Ndugu yangu na wengine sita wakamatwa usiku wa manane wakihisiwa kujifunza ugaidi na hatujui waliko hadi sasa

Kama walimkata kama unavyodai ulijuaje kwamba anatuhumiwa kujifunza ugaidi? Wewe unatakiwa uisaidie polisi
 
Ila hii nchi ya ajabu unaenda kumvamia mtu unamchukua ndugu zake hawajui alipo.Akifia mikononi mwenu mtajibu nini?Ndio maana wengine kwenye hizo kazi wanakufaga vifo visivyoeleweka sababu zinakuwaga hizihizi
 
Poleni! Wafuatilie vituo vya polisi, mkuu wa wilaya/mkoa n.k.
Kila siku haya mambo yanaongelewa Maria spaces, nafikiri WaTz hawajali ni mpaka mtu yampate.
 
kma una ndugu dar waambie waende police pale Tazara watawapa ripot yote
 
Mungemuonya huyo kaka yenu kwanza kwa tabia zake, naona unasema hayo yote kisa ni kaka yako, wacha vyombo vya usalama vifanye kazi yake.
 
Tafuteni picha yake wekeni mitandaoni.
Sambazeni taarifa zao mitandao ya kijamii.

Pelekeni malalamiko yenu vituo vya polisi.
Nendeni kwa wakuu wenu wa dini wawasaidie kuwatafuta wapendwa wenu katika imani, sio mnatoa sadaka tu halafu kwenye majanga wanawaacha.
Waombeeni wawe salama.

Kamata kamata kipindi cha jpm ilienda na wengi sana, wiki mbili sio nyingi sana huwa wanakaa nao kwa muda kiasi.
 
Poleni! Wafuatilie vituo vya polisi, mkuu wa wilaya/mkoa n.k.
Kila siku haya mambo yanaongelewa Maria spaces, nafikiri WaTz hawajali ni mpaka mtu yampate.
Maria spaces ndo nini
 
Huwezi kukamatwa hivi hivi lazima uwatakuwaa na connection
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…