kwanza fanya kuanza kuondoa sumu ya unachokula , anza kula vyakula vyenye kukupa afya bora kuanzia asubuhi mpka jioni anza tartbu mpaka uzoee, asubuhi kula mboga mboga, maziwa, na kiazi/gimbi/ndizi/ usiweke vyakula vya mafuta mengi au wanga uliokobolewa, mchana unaweza kupata mlo wako kwa kiasi kama unakula sanaa punguza kiasi cha chakula usisahau matunda na mbogamboga kwenye mlo wako ila mlo usiwe mwingi sana, hapa kwa mchana unawez kula ugali/wali/ndizi kwa kiasi kdgo , jioni hakikisha huli chakula chochote zaidi ya mchanganyiko wa matunda na maziwa ukiweza na mboga mboga kula, kwa mwanzo anza kula matunda ushibe maana tumbo linakuwa halijazoea kula hata sahani mbili, usisahau kunywa maji asubuhi mchana nA jioni kadri uwezavyo, kumbuka maziwa fresh kwa usiku ni kama ant depression maana yanakupa feeling ya utotoni na unapata mood ya kulala kirahisi bila mawazo yoyote, kitu cha pili ni kuondoa sumu ya kwenye akili cha kwanza kabisa ukiamka asubuhi anza kwa kumuomba Mungu na kutamka kwamba wewe ni mbarikiwa, umezaliwa ni mshindi na unashinda zaidi ya kushinda, Mungu anaishi ndani yako, kila kitu kwako kinawezekana, mpe Mungu nafasi ndani ya moyo wako, amini kuna jambo Mungu yupo tayari kukutendea leo kwenye afya, mahusiano, kazi, huduma, wabariki wengine, wafurahie wengine na anza kuona Mungu yupo upande wko ndo maana amekuokoa na kila jambo na upo hapo sio kwa bahati mbaya, jione wewe ni mtu mwenye kibali na kimstart.... kama una mziki kwako fungulia sauti isiyoweza kuwasumbua majirani anza kucheza tafuta ma amapiano ucheze, singeli kata mauno kama hujui jifunzee, cheza mziki wowote unaokuchangamsha kwa mda wa dakika 30 nk mpka uone hapa mwili mzima unatoka jasho, ukitoka hapo kujiandae uende misele kama huna kazi fanya kazi za nyumbani huku ukiendelea na imani yako Mungu ameanza kubadilisha maisha yako na chochote kinachotokea ni mpango wa Mungu kwako na anakuanda kwa jambo kubwa zaidi, pia achana na marfki ndugu wanaokufanya kujiona hufai, mnyonge, ukose amani, watoe kwenye akili na moyo wako, weka nguvu kwenye kuboresha maisha yako, hakikisha unaishi kwa amani bila wao, usifanye mtu kuwa ngao ya maish yakooo, jishughulishe na maisha yKo acha mbwembwe jifurahie, jisherekeeee jua wewe ni wa thamani sana...ukirudi jioni usisahau kucheza mziki tena, kama unaweza kukimbia kimbia ila zoezi la mziki ni zuri kwa afya ya akili, kama unaona una nguvu mda hauna kitu cha kufanya jifunze vitu online kama ni msomi jikumbushe masomo yako ya chuo uendelee kuwa bora kwenye fani yakoo.....
kwa mtiririko huo wa maisha naona kabisa ukibadilika na ukirejea kwenye tumaini kuuu.