covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,355
- 20,792
Natumaini mpo salama. Nimeamua kuleta changamoto yangu hapa kwenu kwa sababu jamii forum ni kama familia, na mara nyingi tumekuwa tukishirikiana na kusaidiana katika nyakati tofauti.
Mimi ni mjasiriamali ninayejiendesha kwa kazi ya bajaj, ambayo ndiyo tegemeo langu kuu la kipato kwa ajili yangu na familia yangu. Kwa sasa nimekutana na changamoto kubwa: bajaj yangu imeharibika vibaya na haiwezi kabisa kukaa barabarani.
Hali hii imenifanya nisimamishe kazi, na kadri muda unavyoendelea ndivyo hali ya maisha inavyozidi kuwa ngumu.
Ili niweze kurudi kazini, nahitaji kufanya service kubwa ikiwemo kubadili block, mkono, oil pamoja na malipo ya fundi na gharama nyingine ndogo ndogo.
Gharama zote kwa ujumla ni takribani Tsh 350,000/=. Kiasi hiki, kitawezesha bajaj kurudi barabarani na mimi kuendelea na shughuli zangu kama kawaida.
Kwa sasa sina sehemu wala njia nyingine ya kupata fedha hizi, ndipo nikaona nije niombe msaada kwenu ndugu zangu.
Msaada unaweza kuwa kwa kunikopesha fedha taslimu au hata kulipia moja kwa moja gereji gharama za service kwa makubaliano tutakayokubaliana kwa pamoja. Hata ushauri wa kunijenga nao nitauthamini sana.
Naomba kwa unyenyekevu sana msaada wenu, maana hali ni ngumu na kuchelewa zaidi kutazidi kuniumiza mimi na familia yangu. Mwenyezi Mungu awabariki sana wote mtakaoguswa kusaidia au kushauri.
Asanteni sana kwa mtaoguswa na hali hii. 🙏🏽
Ninaishi dar es salaam.