Ndugu zangu, naomba msaada wenu – tegemeo langu la kipato limesimama

Ndugu zangu, naomba msaada wenu – tegemeo langu la kipato limesimama

Status
Not open for further replies.
BRO MIN MEE UNA UMRI GANI? UNAKIPAWA KIKUBWA SANA CHA KUONA JAMBO NA KULIPIMA, HII ID NI YA KITAMBO SANA NMEIKUTA HUMU MIAKA CHA KUSHANGAZA WATU WANABEZA KWA KWELI MAISHA HAYA, INA MAANA SAKATA LA MKUBWA FELLA HALIJA TUSAIDIA TU BADO, HUYU MTU ALITAKIWA ASAIDIWE SI KUMKEJELI HAWA NI MEMBER WANAOPASWA KUHESHIMIWA SANA ILA HUMU NA MASHAKA SANA WATOTO WENGI HII NDO CHANGAMOTO ILIOPO HUMU
Asante sana , japo Sio kila wakati nakua makini, yeah watoto ni wengi mno.
 
JF ukitaka ugomvi na member anza kuomba pesa..!!

Kuna uzi wa kuwachangia mods na pipo zimegoma hadi wakaanza kutupiana shit sembuse wewe unayetaka pesa ya kutengeneza bajaji yako?

Hapa jiandae kula vichambo, stress za ada zote watakumalizia wewe 😹😹😹
Hahahaha jf mtu akisaidia ni kumi katika mmoja watu wa humu makauzu sana....

Binafsi nimepitia msoto mkali mno so naelewa mtu kuja JF na kuomba msaada, bado najitafuta ila nikikaa sawa na kuwa na kipato kizuri Mungu akitia baraka zake nitashika watu wengi sana mkono wenye uhitaji, kuna baraka sana kusaidia watu...ukimsadia mtu mwenye shida ya kweli anakuona kama Mungu wake wa pili.

Picha linaanza uzi wa kulia njaa mods hua wanapita nao ana bahati huyu nashangaa huu uzi bado upo.
 
Alafu hizo kauli za "Ukiona wewe umeyapatia, ukiona wewe umejipata" hua zinaleta matabaka yasiyo na kichwa wala miguu.. Nani kajipata?????? Ilikuaje akajipata? kwamba alijipoteza au???

Hili jukwaa tukishindwa kujengana kisaikolojia tutajikuta tumekuwa kama tiktok, sio mida zitaanza challange humu.

Wote hali zetu ni zilezile, harakati za mtu mweusi tunazijua na tunazipita. Tunakumbushana tu wanaume wanaishi kwenye misingi gani. Aache kuanika matatizo yake hovyo, anaweka na namba zake za simu kudadeki. Kama kawahi kuwatukana wenyewe hivi ndo amefungua mlango wa kuacha kula ugali kwa amani.

Hata hivo mwamba anajiweza kiuchumi, ghalama ya kununua bajaji nadhani unaijua, si chini ya 11m. Unajua vitu vingine havileti mantiki kabisa
Basi sawa
 
wanaumme kamiri ni pale unapo pambana na changamoto za maisha yako bila kujitanganza au kuonyesha udhaifu wako.......wanaume tunapitia mengi zaidi ya hayo ila tunaficha.
Zaman nilkuwa wa kulilia watu hasa ndugu zangu,mim ni wa pili kuzaliwa afu nmezaliwa na wasichana tu ila wapo vzur kiuchum

Siku moja dogo langu anaenifata alisema mwanaume anatakiwa kuwa muscurality au muscular mpaka leo nakumbuka hyo sentens

Toka siku hyo niliamka na kuamin hapa dunian nipo peke yang na ntapambana mwenyew
 
Kaweka namba zake za simu zenye majina yake sio anonymous tena, tena hapa jf anaomba msaada sio ushauri, ila akajusahau kwamba jf haina forum ya bima ya vyombo vya moto au mikopo ya dhalura tuna ushauri na mawazo, kutokana na uzoefu wetu.mbalimbali.
Bado hatuna uhakika kama hiyo namba aliyoweka kasajili kwa majina yake halisi kwahiyo bado sio halisia

Shida ni ya kila mtu ukipatwa na tatizo litoe kwa wadau huenda ukapata msaada kifedha au ushauri
 
Hahahaha jf mtu akisaidia ni kumi katika mmoja watu wa humu makauzu sana....

Binafsi nimepitia msoto mkali mno so naelewa mtu kuja JF na kuomba msaada, bado najitafuta ila nikikaa sawa na kuwa na kipato kizuri Mungu akitia baraka zake nitashika watu wengi sana mkono wenye uhitaji, kuna baraka sana kusaidia watu...ukimsadia mtu mwenye shida ya kweli anakuona kama Mungu wake wa pili.

Picha linaanza uzi wa kulia njaa mods hua wanapita nao ana bahati huyu nashangaa huu uzi bado upo.
Kila mtu ana changamoto zake na wengi humu JF njaa kali ni vile hatuonani live tungechekana sana..!! 😹😹😹

Mtu 24/7 yuko JF anazurula km paka la bar ila umkute anavyojifanya ana pesa utacheka uzimie..!! 🤣😹
 
Naona mitazamo ya watu wengi humu ni tofauti na nilivyofikiri..

Jamii forum ni sehemu ya maisha yangu nilijiunga toka nipo form 5 back way huko hadi sasa tuna mafamilia sijawahi kuiacha pengine ni mtandao wangu pendwa sana kuliko mingine. Ndio maana pia nimeona niletejambo langu huku... kupitia jamii forum kuna watu walipata kazi za ndoto zao na wengine wengi walipata misaada na pia wapo waliotapeli watu humuhumu.. yote hayo ndio maisha yenyewe.

