net profit 1.5m huku mtaji wako uko intact.
Usiajiri watu wasio na elimu ajiri mwenye elimu uwe tayari hata kumlipa laki 5 au 6 ili aheshimu kazi yake.
Hii biashara nimeifanya na endelea nayo. Haina longolongo pale unapoajiri mtu aliyesoma. Kuna msimu hiyo 20m unapata commission hadi 5m hasa msimu wa kulipia ada. Ila hata kuwe mdororo vipi haijawahi kushuka chini 2.5 kwa uzoefu nilionao.
Pia katika hiyo 70m kiasi kinachobakia kama 20m fungua uwakala wa vinywaji. Uwe unauza maji kwa jumla. Hii biashara ina inalipa kidogo kidogo lakini ina uhakika wa faida.
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Nikwambie kitu jamaa, acha kazi chukua hela halafu njoo nikwambie kitu!!!
 
Tupige hesabu kidogo.
200m ÷1.5m = 133. 3
Kwa hiyo katika 200m kuna jumla ya mishahara 133.3

133.3 ÷ 12 = 11.1(years)

Kwa lugha nyingine jamaa anakupa mshahara wa miaka 11.1

Kama unaogopea kupoteza mshahara wako wa 1.5m basi fanya hivi.

Chukua mshahara wa miaka 5 katika ile miaka 11.1 weka bank kwa makubaliano ya kupewa kila mwezi 1.5m.

Kisha nusu ingine ya mshahara wa 11.1 ingiza kwenye biashara, kwa hiyo hapa una uhakika wa mshahara wa miaka 5 na fungu la biashara kwa hivo ndani ya miaka 5 una uhakika wa mshahara na biashara ikifanya vema itakua bonus +++++ ikidoda bado una backup ya ile ya bank unayopewa kwa makubaliano.
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Hakikisha anakuingizia hiyo hela kabla hujaacha kazi yako. Akigoma eti mpaka uache kazi achana naye
 
mkuu mbona unakosa uaminifu hata kwenye ideas?.uaminifu na ukweli ni kitu muhimu na cha kwanza kwenye kila kitu iwe biashara au ajira....wizi, utapeli, uongo-uongo hautakufikisha mbali..ni jambo la muda mfupi tu lenye hasara kubwa mbeleni.

Vijana wa Tz tujifunze kuwa honest kwa mafanikio sustainable na yenye baraka za Mungu.
Huyu mtu ni muoga wa biashara
Like many employees
Msimuingize mkenge
 
Faza kama utanisikiliza nielewe, hiyo m 200 chukua na nenda Iringa ukalete lori 2 za mbao pia uhakikishe umefungua duka la vifaa vya ujenzi. Unaweza kuona kama ni kusadikika ila hapo pesa ipo haswaa! Unaweza ukaitenga m100 kuhakikisha kila kitu kimekaa sawa na ukaja ukaona umechelewa sana kwenye kuajiriwa.

Watu wengi sana walichezea pesa kipindi cha JK, hawakujenga sasa kaingia mama pesa kwa upande fulani inaonekana, watu wanajenga hasaa.
 
Weka bank,nakuhaid utakula pesa umelala

Kwenye mil 10-20 hukos laki 3 kila mwez

Kwahyo hyo 200 mil hukos mil 3 kila mwez
 
Nkopeshe laki moja nkupe ushauri HEAVY utakao badiri kurasa za maisha yako[emoji3166][emoji855]..
hii ni Sirius hakuna ushauri mzuri unaopatikana bure na kiwepesi hivi, ndiomaana humu hakuna anaekushaur vyamaana zaidi ya upuuzi na starehe[emoji3166].

Kunjua muhamala huo nkupe ufunguo wa akili[emoji3166].
 
Wazee wa fursa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tafuta wasomi wakuandikie mchanganuo wa biashara ya USD200,000. Halafu mwombe a-double mtaji. Mwambie wasomi wanasema ili biashara hiyo iwe viable, inahitajika USD200,000. Nadhani mtaji wako ukiwa mkubwa, unakuwa salama zaidi hata ukiacha kazi.
Halafu yaani umeongea point, maana ananiambia I have to learn to take risks. Anasema nikikataa nikaja kupoteza kazi yangu nisimwombe tena hiyo hela! I have to decide now!

In fact hata alijoke kwamba kwani wewe ulipokuwa unamchumbia shemeji angekutalia kwa kuwa ana mtu halafu aje akufuate baadae kwa kuwa mtu wake amemwacha ungekubali kumchukua?🤣🤣🤣
 
Safi. Nadhani ningekuwa yeye ningekuuliza hiyo biashara ni biashara gani. Nadhani hili pia ndilo swali lake lake la msingi.
Nilitaka niandike hili jambo, nikaona nipitie kwanza isijekua tayari kuna mtu ameshaandika.

Kwa mtu asiye na uzoefu wa biashara, hatakiwi kukurupuka, idea nyingi zitakuja na kwa kuwa ana pesa, atapenda aijaribu kila moja, kuja kutahamaki pesa yote imekata.

Anunue bond za muda mrefu kama za 100M kisha 80 M aweke fixed ya mwaka. 20 M aanze kufanyia mradi mdogo.

Hasi mwaka uishe, atakua ameshapata uzoefu na uelekeo wa biashara, ataqeza kuchukua kiasi kwenye ile 80M bila kuathiri makubaliano ya fixed account. Hii itampa uwezo wa kupanua biashara kulingana na mahitaji.

Wakati huo 100M inaendelea kumpa interest kama kawaida.
 
Mawazo kama haya bila shaka ndio muuliza swali anahitaji.
Ushauri wangu, fanya biashara kati ya hizi
1.Fungua duka la vifaa vya Ujenzi hutajilaumu.
2.Fanya biashara ya vinywaji Soda,bia,na maji, unakuwa Wakala ,unafungua bonge la Depot yako.
3.Fanya biashara ya Mazao,nenda maeneo ya boda, mfano Tunduma jenga Godown lako, linaweza kula km Million 40,zinazobaki unakuwa mtaji wako wa kukusanyia Mazao vijijini,then unakuwa unakuwa unawauzia wafanyabiashara kutoka nchi Jirani.Biashara hii inalipa sana.
4.Nunua mashine kubwa ya kukoboa mpunga,pesa inayobaki nunua mpunga wako na kukoboa,then unauuza,pia unakuwa unawakobolea na watu wengine, aisee bonge la biashara.
5.Jenga Lodge sehemu nzuri,then fanya biashara Wewe mwenyewe, utakuja kunishukuru.
6.Nunua Semi trailer, kwaajili ya kubebea mizigo ya wafanyabiashara ndani ya Mwaka unanua nyingine.
 
Nadhani ni 2.5 mil/month (yaani 15% interest rate).
Weka TB za BOT za miaka 20 au 25 unavuna 2.7m kila mwezi hiyo unajibana unawekeza mdogo mdogo. Mambo yakikaa sawa yakisha materialize unauza kwenye secondary market then una re-invest elsewhere
 
Back
Top Bottom