Ndugu yangu anafanya na kuongea mambo ambayo hayaeleweki

Ndugu yangu anafanya na kuongea mambo ambayo hayaeleweki

Pole sana kuna jambo huenda ni zito amelifanya sasa anapata mawenge hii kauli " Polisi hao" Watu hao" kuna iisue hapo hiyo hali imemwathiri chakufanya.

Kumuone Dr. Wakati huo mpe soda hasa fanta orange, juice ya machungwa kwa wingi na maziwa fresh hii inasaidia kupambana na hali hiyo.

Kuna Ndugu yetu alipata hali kama hiyo baada ya kutoka kwenye Ugojwa ulimpelekea kuwa kwenye Corma kwa masaa kadhaa.

Baada ya kuruhusiwa aliporudi nyumbani alinza kupaata hali kama hiyo
 
Mkuu hospital na maombi mkuu. Dunia hii Kwa sasa ni changamoto Sana. Maofisini huko kuna mambo mengi Sana. Hata mitaani Tu. Hivyo unapiga kotekote. Kwa mganga tu ndiyo nasema asikanyage kabisa. Ila hospital na maombi ni tick.
Mimi nishauguza mtu wa namna hiyo.

Alikutana na wachungaji wakawa wanampoteza sijui kuibiwa nyota sijui takataka gani za majini.... Akahama akili kuona kila mtu mchawi....

Mwisho wa siku akaponea hospital na nilipiga marufuku kwenda kuombewa....

Hawa wachungaji wa sasa ni wajasiriatumbo.

Nina experience na hao watu.
 
Mimi nishauguza mtu wa namna hiyo.

Alikutana na wachungaji wakawa wanampoteza sijui kuibiwa nyota sijui takataka gani za majini.... Akahama akili kuona kila mtu mchawi....

Mwisho wa siku akaponea hospital na nilipiga marufuku kwenda kuombewa....

Hawa wachungaji wa sasa ni wajasiriatumbo.

Nina experience na hao watu.
Bora tumuombee sisi wenyewe hapa jf lakini sio kumpeleka sjui kwakina mwamposa mzee wa upako gwajima na takataka kama hizo
 
Bipolar ina dalili za hallucination?
Depression hizo.

Atakua anakaribia kupata bipolar disease.

Mpeleke mwananyamala wata kurefer muhimbili kuna wataalamu pale watakusaidia.

But currently unaweza mpa dawa za usingizi apumzishe akili.

Mpeleke hospital na usije kujaribu kumpeleka kwa waganga wala watu wa maombi hataharibikia huko.

Please do the need.
 
Kutakuwa kuna tatizo alipitia labda alivykuwa mdogo hivyo alikuwa akilifiria kwa muda mrefu mpaka leo.
Na ndio sababu ya yote hayo.

mpeleke hospitali haraka kabla hajachoka na kuamua kujitoa roho.
 
Moja ya dalili za mental illness hamna cha ushirikina wala nini.

Mpeleke hospital hizo ni hallucinations tu
 
Ukimleta kanisani kwetu atafunguliwa, wameshaletwa watu wanaofungwa hadi kamba, vichaa kabisa na wanafunguliwa.

Na ataombewa kwa jina la Yesu pekee hakuna mambo ya kishirikina kama chumvi na vingine. Jina la Yesu limekamilika lina nguvu ya kuponya na kufukuza takataka zote.

Kama hutojali karibu PM
Waongo nyie
 
Mpelekeni hospitali ya wagonjwa wa akili au kwa watu wa ushauri na saikolojia msiende kupiga ramli kaliua!
 
Watu bana! Ushauri mwiiiiiingi kumbe nyuma ya pazia wanaelewa kinachoendelea. Wengi wao ni members.
Tuwe waangalifu, hivi sasa hali ni mbaya sana sana!
 
Ukimleta kanisani kwetu atafunguliwa, wameshaletwa watu wanaofungwa hadi kamba, vichaa kabisa na wanafunguliwa.

Na ataombewa kwa jina la Yesu pekee hakuna mambo ya kishirikina kama chumvi na vingine. Jina la Yesu limekamilika lina nguvu ya kuponya na kufukuza takataka zote.

Kama hutojali karibu PM
Amina
 
Iliwahi kunitokea kipindi cha nyuma kwakuwa walidhani ni matumizi ya pombe nilipelekwa sober house ilhali mambo yaliendelea vilevile mpaka nilipomaliza miezi minne ndipo nilipoanza kupata nafuu
hhhhhhhhhhhhh chapombeee
 
Habari za wakati huu wana JF wenzangu. Washiriki wenzangu wa kila hali.

Leo na mimi nimepata tatizo, tena kwa ndugu yangu, tena ninayekaa nae nyumbani kwangu. Tatizo analolipitia ni anasikia SAUTI za watu zikimuita akiwa ndani, anasikia magari yanakuja nyumbani, anataja polisi wanakuja, mara watu. Asubuhi ya leo alisema kuna muda kamuona mtu ambae sisi hatumuoni, hadi muda huu ni mtu wa hivyo.

Ila ni kijana smart mwenye kazi yake. Ameshindwa hata kufika ofisini. Inshort ni mtu wa mawazo hadi muda huu.

Sasa embu mnipe msaada wa mawazo kwenye hili. Maana mimi kwangu naona kama naliweza ila naona hali inayoendelea ni ile ile. Nimekaa nae toka asubuhi.

Nafanya ajione yupo kwenye dunia ya kawaida asione amechanganyikiwa ila kiuhalisia jamaa yangu huyu amechanganyikiwa.

Muda huu sauti ya TV ipo juu ili asisikie hizo sauti. Naona inafanya kazi mbinu hiyo maana mpaka analala.
Hiyo kitu inaitwa hallucination,aende hospitali atapatiwa matibabu.
 
Back
Top Bottom