Kuna wenye mtazamo hasi na mtazamo chanya yote ni sawa maana mwenye shida ni mimi na lazima nitaitatua tu ikishindikana huku nitatafuta alternative nyingine hadi nikamilishe..
 
Watu wenye utu wapo wengi tu, japo inaonekana kama hawapo.
Nyie mnauvua utu wenu wenyewe. Upo tayari kuyatoa ya sirini kisa watu wakupe hela.. Apo unakua umevua utu wako mwenyewe. Nisawasawa ubakwe alafu unajitokeza kwa kila mtu kutangaza umebakwa.. Ndomaana hata vyombo vya habari hua wanafuta picha na wakati mwingine mpaka majina yanafutwa kama wanatoa habari ya kuutweza utu wa mtu.

Sasa nyie ndugu zangu mnajitoa utu wenu ninyi wenyewe... MMENISIKITISHA SANA LEO. Ngoja nikanywe pombe tu.
 
Kwenye maisha haya kufanya makosa kwenye maamuzi ni kawaida tu
leo upo juu kesho upo chini
yote ni sababu ya kutofanya maamuzi sahihi au kujisahau tu ukiwa kwenye peak..

Km anahitaji msaada msaidieni dunia inazunguka hii huwezi jua kesho yako!
 
Nyie mnauvua utu wenu wenyewe. Upo tayari kuyatoa ya sirini kisa watu wakupe hela.. Apo unakua umevua utu wako mwenyewe. Nisawasawa ubakwe alafu unajitokeza kwa kila mtu kutangaza umebakwa.. Ndomaana hata vyombo vya habari hua wanafuta picha na wakati mwingine mpaka majina yanafutwa kama wanatoa habari ya kuutweza utu wa mtu.

Sasa nyie ndugu zangu mnajitoa utu wenu ninyi wenyewe... MMENISIKITISHA SANA LEO. Ngoja nikanywe pombe tu.
Sawa
 
Naona mitazamo ya watu wengi humu ni tofauti na nilivyofikiri..

Jamii forum ni sehemu ya maisha yangu nilijiunga toka nipo form 5 back way huko hadi sasa tuna mafamilia sijawahi kuiacha pengine ni mtandao wangu pendwa sana kuliko mingine. Ndio maana pia nimeona niletejambo langu huku... kupitia jamii forum kuna watu walipata kazi za ndoto zao na wengine wengi walipata misaada na pia wapo waliotapeli watu humuhumu.. yote hayo ndio maisha yenyewe.

Kuna wenye mtazamo hasi na mtazamo chanya yote ni sawa maana mwenye shida ni mimi na lazima nitaitatua tu ikishindikana huku nitatafuta alternative nyingine hadi nikamilishe..
Mimi nakushauri ungekuja na gia ya kuomba angalau kibarua cha kujishikiza update hiyo amount ungesaidika kwa haraka sababu umekuja na ID yako hii inayojulinana kuliko kuomba pesa direct
 
Labda alikua anatoa deiwaka.

Mie kwa kweli tuonane wabaya tu ila kukupa chombo yangu ukafosie hela ni Big no.

Kuna jamaa alikujaga kuazima gari kwa mshua eti kwa sababu alikua shemeji ake akaona shemeji hawezi kuninyima gari.

Mshua alimjibu bila kupepesa,

Gari yangu ni mke wa pili, sasa siwezi kukuazima mke wangu ukamtumie unavyotaka wewe.
Hii nilikua sijawai kuisikia mke wa piliii...

Noted
 
Kwanza kukosa sio ujinga wala kupata sio ujanja,ni harakati za maisha ya mtu mweusi,changomoto ni sehemu ya maisha,wale wote ambao wamewahi kupitia msoto na mimi nikiwa mmoja wapo,tunajua inakuwaje ukiwa umechacha

Watu mmetoa lawama nyingi sana,kwanini Bajaji haijajiwekeza mpaka inakufa,kiukweli vifaa vya moto vina changamoto nyingi sana,tena ndio uwe hauna source nyingine ya income,polisi hawaja kulamba road,kuna ajali za hapa na pale zote hizo ni liability [hela inatoka]

Hatujui bado huenda kuna mkopo anarejesha hiyo nayo ni liability au matumizi au mahitaji ni makubwa kiasi kwamba kipato hakitoshi hata kusave

Tunaweza kuzungumza mengi hapa,lakini changamoto zipo na kwa kila changamoto ni somo ambalo tunajifunza

Niwaombe huyu mwamba ni mwanafamilia mwenzetu,ingekuwa ni I'd mpya huenda tungekuwa na hofu,lakini hii ni I'd ya zamani hakuna sababu ya kutia shaka,just imagine hakuona haya pamoja na I'd hii maarufu lakini amejitokeza mbele yetu kama wanafamilia tumshike mkono

Please kwa mwenye uwezo wowote ule kwa utachojaaliwa let us show love kwa mwenetu, haina haja ya kuexpose number yako,just go kwa wakala hlf drop some love kwa ndugu yetu

Hautakuwa umemsaidia yeye tu ila na watoto pale nyumbani,huenda unaplan ya kwenda sehemu kula bata na familia,lkn mfikirie na mtu ambaye hajui jioni au kesho atakula nini,guys sioni aibu binafsi nimepitia msoto najua vile inavyokuwa pale ambapo hauna stable income,hata usingizi kwako ni shida,please wadau naguswa na hili najua mwenetu anapitia wakati mgumu sana kwa mujibu wa maelezo yake na amesema kadri siku zinavyo zidi kwenda hali inakuwa mbaya

asante.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom