Ndugu yangu anafanya na kuongea mambo ambayo hayaeleweki

Chance ndoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
4,363
Reaction score
10,265
Habari za wakati huu wana JF wenzangu. Washiriki wenzangu wa kila hali.

Leo na mimi nimepata tatizo, tena kwa ndugu yangu, tena ninayekaa nae nyumbani kwangu. Tatizo analolipitia ni anasikia SAUTI za watu zikimuita akiwa ndani, anasikia magari yanakuja nyumbani, anataja polisi wanakuja, mara watu. Asubuhi ya leo alisema kuna muda kamuona mtu ambae sisi hatumuoni, hadi muda huu ni mtu wa hivyo.

Ila ni kijana smart mwenye kazi yake. Ameshindwa hata kufika ofisini. Inshort ni mtu wa mawazo hadi muda huu.

Sasa embu mnipe msaada wa mawazo kwenye hili. Maana mimi kwangu naona kama naliweza ila naona hali inayoendelea ni ile ile. Nimekaa nae toka asubuhi.

Nafanya ajione yupo kwenye dunia ya kawaida asione amechanganyikiwa ila kiuhalisia jamaa yangu huyu amechanganyikiwa.

Muda huu sauti ya TV ipo juu ili asisikie hizo sauti. Naona inafanya kazi mbinu hiyo maana mpaka analala.
 
Daaaaaaah, nikiiona hii stori namkumbuka mwanangu Ngomuo,Rest Easy baba Kevin

Nae alikuwa akija ofisini anatuambiwa vitu hivhv anavyovisema huyo ndugu wa mleta mada,baadae akajirusha barabarani,Hiace ikajitahidi kumkwepa,ila tairi la nyuma likampitia mshkaji wangu akakata roho hapo hapo,ndoa zingine ni ndoano sana aisee
 
huwenda kuna jambo baya kafanyiwa, hilo jambo limemuaathiri psychologically na emotionally

huwenda kuna jambo baya kalifanya, hilo jambo limemuathiri psycholgically na emotionally

kama anaweza kuongea na mkafanya dialogue vizuri, basi kaanae chini muulize taratibu ajieleze nini kimemkumba

kama anaropoka ropoka tu maneno, basi kazi inakuwa ya ziada kwako kuunga maneno yake na matukio yake ya awali kujua nini kimemkumba

kama ikishindikana kufanya nae mawasiliano kwa kuongea, na kama mkishindwa kabisa kuunga maneno yake na matukio aliofanya kabla ya kupata tatizo, jaribuni kumtuliza mind yake na mawazo yako. yani jitahidini asiwe active muda mwingi. jitahidi muda mwingi awe amelala tu hii itamsaidia kutuliza hivyo anavyoviwaza mapka kumfanya aongee pekeake

kama itashindikana kulala kwa kawaida atumie dawa za kuleta usingizi, lakini dawa hizi kwa kawaida zinatolewa ukiwa na cheti kutoka kwa doctor, so kama ya hapo juu yote yakishindikana mpeke hospital
 
Unachokiongea kinaendana kabisa na kinachoendelea kutokea. Kweli nimetoka pharmacy ni mpaka nipate cheti.
 
huwenda kuna jambo baya kafanyiwa, hilo jambo limemuaathiri psychologically na emotionally

huwenda kuna jambo baya kalifanya, hilo jambo limemuathiri psycholgically na emotionally

kama anaweza kuongea na mkafanya dialogue vizuri, basi kaanae chini muulize taratibu ajieleze nini kimemkumba

kama anaropoka ropoka tu maneno, basi kazi inakuwa ya ziada kwako kuunga maneno yake na matukio yake ya awali kujua nini kimemkumba

kama ikishindikana kufanya nae mawasiliano kwa kuongea, na kama mkishindwa kabisa kuunga maneno yake na matukio aliofanya kabla ya kupata tatizo, jaribuni kumtuliza mind yake na mawazo yako. yani jitahidini asiwe active muda mwingi. jitahidi muda mwingi awe amelala tu hii itamsaidia kutuliza hivyo anavyoviwaza mapka kumfanya aongee pekeake

kama itashindikana kulala kwa kawaida atumie dawa za kuleta usingizi, lakini dawa hizi kwa kawaida zinatolewa ukiwa na cheti kutoka kwa doctor, so kama ya hapo juu yote yakishindikana mpeke hospital
Haya Mambo ya kuchanganyikiwa huwa yanaanza kidogo kidogo Kama hivi.

