Kesho asubhi na mapema
Namba ngeni
Yeye : halloh vipi kaka mi ni frank yule jamaa wa jana.. ushaamka
Me; nimeamka mkuu habari yako.
Yeye; salama vipi mkuu mda huu ushaanza kuja nikuelekeze
Me; hapana mkuu ila sio mda nakuja
Yeye: sawa ukifika hapa majumba sita nistue nakusubiri..
Badaaaeee
Me ; kaka kaka nishafika
Yeye:; njoo mpaka huku mwisho wa mwendokasi
Me; sawa kaka nakuja.
Kidogo nakutana na kijana smart kachomekea na kunipokea kwa bashasha la tabasamu..
Yeye; karibu kaka karibu sana
Me; aaaah ahsante ndgu yangu nishakaribia aiseee...
Tunaanza kutembea .. naona nakutana na watu wengi alafu wana kama vipeperushi.. hapo kitaa chekundu kilicheza kichwani nikaona kabisa hapa leo nitatukana mtu.
Kufika sasa...
Mama mmoja; frank nilikuambiaje kuja na mgeni mda kama huu mbona kachelewa hivi aujui mwisho saa tano
Yeye: hapana bahati mbaya ila kashafika
Mmama; haya anza kumuelekeza akitoka hapo aje huku
Yeye: sawa
Darasa likaanza kachukua peni na kuanza kunipa darasa....
Ahahahaha mimi kimoyo moyo nasema "" hawa *** kweli an yale yale niliyokutana nayo mbezi ngoja tuone"""
Akaanza kutoa darasa kidogo
Yeye;; aaaah karibu sana
Fundi manyumba hapa kiufupi tunajihusisha na tiba hasili/tiba lishe..
Wewe hutouza dawa ila wewe kazi yako itakua ni kupeleka hivi vipeperushi kwa watu ili watumie dawa zetu.
Mshahara upo hivi ukiwa daraja la kwanza utapata ....
Ukiwa daraja la pili utapata.....
Ukiwa daraja la tatu utapata...
Uki..... Daraja la 10 unapata nyumba na gari.
Ila pia ukiwa na team yako ya watu 6 na wao wakaleta sita wewe unakua una daraja la....
Kamisheni inapanda mpaka daraja la.....
* Jamaaa. Akaanza kuandika na formula za * pale *** yuleeee mi namchora tuu ....
Mwisho akasema kujiunga ni elfu 72 ila hata kama nina 30 naweza toa nyingine wataongezea wao
Ila all in all jamani tutafute pesa aiseeee yaani watu wanapendeza ila kichwani ni utapeli tuuu facvken sana