Anxiety disorder nimepigana nayo mwaka mzima ndugu yangu. Mwanzo nilianza kupata hali za kutokujiamini, nikawa naogopa vitu nisivyovijua, mwisho nikaanza kupata panick attacks, mwanzo nilihisi ni shambulio la moyo, ila madaktari walivyoona ule mfadhaiko, increased heart rate, kukosa pumzi na kutokutulia ndio wakaniambia tatizo ni stress. Ni hali za muda mchache ila ni ngumu, maana unaona kabisa hapa nakufa. Nimejitahidi kucope na hali ila panic hainiachi. Inanitishia kila mara kiasi nayo imekuwa sehemu ya stress.