Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

Kazi wanayoipenda vijana Saiv ni kua CHAWA na Roll modo wao ni BABA LEVO na MWIJAKU ukute uyo ndugu yako anasubiria iyo nafasi manake Baba Levo juzi alisema htki tena kua CHAWA
 
Una moyo mzuri sana kulingana na Dunia ilikofikia
Ingekuwa mm ningesitisha kumpa hiyo 50 then natulia tu watu wengi sana wanashindwa maisha sababu ya majivuno na kujisikia kuwa amesoma chuo wakati fursa zipo nyingi tu Hana shukrani
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi.

Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k, kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Masihara haya mkuu.
umefuga mbwa mwenyewe halafu anakubwekea bwekea.

mwishowe atakutoa damu.
 
Wewe ndio umemkosea kwa kumpatia 50 kila wiki il-hali pahala pa kulala na kula papo. 50 kwa wiki bila kazi ni mshahara mzuri
 
Mimi nina rafiki yangu wa tangu chuo yeye alianza kupata mishe kabla yangu alikua anapiga kazi Fanikiwa.

Baada ya kama miaka miwili akapigwa chini akawa anafanya kazi za hapa na pale kipindi chote hicho tunatiana moyo tu, sasa mwaka huu mwanzoni akaniambia anadaiwa kodi na hana mchongo ile ishu ikanigusa kwakua mimi kama wa kiume naelewa hizo ishu.

Wiki mbili zilizopita kuna binti akaniconnect na ofisi fulani hivi ni Microfinance. Nikaenda kupiga interview kati kati ya maongezi nikamuambia jamaa wa usaili kwamba nina rafiki yangu ni mzuri sana katika hii ishu yenu coz kapiga sana kazi Fanikiwa.

Jamaa akanipa contacts nimpe mshkaji waongee. Nikampanga mshkaji wangu nikamuambia na mshahara (250K) akaniambia anamcheki mshkaji.

Kesho yake akaniambia amefikiria ameona hana haja na hiyo kazi, jamaa nilimmind coz mi nimepiga krosi kisha analeta drama. Nikamjibu sawa mzee haina shida. Nimeazimia kwamba hata itokee ishu gani siwezi kumwambia jamaa.

Before u go on a rant. Yes 250 ni ndogo lakini kipi bora sasa?
 
Unamlipa 50,000 kwa wiki kwaajili ya uwepo wake nyumbani kwako.
Kwa mwezi inakuwa 200,000 na point af unataka akafanye kazi mshahara sh 300,000 Upo serious kweli?
Yupo sahihi, Ameona bora akomae hapo hapo home kwa mshahara wa 200,000.
Halipi nauli wala dharula nyingine
 
Mtafutie mume akalelewe vizuri,otherwise atamla mkeo kwa jinsi unavyojifanya unampenda sana.
 
Mimi nina rafiki yangu wa tangu chuo yeye alianza kupata mishe kabla yangu alikua anapiga kazi Fanikiwa.

Baada ya kama miaka miwili akapigwa chini akawa anafanya kazi za hapa na pale kipindi chote hicho tunatiana moyo tu, sasa mwaka huu mwanzoni akaniambia anadaiwa kodi na hana mchongo ile ishu ikanigusa kwakua mimi kama wa kiume naelewa hizo ishu.

Wiki mbili zilizopita kuna binti akaniconnect na ofisi fulani hivi ni Microfinance. Nikaenda kupiga interview kati kati ya maongezi nikamuambia jamaa wa usaili kwamba nina rafiki yangu ni mzuri sana katika hii ishu yenu coz kapiga sana kazi Fanikiwa.

Jamaa akanipa contacts nimpe mshkaji waongee. Nikampanga mshkaji wangu nikamuambia na mshahara (250K) akaniambia anamcheki mshkaji.

Kesho yake akaniambia amefikiria ameona hana haja na hiyo kazi, jamaa nilimmind coz mi nimepiga krosi kisha analeta drama. Nikamjibu sawa mzee haina shida. Nimeazimia kwamba hata itokee ishu gani siwezi kumwambia jamaa.

Before u go on a rant. Yes 250 ni ndogo lakini kipi bora sasa?

Dah kama huna ishu kabisa bora hiyo 250
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi.

Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni kama laki 3 na elf 30 hivi, pia kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15..kuhusu chakula cha mchana na maji kipo, kinapikwa nyumbani gari inaleta ofisini.. kasoro jumamosi tu.

Hii ni fursa nzuri kwake hasa ukizingatia atakuwa na uhuru wa kutosha akijipangia sehemu yake, hasa ukizingatia bado ni kijana,.mfano hapa kwangu ni marufuku kuingiza binti, saa moja geti linafungwa, n.k.

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Elimu ya Chuo aweke pembeni achape KAZI, ikiwa hataki achana nae.
Hii kitu huwasumbua sana vijana wengi wanaohitimu Chuo
 
Nimepanic (hapa msomaji weka tusi lolote utaloona linamfaa huyo kiazi)

Kila siku humu nazungumzia swala la kujali muda,,, halafu huyo mpuuzi anaona bora kushinda na remote huku akichati ,, kuliko kuamka na kwenda kutafuta mkate wa kila siku.....

Bichwa lisilo na akili, ni adhabu kwa miguu.
 
Kuna watu wataamini kwamba unasema kweli
Mkuu inaelekea huwajui vizuri vijana wa siku hizi.

Mimi binafsi nilishawaunganishia kazi vijana wawili kwa nyakati tofauti na wote wakazikataa kisa wanadai mshahara mdogo.

Kazi zenyewe ni ile mtu anakuja anakuambia aisee kwenye kampuni yangu nahitaji kijana mwenye sifa hizi, unaweza kunisaidia? Unampeleka kijana hakuna cha interview wala nini anapewa mkataba anaupiga chini! Kazi yenyewe ya ofisini.

Kijana wa sasa anaona bora kulala sebuleni akiangalia TV, kuliko kwenda huko duniani kupambana. Asijue kwamba ukishakua na kazi ni rahisi sana kupata kazi nyingine kuliko ukiwa huna kabisa!
 
Back
Top Bottom