Leo wakati naingia officen nikawa nasikia mtu anaongea ndani kwa sauti, nikasema ngoja nisikilize umbea Kama kutakuwa na issue ya kusagiana kunguni hapo job, aisee kumbe jamaa yangu wa Karibu kavulugwa na ameamua kuongea mwenyewe mavitu ambayo hata hayaeleweki.

Ile nafungua mlango tu akazuga eti alikuwa anakemea mapepo😅😅
 
Jambo la kwanza msaidie akacheck afya ya akili, then afya nyingine kwa kupimwa magonjwa yaletayo hali ya kuchanganyikiwa...

Kuna watu pia huwa na hali kama hiyo pale roho zao zinapokaribiankutengana na nafsi/mwili, huwa na hali ya kuona watu wa kale n.k...
 
Iliwahi kunitokea kipindi cha nyuma kwakuwa walidhani ni matumizi ya pombe nilipelekwa sober house ilhali mambo yaliendelea vilevile mpaka nilipomaliza miezi minne ndipo nilipoanza kupata nafuu
 
Kipapai wazee wa kigoma au handeni hao kama kadhulumu ,kaiba mke wa mtu mwambie akuuleze vizuri

Yalishamkuta mwana kumbe alimdhulumu mpemba kwenye dili za samaki mpaka aksema ukweli jamaa alikuwa yeye anapiga kelele anasema kuna watu wanamfuata wamkamate hata kama tumekaa wengi unashangaa ana amka na kukimbia kwa kelele

Aliitwa aseme maana watu walizunguka hospitali siku moja akasema kuna mpemba alimdhulumu samaki walivua pamoja yule mpemba akamwambia ntakushtakia kwa mungu kwa vile anajulikana alitafutwa akapewa chake akafanya manuza wiki jamaa kakaa sawa
 
inaitwa hallucination ni kasoro katika sense organ mfano ngozi, macho nk. kuna vyanzo vingi vinvyosabibisha hali hiyo ikiwemo ugonjwa mfano malaria
Inshort ni hali ya kawaida nenda hospital wakajue chanzo, wakitibu chanzo na hiyo hali itaisha

onyo: usiende kwa washirikina utagombanishwa na watu na kuliwa pesa wakati huo unachelewesha huduma sahihi kwa victim
 
Habari za wakati huu wana JF wenzangu. Washiriki wenzangu wa kila hali.
Leo na mimi nimepata tatizo, tena kwa ndugu yangu, tena ninayekaa nae nyumbani kwangu.
Tatizo analolipitia ni anasikia SAUTI za watu zikimuita akiwa ndani, anasikia magari yanakuja nyumbani, anataja polisi wanakuja, mara watu. Asubuhi ya leo alisema kuna muda kamuona mtu ambae sisi hatumuoni, hadi muda huu ni mtu wa hivyo.

Ila ni kijana smart mwenye kazi yake. Ameshindwa hata kufika ofisini. Inshort ni mtu wa mawazo hadi muda huu.
Sasa embu mnipe msaada wa mawazo kwenye hili. Maana mimi kwangu naona kama naliweza ila naona hali inayoendelea ni ile ile. Nimekaa nae toka asubuhi. Nafanya ajione yupo kwenye dunia ya kawaida asione amechanganyikiwa ila kiuhalisia jamaa yangu huyu amechanganyikiwa.

Muda huu sauti ya TV ipo juu ili asisikie hizo sauti. Naona inafanya kazi mbinu hiyo maana mpaka analala.
Mpeleke hospitali akaonana na Mtaalamu Wa Afya ya Akili. Hizo ni visual & Audio hallucinations (kuona vitu/watu ambao wengine hawavioni an kusikia sauti ambazo wengine hawazisikii). Ni dalili ya ugonjwa wa kuchanganyikiwa (schizophrenia). Muwaishe hospitali mapema!
 
Iliwahi kunitokea kipindi cha nyuma kwakuwa walidhani ni matumizi ya pombe nilipelekwa sober house ilhali mambo yaliendelea vilevile mpaka nilipomaliza miezi minne ndipo nilipoanza kupata nafuu
Nini kilikua kisa chako.
 
Back
Top Bottom