Ndugu zangu, naomba msaada wenu – tegemeo langu la kipato limesimama

Ndugu zangu, naomba msaada wenu – tegemeo langu la kipato limesimama

Status
Not open for further replies.
Katika maisha usikubali adui wakk ajue hali yako ya maisha, katika vita mkiona chakula kina wakaribia kuwaishia kula kidogo kingine utupe jalalani ili madui wako wavita wajue kwamba huyu jama iko vizuri anachakula cha kutosha mpaka kingine anatupa jalalani....hizo ni mbinu za vita sio kuharibu, mkuu komaa tu mIsha sio mepesi kihivo.
Watoto wa siku hizi wako bize na mitandao tu, anakuja kuomba laki tatu Jf inamaanisha hana ndugu, majirani, familia kazika wote kabaki pekeake, madereva wenzie je???? Au hana hata kitu cha kuuza ndani ili akirekebishe "chanzo cha mapato".. Angeanza na hiyo simu aliandikia uzi hapa.
 
wanaumme kamiri ni pale unapo pambana na changamoto za maisha yako bila kujitanganza au kuonyesha udhaifu wako.......wanaume tunapitia mengi zaidi ya hayo ila tunaficha.
Wew huwa unatatua shida zako bila kutegemea wengne? Maisha watu hatulingani, na changamoto tunazopitia zinatofautiana, uwe mwelewa!
 
JF ukitaka ugomvi na member anza kuomba pesa..!!

Kuna uzi wa kuwachangia mods na pipo zimegoma hadi wakaanza kutupiana shit sembuse wewe unayetaka pesa ya kutengeneza bajaji yako?

Hapa jiandae kula vichambo, stress za ada zote watakumalizia wewe 😹😹😹
 
Watoto wa siku hizi wako bize na mitandao tu, anakuja kuomba laki tatu Jf inamaanisha hana ndugu, majirani, familia kazika wote kabaki pekeake, madereva wenzie je???? Au hana hata kitu cha kuuza ndani ili akirekebishe "chanzo cha mapato".. Angeanza na hiyo simu aliandikia uzi hapa.
Mtu kajiunga jf 2014 una mwita mtoto?

Kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na changamoto, maisha yana mbilinge nyingi sana , ukiwa unaona umeyapatia wewe , usione walio feli ni wajinga

Ni rahisi sana kupata msaada kwa watu baki,kuliko hao ndugu jamaa na marafiki kwa maisha yetu wamatumbi.
 
Hiyo ya bajaji sio ya kuficha hasa ukizingatia humu hatujuani mpe tu solution nini cha kufanya kama huwezi muazima pesa
Kaweka namba zake za simu zenye majina yake sio anonymous tena, tena hapa jf anaomba msaada sio ushauri, ila akajusahau kwamba jf haina forum ya bima ya vyombo vya moto au mikopo ya dhalura tuna ushauri na mawazo, kutokana na uzoefu wetu.mbalimbali.
 
JF ukitaka ugomvi na member anza kuomba pesa..!!

Kuna uzi wa kuwachangia mods na pipo zimegoma hadi wakaanza kutupiana shit sembuse wewe unayetaka pesa ya kutengeneza bajaji yako?

Hapa jiandae kula vichambo, stress za ada zote watakumalizia wewe 😹😹😹
Ila sio poa kwa wanachokifanya ,mtu mpaka kuja kuomba msaada humu ni kwamba ka kwama kweli.
 
Mtu kajiunga jf 2014 una mwita mtoto?

Kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na changamoto, maisha yana mbilinge nyingi sana , ukiwa unaona umeyapatia wewe , usione walio feli ni wajinga

Ni rahisi sana kupata msaada kwa watu baki,kuliko hao ndugu jamaa na marafi kwa maisha yetu wamatumbi.
Mkuu.. Wewe ukiwa na shida na hela ya kutengenezea chombo chako cha barabarani utakuja kuomba huku???

Unashida ya kifamilia imekutinga vibaya mno, utakuja juomba msaada huku???

Kwakifupi shida yoyote ya kipesa, utakuja kuomba msaada huku???

Naomba unijibu kwa uaminifu kabisa.
 
Alafu hizo kauli za "Ukiona wewe umeyapatia, ukiona wewe umejipata" hua zinaleta matabaka yasiyo na kichwa wala miguu.. Nani kajipata?????? Ilikuaje akajipata? kwamba alijipoteza au???

Hili jukwaa tukishindwa kujengana kisaikolojia tutajikuta tumekuwa kama tiktok, sio mida zitaanza challange humu.

Wote hali zetu ni zilezile, harakati za mtu mweusi tunazijua na tunazipita. Tunakumbushana tu wanaume wanaishi kwenye misingi gani. Aache kuanika matatizo yake hovyo, anaweka na namba zake za simu kudadeki. Kama kawahi kuwatukana wenyewe hivi ndo amefungua mlango wa kuacha kula ugali kwa amani.

Hata hivo mwamba anajiweza kiuchumi, ghalama ya kununua bajaji nadhani unaijua, si chini ya 11m. Unajua vitu vingine havileti mantiki kabisa
 
Mtu kajiunga jf 2014 una mwita mtoto?

Kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na changamoto, maisha yana mbilinge nyingi sana , ukiwa unaona umeyapatia wewe , usione walio feli ni wajinga

Ni rahisi sana kupata msaada kwa watu baki,kuliko hao ndugu jamaa na marafi kwa maisha yetu wamatumbi.
BRO MIN MEE UNA UMRI GANI? UNAKIPAWA KIKUBWA SANA CHA KUONA JAMBO NA KULIPIMA, HII ID NI YA KITAMBO SANA NMEIKUTA HUMU MIAKA CHA KUSHANGAZA WATU WANABEZA KWA KWELI MAISHA HAYA, INA MAANA SAKATA LA MKUBWA FELLA HALIJA TUSAIDIA TU BADO, HUYU MTU ALITAKIWA ASAIDIWE SI KUMKEJELI HAWA NI MEMBER WANAOPASWA KUHESHIMIWA SANA ILA HUMU NA MASHAKA SANA WATOTO WENGI HII NDO CHANGAMOTO ILIOPO HUMU
 
Mkuu.. Wewe ukiwa na shida na hela ya kutengenezea chombo chako cha barabarani utakuja kuomba huku???

Unashida ya kifamilia imekutinga vibaya mno, utakuja juomba msaada huku???

Kwakifupi shida yoyote ya kipesa, utakuja kuomba msaada huku???

Naomba unijibu kwa uaminifu kabisa.
Nitakuja kuomba ndio , pale inapobidi kufanya hivyo.

Kwanini nipate shida na watu wenye moyo wa kusaidia wapo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom