Ndugu yangu anafanya na kuongea mambo ambayo hayaeleweki

Ndugu yangu anafanya na kuongea mambo ambayo hayaeleweki

Mpeleke hospitali acheki kwanza malaria hienda imepanda kichwani! Pia daktari wa magonjwa ya akili na afya ya ubongo amcheki huenda pia anasumbuliwa na msongo wa mawazo aka depression.
 
mshale huyo kapigwa,kabla ya base ktk hili kaa nae muulize vizuri,Kama ameiba haki ya mtu,akwambie ukweli ujue unaanzia wapi kumsaidia.
 
Iliwahi kunitokea kipindi cha nyuma kwakuwa walidhani ni matumizi ya pombe nilipelekwa sober house ilhali mambo yaliendelea vilevile mpaka nilipomaliza miezi minne ndipo nilipoanza kupata nafuu
Uliponaje mkuu?
 
Habari za wakati huu wana JF wenzangu. Washiriki wenzangu wa kila hali.
Leo na mimi nimepata tatizo, tena kwa ndugu yangu, tena ninayekaa nae nyumbani kwangu.
Tatizo analolipitia ni anasikia SAUTI za watu zikimuita akiwa ndani, anasikia magari yanakuja nyumbani, anataja polisi wanakuja, mara watu. Asubuhi ya leo alisema kuna muda kamuona mtu ambae sisi hatumuoni, hadi muda huu ni mtu wa hivyo.

Ila ni kijana smart mwenye kazi yake. Ameshindwa hata kufika ofisini. Inshort ni mtu wa mawazo hadi muda huu.
Sasa embu mnipe msaada wa mawazo kwenye hili. Maana mimi kwangu naona kama naliweza ila naona hali inayoendelea ni ile ile. Nimekaa nae toka asubuhi. Nafanya ajione yupo kwenye dunia ya kawaida asione amechanganyikiwa ila kiuhalisia jamaa yangu huyu amechanganyikiwa.

Muda huu sauti ya TV ipo juu ili asisikie hizo sauti. Naona inafanya kazi mbinu hiyo maana mpaka analala.
Kama uko DSM wahi Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili huku pia kama mnaamini mpeleke kwenye maombi haraka mno.

Kama ni mkristu uje PM nikupe namba za watumishi waombaji wapo DSM haraka.
 
Mpeleke hospitali akaonana na Mtaalamu Wa Afya ya Akili. Hizo ni visual & Audio hallucinations (kuona vitu/watu ambao wengine hawavioni an kusikia sauti ambazo wengine hawazisikii). Ni dalili ya ugonjwa wa kuchanganyikiwa (schizophrenia). Muwaishe hospitali mapema!
Asante Sana Umeliweka kitaalam
 
Daaaaaaah,nikiiona hii stori namkumbuka mwanangu Ngomuo,Rest Easy baba Kevin

Nae alikuwa akija ofisini anatuambiwa vitu hivhv anavyovisema huyo ndugu wa mleta mada,baadae akajirusha barabarani,Hiace ikajitahidi kumkwepa,ila tairi la nyuma likampitia mshkaji wangu akakata roho hapo hapo,ndoa zingine ni ndoano sana aisee
Poleee sana, kuna tukio kama hilo pia lilitokea Morogoro. Kijana akajirusha barabarani hiace ikampitia akafariki hapo hapo. Alikuwa ana mgogoro na mkewe.
 
Kama uko DSM wahi Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili huku pia kama mnaamini mpeleke kwenye maombi haraka mno. Kama ni mkristu uje PM nikupe namba za watumishi waombaji wapo DSM haraka.
Hao jana wamempaka chumvi ndio wamemchanganya kabisa kufikia hatua hiyo.alienda jana kwaajili ya maombezi ya kuacha pombe. Katoa jioni. Imefika saa kumi na mbili ndio kawa hivi kama kichaa tu.
 
Huyo ni mgonjwa wa akili,mpeleke kwenye kituo cha Afya kilichopo jirani.
 
Mpeleke hospitali akaonana na Mtaalamu Wa Afya ya Akili. Hizo ni visual & Audio hallucinations (kuona vitu/watu ambao wengine hawavioni an kusikia sauti ambazo wengine hawazisikii). Ni dalili ya ugonjwa wa kuchanganyikiwa (schizophrenia). Muwaishe hospitali mapema!
Halafu hii schizophrenia source yake ni Nini
 
Habari za wakati huu wana JF wenzangu. Washiriki wenzangu wa kila hali.

Leo na mimi nimepata tatizo, tena kwa ndugu yangu, tena ninayekaa nae nyumbani kwangu. Tatizo analolipitia ni anasikia SAUTI za watu zikimuita akiwa ndani, anasikia magari yanakuja nyumbani, anataja polisi wanakuja, mara watu. Asubuhi ya leo alisema kuna muda kamuona mtu ambae sisi hatumuoni, hadi muda huu ni mtu wa hivyo.

Ila ni kijana smart mwenye kazi yake. Ameshindwa hata kufika ofisini. Inshort ni mtu wa mawazo hadi muda huu.
Sasa embu mnipe msaada wa mawazo kwenye hili. Maana mimi kwangu naona kama naliweza ila naona hali inayoendelea ni ile ile. Nimekaa nae toka asubuhi. Nafanya ajione yupo kwenye dunia ya kawaida asione amechanganyikiwa ila kiuhalisia jamaa yangu huyu amechanganyikiwa.

Muda huu sauti ya TV ipo juu ili asisikie hizo sauti. Naona inafanya kazi mbinu hiyo maana mpaka analala.
Mwambie aache bange
 
Depression hizo.

Atakua anakaribia kupata bipolar disease.

Mpeleke mwananyamala wata kurefer muhimbili kuna wataalamu pale watakusaidia.

But currently unaweza mpa dawa za usingizi apumzishe akili.

Mpeleke hospital na usije kujaribu kumpeleka kwa waganga wala watu wa maombi hataharibikia huko.

Please do the need.
 
Kama uko DSM wahi Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili huku pia kama mnaamini mpeleke kwenye maombi haraka mno. Kama ni mkristu uje PM nikupe namba za watumishi waombaji wapo DSM haraka.
Maombi atapotea. Aende hospital.
 
Back
Top Bottom